Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

diranqhe

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
889
1,000
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
 

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
804
1,000
Waongoza Misa leo walikuwa maaskofu wa Iringa na sijui wapi kule kusini, hivi Dar hakuna askofu au Pengo hana msaidizi? sijui hili limekaaje, hebu tufafanulieni mnaojua ni utaratibu gani ulitumika maaskofu wa mbali hivyo kuja Dar kuongoza ibada ili hali wa Dar au Morogoro wapo
 

kifinga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
4,562
2,000
Askofu hawezi kukufanya uende peponi bali matendo yako ukiwa hai so hata ukizikwa na katekista kama ulikua mtenda mema utaenda peponi we fikiria watu waliokufa kabla hizi dini hazijaja Tanganyika miaka ya 1,500 huko je hawataenda peponi kisa hakukuwa na maaskofu maanake dini zimekuja juzi tu
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
3,830
2,000
Waongoza Misa leo walikuwa maaskofu wa Iringa na sijui wapi kule kusini, hivi Dar hakuna askofu au Pengo hana msaidizi? sijui hili limekaaje, hebu tufafanulieni mnaojua ni utaratibu gani ulitumika maaskofu wa mbali hivyo kuja Dar kuongoza ibada ili hali wa Dar au Morogoro wapo

Yule Ngalekumtwa wa Iringa ndo mkuu wa Baraza la maaskofu TEC ( Sijui anaitwa Rais wa TEC/mwenyekiti)

Kwa maana hiyo ndio kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania
 

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,290
2,000
Yule Ngalekumtwa wa Iringa ndo mkuu wa Baraza la maaskofu TEC( Sijui anaitwa Rais wa TEC/mwenyekiti)

Kwa maana hiyo ndio kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania
Mkuu usipotoshe uma Kama huna taarifa sahihi kukaa kimya ni busara.
Mhashamu baba Askofu Ngalalekumtwa ni Askofu wa Iringa. (Rais mstaafu wa TEC)
Rais wa TEC ni Askofu Gervas Nyaisonga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom