Wakristo Wenzangu Hivi Kumchezea Mungu Ndombolo, Sebene Na Kwaito Alituagiza?

Naona wana wa binadamu kutoka italia mmefungua huu uzi kuleta mapokeo/liturujia yenu kuzuia Yesu asisisfiwe.
Mungu tumwaminiye anachezewa sana tu,Mfalme Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka,Wengine waliimba na kucheza(Waisraeli) mpaka Ukuta wa Yeriko Ukaanguka.
Maria mama wa Yesu hatumuimbii wala kumuomba maana hata yeye anasubiri siku ya mwisho.

Note:Okoka ujue mambo ya Uungu
Daudi alicheza hadi nguo zikadondoka, unajua alivaa nguo gani? Usidhani eti alivaa suruali na shati kama wewe pamoja na laizoni zako!! Alivaa lubega, sasa na wewe uje ucheze mpaka suruali yako idondoke tuone, makanisa ya Kilokole jamani mnadhalilisha Ukristo, bora kanisa libaki moja takatifu Katoliki la mitume tu
 
mimi napendaga sebene lile la usiku, full kusebeneka, jamani wokovu ni raha, hacha tule raha na watoto wa Yesu, ninyi vipi???
 
Msiponiimbia mawe yataniimbia

Mfalme Daud alivua nguo zake na kuvaa magunia alimchezea Mungu staili zote alizoweza...
Nimesahau vifungu vya bible

Kwani Mfalme Daudi Ni Nani? Je hakuwa mwanadam wa kawaida Kama sisi? Tumuige yeye Kama Nani? Kwa andiko lipi? Haya basi igeni na madhaifu Yake ya ufedhuli wa hila ya kumuua Uria vitani kisha kumchukua mkewe! Kwanza siyo Kweli kuwa Mfalme Daudi kuwa alicheza Nguo zote zikaanguka , Mwenye reference alete hapa! Haisemwi Kwa usahihi! Yatupasa kujifunza zaidi
 
Shalom Nyote!

Leo Jumapili Hii Nipo KIROHO Zaidi Ila Sitaki Ipite Hivi Hivi Bila Kutoa DUKU DUKU Langu Nililonalo Kwa Kipindi Sasa.

Hivi Sisi WAKRISTO Ni Kwamba Siku Hizi Tumepiga MAENDELEO Ya KIROHO YALIYOTUKUKA au Ndiyo TUNAMKASIRISHA Mwenyezi Mungu Tu?

Siku Hizi Ukienda Kanisani Na Labda Tu Ukiondoa Kwa Sisi WAKATOLIKI TULIOTUKUKA Basi Humo Katika Kanisa Hizo Nyimbo Za DINI Ambazo Zitapigwa Hazitakuwa Na Tofauti Sana Na Masebene Ya Ndombolo, Zitutana, Kwasakwasa, Kibindankoi Na Ekotitee.

Jamani Hivi:

  • Kukatika KIUNO Madhabahuni Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Wanacheza Sebene Hadi Wanaelekezeana Makalio Yao Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Kucheza Pale Madhabahuni Hadi Wengine WANAJAMBA Na Harufu Sometimes Sisi Tuliokaa Tunaisikia Huku Wakitokwa Na MIJASHO Ni Kupena UPAKO Huko au Kutafutiana Tu NUKSI?
  • Muimbaji au Kwaya Husika Kuvalia Nguo ZILIZOBANA KUNAKOTUKUKA Hadi Unaona Kila Kitu Kilichoumbwa Na Mwenyezi Mungu Huyo Huyo Ni HALALI Kiroho?
Yangu Ni Haya Tu WATUMISHI Wenzangu Wa KIKRISTO Na Naomba ROHO MTAKATIFU AWAONGOZE KATIKA KUNIJIBU MTAKATIFU MWENZENU NILIYETUKUKA. Bwana Yesu ASIFIWE!

Karibuni Na Hata Ndugu Zangu WAISLAMU Nanyi Pia Mnakaribishwa Kuchangia Na Kutoa Pia Maoni Yenu Kwani Naamini Wote TUNAMWOMBA MUNGU Mmoja Ni Hizi Zingine Ni Mbwembwe Zetu Tu SISI Wanadamu.
Ni observation nzuri sana mkuu.Halafu bila aibu wanatamba kwamba wanamchezea Bwana Yesu, huku wakicheza Sebene,Kwaito,Ndombolo au upuuzi mwingine,styles ambazo zimebuniwa kuzimu!! Huwezi kuhamisha mitindo kama Sebene iliyobuniwa kuzimu na kuingiza kanisani,halafu eti unasema unamchezea Mungu!That is spiritual blindness.Indirectly hiyo ni kusema kwamba Mungu ameshindwa kubuni styles za kucheza zinazo mtukuza. What they are also saying is that God is bankrupt,so we have to copy and paste Sebene.Watu kama hao au Makanisa hayo ni Makanisa yaliofirisika kiroho ambayo tamaa za mwili ndizo zinazo yatawala.We have to run away from such so called churches, hakuna kitu hapo. Neno la Mungu linasema wazi kuhusu makanisa hayo,"yana muabudu Mungu bure, lakini mioyo yao iko mbali naye,huku yakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu." Mungu anasema "tokeni katikati yao mkatengwe nao. "
 
Kwani maana ya ulokole ni nini? Naomba kusaidiwa hapo! Eti wengine unakuta wanavaa Nguo fupi Juu ya magoti halafu anasema kaokoka wadada wanavaa suluari eti nao wanasema wameokoka kijichubua, choyo , masengenyo , Bwana Yesu Kristo alisema " atakae kumfuata na ajikane kisha ajitwike msalaba wake amfuatilie" sasa Kama dada/mama unazani bado unataka kuvaa vimini yani Nguo fupi Juu ya magoti, kuvaa masuluari, kujichubua, kuvaa mawigi n.k unazani ushuhuda gani unawapa Watu ? Watu hatutaki kujikana, misalaba hatutaki kuibeba halafu eti !
 
Mungu anaangalia roho mingine niziada

Hiyo peke Yake haitoshi @ Dada! Hata Mtume Paulo alifika wakati akifundisha katika nyaraka zake alisema" Ni Kweli kikombe huoshwa Kwa kuanzia ndani lakini nje Yake nayo yapasa kuwa safi" halafu barua unaanzaje kuisoma Kama siyo nje?!
 
Mungu anaangalia roho mingine niziada
Hapana mkuu, Biblia inasema "kimtokacho mtu ndicho kiujazacho moyo wake." Hii ina maana kwamba matendo ya nje yakiwa kinyume na Mungu, hilo Kanisa au mtu huyo pia yuko kinyume na Mungu or spiritually wicked and bankrupt.Tusijidanganye ndugu.
 
Swala la mavazi ktk makanisa ni changamoto kubwa sana Siku hizi Na cha ajabu hao watumishi hawana ujasiri wa kuyakemea tena , sijui Kwa nini?!
 
Ni chungu kumeza lakini tujitahidi kumeza tu walokole ili tu jirekebishe Jamani! Kwenye Biblia Imeandikwa " mwanamke asiache kuvaa mavazi ya kujistiri "
Nacheza lakin nimevaa nguo ya heshima kwan tatizo? Nachangamsha mwili mkuu
 
Shalom Nyote!

Leo Jumapili Hii Nipo KIROHO Zaidi Ila Sitaki Ipite Hivi Hivi Bila Kutoa DUKU DUKU Langu Nililonalo Kwa Kipindi Sasa.

Hivi Sisi WAKRISTO Ni Kwamba Siku Hizi Tumepiga MAENDELEO Ya KIROHO YALIYOTUKUKA au Ndiyo TUNAMKASIRISHA Mwenyezi Mungu Tu?

Siku Hizi Ukienda Kanisani Na Labda Tu Ukiondoa Kwa Sisi WAKATOLIKI TULIOTUKUKA Basi Humo Katika Kanisa Hizo Nyimbo Za DINI Ambazo Zitapigwa Hazitakuwa Na Tofauti Sana Na Masebene Ya Ndombolo, Zitutana, Kwasakwasa, Kibindankoi Na Ekotitee.

Jamani Hivi:

  • Kukatika KIUNO Madhabahuni Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Wanacheza Sebene Hadi Wanaelekezeana Makalio Yao Ni Halali Kwa Mungu?
  • Waumini Kucheza Pale Madhabahuni Hadi Wengine WANAJAMBA Na Harufu Sometimes Sisi Tuliokaa Tunaisikia Huku Wakitokwa Na MIJASHO Ni Kupena UPAKO Huko au Kutafutiana Tu NUKSI?
  • Muimbaji au Kwaya Husika Kuvalia Nguo ZILIZOBANA KUNAKOTUKUKA Hadi Unaona Kila Kitu Kilichoumbwa Na Mwenyezi Mungu Huyo Huyo Ni HALALI Kiroho?
Yangu Ni Haya Tu WATUMISHI Wenzangu Wa KIKRISTO Na Naomba ROHO MTAKATIFU AWAONGOZE KATIKA KUNIJIBU MTAKATIFU MWENZENU NILIYETUKUKA. Bwana Yesu ASIFIWE!

Karibuni Na Hata Ndugu Zangu WAISLAMU Nanyi Pia Mnakaribishwa Kuchangia Na Kutoa Pia Maoni Yenu Kwani Naamini Wote TUNAMWOMBA MUNGU Mmoja Ni Hizi Zingine Ni Mbwembwe Zetu Tu SISI Wanadamu.
Ukienda kanisani kwa nia ya kumtafuta Mungu, yakini utamwona Mungu ila ukienda kutafuta ya shetani hakika utayaona manana shetani pia ni roho hai.

Sasa hapo ni jukumu lako mwenyewe kuwa wakala wa nani katika hizo roho, Mungu ama shetani.
 
Kuomba huku unamaovu ni kumpigia mungu makelele.omba kwa IMANI ya kiroho na si ndombolo na kwasakwasa.ipo siku kisingeli kanisani
Naomba nikushauri kitu Mkuu!

Unapomuandika Mungu muumba wa Ulimwengu basi umwandike kwa herufi kubwa, Yaani Mungu, au MUNGU na si mungu.

Ukimuandika kwa herufi ndogo, basi hata tafsiri nayo inabadilika.
 
Swala la mavazi ktk makanisa ni changamoto kubwa sana Siku hizi Na cha ajabu hao watumishi hawana ujasiri wa kuyakemea tena , sijui Kwa nini?!
They have no spiritual authority because they are spiritually bankrupt.
 
Kwani Mfalme Daudi Ni Nani? Je hakuwa mwanadam wa kawaida Kama sisi? Tumuige yeye Kama Nani? Kwa andiko lipi? Haya basi igeni na madhaifu Yake ya ufedhuli wa hila ya kumuua Uria vitani kisha kumchukua mkewe! Kwanza siyo Kweli kuwa Mfalme Daudi kuwa alicheza Nguo zote zikaanguka , Mwenye reference alete hapa! Haisemwi Kwa usahihi! Yatupasa kujifunza zaidi

Sijasema umuige daud na ndo maana hata mtume alioa mtoto wa miaka 12 hakuna anaye muiga , fuata matendo yao mema
 
Back
Top Bottom