Wakristo: Msaada wa ufafanuzi kuhusu kunena kwa lugha

Kaboom

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
10,828
14,996
Habari wapendwa..

Nianze kwa kusema kuwa sipo hapa kukashfu,kudhihaki au kuponda imani ya mtu yeyote.Nipo hapa kujifunza ..Binafsi ni Mkristo japo sipo vizuri sana kwenye mambo ya dini..

Naomba kupewa ufafanuzi kwenye mambo yafuatayo

1-Nimeona mahubiri mengi ambayo yanaongozwa kwa lugha ya kingereza na pembeni kukiwa na mkalimani anatafsiri kile muhubiri anachozungumza..Kinachonishangaza ni kuona mkalimani anatafsiri hata kipindi muhubiri akiwa ananena kwa lugha..Najiuliza hivi huyo mkalimani uwa anaelewa lugha anayoiongea huyo muhubiri kiasi cha kuweza kuitafsiri?..

2-Nimeona kwenye baadhi ya makanisa ikifika muda wa maombi utakuta Katikati ya maombi Pastor anawaambia waumini wake waanze kunena kwa lugha na wao wanaanza kutirirka..Je hii ni sahihi??..Kwa upeo wangu mdogo ninachofahamu ni kuwa..kunena kwa lugha sio kitu cha kuambiwa ufanye ukafanya..Ni mtu anajazwa nguvu ya roho mtakatifu na automatical anajikuta tu anaflow hata bila yeye kutegemea(Naweza kukosolewe pia)

3-Ukisoma kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya pili utakutana na habari ya Mitume na wanafunzi wa Yesu walivyojazwa roho mtakatifu siku ile ya Pentekoste na kuanza kunena kwa lugha za mataifa mbalimbali kitu kilichopelekea watu kushikwa na mshangao kuona mtu wa taifa jingine anaongea lugha yake(Mf:Mwenyeji wa Galilaya anaongea lugha ya Libya au Roma)..

Swali langu kwenye hili ni kuwa
i)Kwanini haiwezekani Msukuma akajazwa Roho mtakatifu then akaanza kuongea kimakonde,kizigua n.k
ii)Kwanini wengi wanaonena kwa lugha wananena kwa lugha ambayo watu hawaielewi na mara nyingi ina tone inayofanana..Sijawahi kusikia mtu ananena kinyakyusa,kirusi,Kingereza n.k..Hii imekaaje?

Naomba ufafanuzi tafadhali
 
Sikweli kwa mch.Kusema anza kunena na watu kunena.Kunena kwa lugha hutokea kama Roho atakapomjalia mtu.Hivyo lugha ya kunena roho ndio mwamzi.Pia karama ya kutafsiri haipo kwa kila mtu.Biblia inasema anenaye huinufaisha nafsi yake hivyo si kila mtu anapaswa kujua nini kinanenwa ila kama ni kwa ajili ya watu wengi ndipo hutafsiriwa.
 
Lugha ni kwa ajili ya mawasiliano.
Kama unaona mtu ananena kwa lugha mbele ya watu alafu haeleweki sio sawa.

ndio maana hao wa matendo walieleweka. Inawezekana msukuma kunena kiarabu hata kama akijui kwa mfano wa kitabu cha matendo. Ila ni ajabu kunena kisukuma uarabuni wakati wanaokusikiliza hawakuelewi
 
Hata anayenena haijui maana yake wala hajui ananena lugha gani,huo ndio ukweli halafu sasa kwanini unene mfano kirusi wakati unajua waumini hawaijui wala hukuwafundisha hiyo lugha na isitoshe hakuna anayekuelewa sasa utakua unaongea kwa faida ya nani?
 
Sikweli kwa mch.Kusema anza kunena na watu kunena.Kunena kwa lugha hutokea kama Roho atakapomjalia mtu.Hivyo lugha ya kunena roho ndio mwamzi.Pia karama ya kutafsiri haipo kwa kila mtu.Biblia inasema anenaye huinufaisha nafsi yake hivyo si kila mtu anapaswa kujua nini kinanenwa ila kama ni kwa ajili ya watu wengi ndipo hutafsiriwa.
Mkuu shtuka.hakuna kitu kunena kwa lugha isiyoeleweka kwa kua kusudio la mungu ni kila mtu alijue neno na kuyaishi ktk kweli.sasa hawa waneonao kwa lugha ni wapiga dili na waganga njaa wachumia tumbo tu.wajanja wanasanuka lakini wajinga ndio wanaingia chaka..hatareeeee
 
Sikweli kwa mch.Kusema anza kunena na watu kunena.Kunena kwa lugha hutokea kama Roho atakapomjalia mtu.Hivyo lugha ya kunena roho ndio mwamzi.Pia karama ya kutafsiri haipo kwa kila mtu.Biblia inasema anenaye huinufaisha nafsi yake hivyo si kila mtu anapaswa kujua nini kinanenwa ila kama ni kwa ajili ya watu wengi ndipo hutafsiriwa.
Mkuu mi mwenyewe hilo la kuambiwa nena na ukanena linanitatiza..Wapo watumishi wanaoenda mbali zaidi na kusema kunena kwa lugha mtu unaweza kufundishwa
 
Kwa ufupi
1.Kunena kwa lugha ni ishara ya kuwa umepokea Roho mtakatifu,
2.Kunena kwa kutoa unabii, huku ndiko kunakohitajika mtu atafsiri jambo ambalo Roho wa Mungu hunena ,kazi hii ya kutafsiri inaweza kufanywa na mnenaji mwenyewe au mtu yeyote aliyejaaliwa na karama ya kutafsiri lugha na si kila mtu aliyejawa roho mtamatifu anaweza kutafsiri.
3.Kunena kwa lugha ili kujijenga nafsi yako binafsi, mtu anaponena kwa lugha kwa ajili ya kuongea na Mungu kwaajili yake mwenyewe hapa hahitajiki mtu wa kutafsiri maana ananena mambo ya siri ambayo Mungu pekee hujua na ndipo mtu huimarika katika maisha ya kiroho na kimwili na hata uchumi pia.
Pia wapo wanenao kwa nafsi zao, yaani hunena kwa kukariri yale wanayosikia kwa watu au viongozi wao wanaponena ili na wao waonekane wamejawa na roho mtakatifu ingawa hii ni hatari ,kwani mtu huyu akiendekeza tabia hii mwisho atavamiwa na roho/pepo mchafu bila kujijua na kumfungua itakuwa vigumu.
4.Pia kuna kunena kwa mapepo na watu kwa kukosa Maarifa wakajua ni roho ananena.Nimewahi kuwatoa pepo watu wanaonena kwa lugha katika mizunguko ya huduma zangu.
Natamani ungesoma kitabu changu nilichofundisha kuhusu ROHO MTAKATIFU NA KARAMA ZAKE.
Kama utataka maelezo zaidi kuhusu karama hii ya KUNENA KWA LUGHA AU YOYOTE ILE WAWEZA NICHEK PM weka namba takupigia nikueleze kwa urefu kidogo bure
 
Sijakuelewa vizuri au?

Unasema kwamba muda mwingine hata mnenaji anaweza asijue anachokisema hispokuwa muumba wake ndiye anajua, sasa yeye anajuaje kama Mungu wake ndiye kamteremshia hayo huku haijui lugha?

Sasa kama kipawa kinamfanya mtu kutamka hata lugha asiyoijua iweje kuwe na umuhimu wa kujifunza?

Kama unanena hukijui je kama katika Lugha nyingine ni matusi au maneno ya kumkejeli Mungu wako?

Je kwasababu wengi wakinena hivyo hauna uwezo wa kujua kuwa ana kipawa/upako au roho mtakatifu waumini huamini vipi ayasemayo?

Endeleza darara hapa wajifunze namna ya kufanya hivyo mambo ya pm achana nayo
 
Hat mimi nataka kujua kuhusu hii kitu, nilishamsikia mtu anasema alifundishwa kunena kwa lugha, mi nikabaki najiuliza hii kitu unafundishwa au inatokea tu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
 
Back
Top Bottom