Wakristu na Waislamu wa Misri walivyosimama pamoja kuupinga Utawala wa Kifisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakristu na Waislamu wa Misri walivyosimama pamoja kuupinga Utawala wa Kifisadi

Discussion in 'Jamii Photos' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 14, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hawakukubali kugawanywa kwa misingi ya dini; hawakuwa tayari kuwekwa kwenye sanduku moja ambalo hawakutakiwa kutoka. Walijua wanasimamia nini na wanapinga kitu gani; walijua kabisa matatizo yao ya ujumla yanasababishwa na nini. Hivyo, japo vyombo vingi vya habari havikuonesha wazi sana ukweli ni kuwa wananchi wa Misri waliosimama dhidi ya utawala wa Mubarak walifanya hivyo bila kujali dini zao. Waliunganishwa na nia ya kuondoka na utawala wa kifisadi uliojikita madarakani kwa miaka thelathini.
  <table border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr class="no-border allsizes-sizes"><th>
  </th><td>
  </td><td>
  </td><td>
  </td><td>
  </td><td class="allsizes-selected">
  </td><td>
  </td><td><small></small> </td> </tr> </tbody></table> [​IMG]

  Chini kundi la vijana wa Kikristu wakiwazunguka kuwalinda Waislamu wakati wa kuswali; Jumapili yake Waislamu waliwazunguka na kuwalinda Wakristu wakiadhimisha Misa Tahrir Square
  [​IMG][​IMG]

  Wakristu na Waislamu wakishika alama za dini zao kuonesha umoja wao dhidi ya ufisadi na utawala wa kifisadi wa Hosni Mubarak

  [​IMG]

  Mmoja kashika Quran mwingine kashika Biblia - dhidi ya serikali ya utawala wa kifisadi


  [​IMG]


  [​IMG] Diverse: Egyptian Christians held mass in Tahrir Square in Cairo in order to counter claims by state television that most of the anti-Mubarak protesters are members of the Muslim Brotherhood


  Read more: Egypt protests: Hosni Mubarak turmoil 'will fuel illegal wave UK migration' warns Nato | Mail Online

  [​IMG]Hossam el-Hamalawy
  Coptic Christians and Muslims unite in Tahrir Square in Cairo, Egypt in an image uploaded to Flickr on Feb. 2.


  [​IMG]

  [​IMG]Egytpian Christians march through Tahrir Square (matthew cassel)


  [​IMG] <cite>Guy Martin</cite> Coptic Christians joined Muslim Egyptians to demonstrate unity as protesters in Tahrir Square on Sunday renewed their calls for the resignation of President Hosni Mubarak.  [​IMG]
  (Egyptians rally at Tahrir Square in downtown Cairo February 1, 2011/Amr Abdallah Dalsh)

  [​IMG]This is one of many incredible photos from a wonderful gallery published by The Guardian. Very significant.

  Here's the caption:
  Protesters hold a Christian coptic cross and copies of the Qur'an as they take part in 'Sunday of the martyrs'. Photo: Amel Pain/EPA

  My Take:
  Mbele ya utawala wa kifisadi, tofauti zetu za kidini, kikabila na kilugha hazina nafasi. Ni lazima tuungane pamoja kuupinga utawala wa mfumo wa kifisadi kwani madhara yake hayabagudi dini, jinsia, rangi, elimu au makazi! (Picha zote vyanzo mbalimbali)

   

  Attached Files:

 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,486
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hii, and this is dirrect example to our country Tanzania ambayo ishagawanywa kidini na wanasiasa
   
 3. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yuko wapi yule Zubeda aliyesema hakukuwa na umoja wa dini zote kumuondoa Mubarak ?
   
 4. W

  We can JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ningejua namna ambayo watawala wetu wasingeiona hii thread, ningeipendekeza! Itawauma sana. Mzee mwanakijiji, Tanzania kwenyewe HAKUNA UDINI. Kuna rushwa, kuna dhuruma, ufisadi, uonevu, nk. i LOVE BOTH MUSELEMS AND CHRISTIANS OF TANZANIA. Nimeguswa sana na wana wa Mungu wa Misri jinsi wanavyopendana. Yaani Waislam wanawalinda wa Kristu wasali na wa Kristu wanawalinda wenzao Waislam waswali, WAO! This is very moving....
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  misri ndio nchi inayoongoza africa kwa graduates wa sheria...

  na pengine kwa wasomi....


  sisi tatizo letu ni kuwa mbumbu,bu ni wengi mno,na ndio wabeba bendera za udini wakisha rubiniwa na wanasiasa uchwara

  safari bado ndefu...
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Natumai Muse A muse, Aswad Band, MaxShimba, Yeshua Hamelech wataipenda hii pia na kufuata mfano huu.
  Inapendeza!
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,486
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  tomaso yule !! aje hapa aone na picha kabisa
   
 8. s

  shosti JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kiza kinene:coffee:
   
 9. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna ule msemo wa 'kusoma hujui na picha pia' ?
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,486
  Likes Received: 19,879
  Trophy Points: 280
  watu siku hizi hawataki kucheka na nyani!! siku 18 watu wamekomaa tu hadi jamaa aondoke!! hii ni pumzi ya ajabu
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa aliulizwa swali pale akajibu hajaiona familia kwa wiki mbili,sisi kila jioni tunataka kuonekana kwenye grocery ya jirani wapi na wapi tutaishia kunung'unika tu.
   
 12. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimekugongea senksi baba. Mwenye macho na aone,mwenye masikio na asikie..:clap2:
  <input id="gwProxy" type="hidden"><!--Session data--><input onclick="if(typeof(jsCall)=='function'){jsCall();}else{setTimeout('jsCall()',500);}" id="jsProxy" type="hidden">
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mubarak alikuwa anadai Muslim Brotherhood ndio tatizo na kuwa wataleta udini; Wapo wanaosema Chadema ni chama cha kidini! Wanasahau kuwa mtoto wa Kikristu anapata kipindupindu kama mtoto wa Kiislamu; mtoto wa Kiislamu anafeli mitihani kama ilivyo mtoto wa Kikristu. Wakati umefika tuwashtukie viongozi wanaoleta udini ili kutugawa tusiwaondoe madarakani.
   
 14. P

  Percival JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Hili no somo kubwa kwetu. Wamisri wangehadaika na kugawanishwa basi wasingemtoa dikteta kwa siku 18 !!. Moja ya silaha kubwa ya wakoloni na madikteta ni " Divide & Rule " yaani "Tenganisha na utawale" Watu waliotenganishwa fikra zao zote zipo kujidhuru wao wenyewe na dikteta anachekelea na kukaa kwenye uongozi.

  Wakristu na Waislamu wana historia ndefu ya kukaa pamoja kwa amani kwenye nchi nyingi lakini kuna wachache wanao haribu.
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huu ni mfano mzuri wa kuigwa!safi sana wananchi wa Misri!!
   
 16. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,720
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  vema kutumia neno mpumbavu....kumuita tomaso inaweza kuwa ni udini pia.

  ni mtazamo tu usijali sana.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natumaini vijana wetu wanawez akuona kuwa kuna wakati tofauti zetu za kidini zinapaswa kuwekwa pembeni. Nilifurahii kuona Waislamu wanawazunguka Wakristu wakati wa Misa Tahrir square wakirudisha kile kilichofanywa Ijumaa na Wakristu. Na ukumbuke hawakuwa na kiongozi wa kuwaambia kuwa msifanye hivyo au fanyeni! Ilitoka moyoni.
   
 18. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Very good stuff. Hilini somo zuri sana... Nimependa MMK kwamba
  PHP:
  mtoto wa Kikristu anapata kipindupindu kama mtoto wa Kiislamumtoto wa Kiislamu anafeli mitihani kama ilivyo mtoto wa Kikristu.
   
 19. A

  ALLY KILUNGUZO SALUM Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Hili ni funzo kwa watawala wa kiafrika kama wana akili za kuelewa.misri wameonesha mfano ambao hapo awali nilidhani nguvu zimewaishia ! Hongera sana misri.huu upepo wa kuwaondoa watawala wa aina ya mubaraka ni lazima utafika huku kusini mwa afrika.
   
 20. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii imetulia kwelikweli, lakini huku kwetu watu wameshaanza kupofushwa na wanasiasa.
   
Loading...