GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,417
- 108,519
Hii kitu nimekuwa nikiiona na ikawa inanifanya nijiulize maswali mengi huku ikinikera sana na leo nimeona nitoe " nyongo " hasa kwa Wakristo wenzangu. Nilichokiaona leo Ibadani ndiyo kabisa " imenitibua ". Hivi kweli Mkristo na Mcha Mungu wa kweli umeamua mwenyewe kwenda Ibadani Kanisani unaweza kuthubutu kuyafanya haya yafuatayo?
Jamani hamjalazimishwa kwenda Kusali Kanisani kama unaona siku hiyo haupo vizuri vinginevyo mnapokuja Kusali na hayo Matendo yenu mnatukera mno Sisi Wakristo wa kweli na tunaomjua Mungu kisawasawa.
Ewe Mwenyezi Mungu nawaomba uwalaani vikali hawa Wakristo wenzangu wenye hizo tabia saba ( 7 ) hapo juu kwani wanatuharibia Imani yetu iliyotukuka kwako.
- Kutoa Sadaka na kuomba chenji kwa Mashemasi tena bila hata aibu?
- Muda wote Ibada inaendelea Wewe unasinzia huku " udenda " ukikutoka " ndomoni? "
- Nyimbo ya kusifu inapigwa " Jitu " linapiga makofi huku " limenuna " mwanzo mwisho.
- Mtu mzima kabisa muda wa kutoa Sadaka unatoa Tsh 500/ huku umevalia Suti.
- Ibada inaendelea unachati na muda mwingine kuinama na kuongea na Simu.
- Mwanamke mzima unakaa Ibadani na " unajipanua panua " miguu yako hovyo hovyo.
- Unajitayarisha kutoa Sadaka yako " lijitu " linakuangalia " kodo " unatoa Tsh ngapi.