Wakristo/Kanisa watoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Msikiti

Makonde plateu

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
1,466
3,515
Kanisa letu la kilokole, lililopo Mafinga, limefanikiwa kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa msikiti. Hatua hii inalenga kuwaepusha Waislamu na adha ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya ibada, sambamba na kuimarisha upendo na amani miongoni mwa jamii. Kama mzee wa kanisa, nimepongeza juhudi hizi za kanisa letu.

Uwepo wa dini ya Kiislamu hapa Mafinga unatarajiwa kuchangia kuimarisha amani na upendo katika eneo letu, kwani dini ya Kiislamu ni dini ya haki na ukweli.
 
Hehehe mnakaribisha moto nyie sasa ngoja kobazi atie maguu hapo mtaimba haleluya
Kweli mkuu hapa kwetu mwaka 2004 tulikua waislamu wawili bila hata mskiti moja sasa hivi kuna misikiti zaidi ya mitano, sijui kwanini Uislamu unakua kwa kasi kiasi hicho.
 
Ni jambo jema, na litakuwa jema zaidi kama watakuwa na Ubinadamu na kujali wengine hata Wagalatia kama ninyi

Hata KKKT Usharika mmojawapo hp Arusha February mwaka huu waliichangia Msikiti 200Mil. kwaajili ya ujenzi wa Msikiti na kukamilisha mradi wa maji, tena msikiti wa Wasunni
 
"Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi."

Mathayo 6 : 3 - 4
 
Ni jambo jema, na litakuwa jema zaidi kama watakuwa na Ubinadamu na kujali wengine hata Wagalatia kama ninyi

Hata KKKT Usharika mmojawapo hp Arusha February mwaka huu waliichangia Msikiti 200Mil. kwaajili ya ujenzi wa Msikiti na kukamilisha mradi wa maji, tena msikiti wa Wasunni
Na kizuri zaidi Uislamu unafundidha binaadamu wote huzaliwa wakiwa waislamu isipo kua hubadilishwa Imani na wazazi wao, kwahiyo sio ishara kutoa waliko tokea huenda siku moja watarudi kwenye Dini yao Mama, Uislamu hufundisha kuheshimu Dini zote ila sio kujiunga nao kufanya ushirikina.
 
Na kizuri zaidi Uislamu unafundidha binaadamu wote huzaliwa wakiwa waislamu isipo kua hubadilishwa Imani na wazazi wao, kwahiyo sio ishara kutoa waliko tokea huenda siku moja watarudi kwenye Dini yao Mama, Uislamu hufundisha kuheshimu Dini zote ila sio kujiunga nao kufanya ushirikina
Watu aina yako ndiyo huwa mnaharibu nyuzi humu, na kupeleea muanze kunyukwa halafu mnaanza kulialia
 
Ubaya uko wapi, kuna mtu nimemtukana au sina uhuru wa kusema ukweli wangu, toa hisia zako kwenye uzi wa mwenzio.
 
Kanisa letu la kilokole, lililopo Mafinga, limefanikiwa kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa msikiti. Hatua hii inalenga kuwaepusha Waislamu na adha ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya ibada, sambamba na kuimarisha upendo na amani miongoni mwa jamii. Kama mzee wa kanisa, nimepongeza juhudi hizi za kanisa letu.

Uwepo wa dini ya Kiislamu hapa Mafinga unatarajiwa kuchangia kuimarisha amani na upendo katika eneo letu, kwani dini ya Kiislamu ni dini ya haki na ukweli.
Hizo hela za kitimoto hizo.
Hapo mafinga wakristo wengi wanafanya biashara ya kitimoto sijui kwanini hao waislam wanakubali kupokea vitu vya makafiri.
 
Na kizuri zaidi Uislamu unafundidha binaadamu wote huzaliwa wakiwa waislamu isipo kua hubadilishwa Imani na wazazi wao, kwahiyo sio ishara kutoa waliko tokea huenda siku moja watarudi kwenye Dini yao Mama, Uislamu hufundisha kuheshimu Dini zote ila sio kujiunga nao kufanya ushirikina.
Kwahiyo hizo dini zingine zinafanya Ushirikina?
 
Back
Top Bottom