Wakristo wataka machinjio yao

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
maoni.jpg

Joseph Marwa Mlemavu wa macho (kipofu) Mkazi wa Bomani Mjini Tarime akitoa maoni yake ya katiba mpya katika uwanja wa sabasaba maoni yake anaomba katiba mpya iwajali watu wenye ulemavu ,iweke wazi kutumika kwa lugha ya alama vyuoni ili watu wanapokuwa watumishi wa Serikali wawasaidie watu wenye ulemavu wakati wanapohitaji huduma za kijamii kama za afya(mawasiliano mazuri) picha na Dinna Maningo
Na Fredy Azzah (email the author)

Simiyu

BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya Busega wametaka kuwepo na machinjio ya Wakristo peke yao kwani hivi sasa wanapa shida wanapochinja mifugo yao ambayo wakati mwingine hukamatwa.

Wakitoa maoni kwenye kata mbalimbali juu ya uandikwaji wa Katiba mpya, walisema kutoka na kutokuwepo kwa machinjio ya Wakristo, baadhi ya maduka ya nyama yamekuwa yakichomwa kutokana na kudhaniwa yanauza nyama ambazo mifugo yake ilichichwa na Wakristo.

"Katiba ikubali kuwa waumini wachinje wanyama wao, tofauti na kuwa kwamba machinjio yote yameshikwa na watu wa dini moja tu," alisema Iswambula Kiswaga mkazi wa kata ya Kalemela

Pia alisema kuwa, katiba hiyo ianishe siku ya kufanyika kwa chaguzi mbalimbali ambapo siku hizo zisiwe zile za kuabudu.

"Uchaguzi uwe unafanyika kati ya siku ya Jumatatu, Jumanne, Jumatano au Alhamisi jambo analosema litaongeza idadi ya watu wanaopiga kura, tofauti na sasa ambapo maelfu wanajitokeza kujiandikisha lakini siku ya kupiga kura ya wanajitokeza wachache.

Naye Enock Kindika, alisema kuwa Rais apunguziwe muda wa kutawala, awe na vipindi viwili vya miaka miwili na siyo vipindi viwili vya miaka mitano.

Anasema kuwa, kwa muda uliopo sasa unawafanya wananchi wateseke kama walifanya makosa katika kumchagua kiongozi huyo wa nchi.

Kwa upande wa Musa Simba (18), mkazi wa Kalemela, alisema kuwa idadi ya wabunge ipunguzwe, na pia kuwafuta wabunge wa kuteuliwa na Viti Maalumu kwa kile alichosema kazi yao haionekani.

"Hata vyama vipunguzwe, tuwe na vyama viwili tu vitakavyoshindana kwenye uchaguzi," alisema.
 
Kundi la WATU wenye imani linapojitokeza kufanya kazi kama kuchinja nyama ni jambo zuri. Huu ni mgawnyo wa kazi Kama ule wa Masai kufuga na mmatengo kulima. Tushirikiane bila kugombania kazi. Wakristu wanaweza kuendelea na kazi ya kupima afya za wanyama hao hao wanaochinjwa Kama wanavyofanya sasa kwani mabwana na Bibi afya kwa karibu asilimia 90 ni Wakristu.
 
Ivi hii imekaaje? Wanaoruhusiwa kuchinja .ni maustadhi tu kwa nini?, hii ni ishu moja mbaya kabisa.
 
Hivi kuna sheria inayosema ni lazima wanyama wachinjwe na muislamu!?? au ni mazoea tu!??
 
Kundi la WATU wenye imani linapojitokeza kufanya kazi kama kuchinja nyama ni jambo zuri. Huu ni mgawnyo wa kazi Kama ule wa Masai kufuga na mmatengo kulima. Tushirikiane bila kugombania kazi. Wakristu wanaweza kuendelea na kazi ya kupima afya za wanyama hao hao wanaochinjwa Kama wanavyofanya sasa kwani mabwana na Bibi afya kwa karibu asilimia 90 ni Wakristu.
Sawa, lakini mbona Muslim anaruhusiwa kuwa bibi/bwana afya, mlokole akichinja iwe haramu kwanini, ebbo!
 
Hivi kuna sheria inayosema ni lazima wanyama wachinjwe na muislamu!?? au ni mazoea tu!??

Ukiangalia kwa haraka haraka huwezi jua kitu kilichopo nyuma ya pazia lakini kuna vitu binaendelea juu ya imani kuonekana kama kunawalio na haki zaidi ya wengine japokuwa hakuna aya katika vitabu vya kiislam vinavyosema ikichinjwa na mkristu wasile
 
Sawa, lakini mbona Muslim anaruhusiwa kuwa bibi/bwana afya, mlokole akichinja iwe haramu kwanini, ebbo!

Watu wanaongozwa na dini na wala sio matashi yao.muuza nyama haipatotizamwa kama huyu ni muislamu ama mkiristo na upipimaji wa mnyama pia hatuangalii.katika kuchinja mnyama lazima tuangalie kwasababu baadhi ya dini hata achinje mtu yeyote wanakula wala hapana tatizo kulingana na dini yao.lakini dini nyengine lipo tatizo kulingana na imani zao.hapo sio mbaya wale walionaimani ya kuchinja wao lazima wachinje wale wangine watakula.
 
Hahaha, huu ukristo wa mwilini nao una kazi. BIBLE inasema mtakula vitu vya kufisha, havitawadhuru! Na hakuna kimuingiacho mtu kimtiacho najisi. Wachinje hata kwa mashine, acheni kum-complicate Mungu.
 
Kuchinja ktk uislamu ni ibada km ilivyo ktk kila ibada yyt ktk uislamu ina mafunzo yake bali kuhusiana na suala la kula vichingo vya wakristo na mayahudi ni halali kwa waislamu kwani m/mungu ameyasema hayo ktk quruan"NA CHAKULA CHA WATU WALIOPEWA KITABU(MAYAHUDI NA MANASWARA) NI HALALI KWENU NA CHAKULA CHENU NI HALALI KWAO"kubwa ni lazima mnyama huyo achinjwe na c kupigwa rungu wala kuchinjwa kwa nyuma ya shingo yake,kuna baadhi ya watu wanasema watu wa kitabu waliokusudiwa ni wale wa zama za mtume ambao wameamini taurat,injili na zaburi ila ukweli aya haijaonyesha ni wepi aidha wale au hawa.Haya ni mambo yamekwishatolewa fatwa wala c swala la kugombana,kwahiyo akichinja mkristo au muislamu sawa.
 
da saafi kabisa halali kuliwa hijalishi nani katoa uhai wa kitoweo
 
da saafi kabisa halali kuliwa hijalishi nani katoa uhai wa kitoweo

Uislamu unafundisha hivo bwana ww kama ni muislamu ukifika maeneo ya wakristo haupaswi kuhoji hii nyama kachinja nani au hii ni nyama ya nguruwe au ya mnyama gani ww kula 2 labda ikitokea mtu akakujulisha kuwa hii ni nyama ya nguruwe usile.kubwa ukianza kula anza na kulitaja jina la mungu kisha kula.
 
Kundi la WATU wenye imani linapojitokeza kufanya kazi kama kuchinja nyama ni jambo zuri. Huu ni mgawnyo wa kazi Kama ule wa Masai kufuga na mmatengo kulima. Tushirikiane bila kugombania kazi. Wakristu wanaweza kuendelea na kazi ya kupima afya za wanyama hao hao wanaochinjwa Kama wanavyofanya sasa kwani mabwana na Bibi afya kwa karibu asilimia 90 ni Wakristu.

Kaka you made my day.
 
Uislamu unafundisha hivo bwana ww kama ni muislamu ukifika maeneo ya wakristo haupaswi kuhoji hii nyama kachinja nani au hii ni nyama ya nguruwe au ya mnyama gani ww kula 2 labda ikitokea mtu akakujulisha kuwa hii ni nyama ya nguruwe usile.kubwa ukianza kula anza na kulitaja jina la mungu kisha kula.

duh! This is new to me. Sasa mbona huwa inafanyika kisiri siri?
 
Napendekeza nchi igawanywe kuwe na nchi ya Wakristo peke yao na pia nchi ya Waislam peke yao. Mashariki/Pwani iwe ni nchi ya Waislam tu and the rest iwe sehemu ya Wakristo. Ni maoni yangu tu.
 
Hivi kuna sheria inayosema ni lazima wanyama wachinjwe na muislamu!?? au ni mazoea tu!??

hakuna alie katazwa kuchinja ni kuto jiamini kwenu tu ile ni ajila kama ajila nyingine nenda kaombe kazi kama nafasi ipo utapata ajira hacheni KUJISHUKU walaji ndio wa Amuzi watakula au namnagani vipi...
 
Back
Top Bottom