Wakosoaji wa Falsafa ya Magufulism katika uhusiano wa kimataifa

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
WAKOSOAJI WA FALSAFA YA MAGUFULISM KATIKA UHUSIANO WA KIMATAIFA.

Dr. John Pombe Magufuli aliamini katika uhusiano wa kimataifa usio na chembe za unyonyaji, dharau na wenye usawa na staha miongoni mwa washirika wa Jumuiya za Kimataifa, Taasisi za kimataifa, makampuni ya kimataifa na wawekezaji wa Kimataifa. Dr Magufuli hakuamini kuwa Taifa la Tanzania lina sababu ya kuwapigia magoti mataifa ya Kimataifa ili kuweza kujiimarisha kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

Kuonyesha kuwa Dr. Magufuli aliamini katika kuimarisha Uhusiano na mataifa ya Kigeni alitimiza wajibu wake wa kuteua mabalozi walio iwakilisha Tanzania katika mataifa mbalimbali, na pia aliwapokea mabalozi wa mataifa ya Kigeni na kuwahakikishia mazingira Bora ya kufanya shughuri zao Nchini.

Dr. Magufuli alishiriki katika mikutano na vikao vya Jumuiya mbalimbali za maendeleo ndani Bara la Africa na Nje ya Bara la Afrika kwa kushiriki yeye mwenyewe ama kwa uwakilishi wa aliyekuwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Mawazieri wa mambo ya Nje na hata mabalozi wa Nchi husika. Mpaka umauti unamfika Dr. Magufuli alikuwa amehudumu kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC), Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) nk.

Lakini pia Serikali ya Tanzania iliyokuwa Chini ya Uongozi imara wa Dr. John Pombe Magufuli ilitoa fursa kwa wawekezaji kutoka mataifa yote Duniani kuja kuwekeza Nchini Tanzania kwa kufuata Sheria na taratibu za Nchi. Wawekezaji wote waliowekeza Tanzania kutoka mataifa ya Kigeni hawakuwahi kubugudhiwa Chini ya Utawala wa Dr. Magufuli.

Kipindi chote cha miaka mitano ya Uongozi wa Dr. John Pombe Magufuli hakukuwahi kutokea kwa matukio ya Kichokozi kati ya Tanzania na mataifa mengine yaliyopelekea kutokea kwa taharuki ya Vita ama kufunga mipaka. Katika kuthibitisha kuwa Dr, Magufuli aliimarisha ushirikano wa Kindugu na mataifa mbalimbali , mataifa mengi na taasisi za Umoja wa Mataifa zilionyesha masikitiko yake katika kipindi cha Msiba wake. Bendera ya Umoja wa Mataifa ilipepea nusu mlingoti kuonyesha kuguswa na kifo cha mwana megeuzi huyu wa bara la Afrika.
Hayo ni mambo machache kati ya mambo mengi yanayothibitisha kuwa Dr. Magufuli aliamini katika uhusiano mzuri na Jamii ya Kimataifa katika misingi ya Haki na Usawa.

HOJA ZA WAKOSOAJI WA FALSAFA YA MAGUFULISM NA UHUSIANO WA KIMATAIFA.
1. Wakosoaji wengi walimuona Dr. Magufuli kuwa amejitenga na Mataifa Mengine kwa tabia yake ya Kutosafiri kwenda katika mataifa ya Kigeni tofauti na mtangulizi wake Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa akisafiri kila mara na kupelekea kushutumiwa na Viongozi wa Vyama vya Upinzani kuwa muda mwingi ana utumia Nje ya Nchi. Mara nyingi Dr. Magufuli alijibu hoja hii kwa kusema yeye amechaguliwa na Watanzania hivyo atabaki Nchini kuwatumikia Watanzania na ziara za Kimataifa atawakilishwa na Makamu wa Rais, Mawaziri wa Mambo ya Nje na mabalozi.

2.Msimamo wa Dr. Magufuli kufuta Safari za Nje.
Katika awamu zilizotangulia kabla ya Dr. Magufuli Safari za Nje kwa Mawaziri, Manaibu waziri, Makatibu wakuu na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma ilikuwa jambo la Kawaida. Baada ya Dr. Magufuli kuingia madarakani alipiga marufuku Safari hizo kwani aliona zinatumia gharama kubwa lakini hazina matokeo chanya kwa Ustawi wa Taifa. Wakosoaji wa Dr. Magufuli waliona uamuzi huu utazorotesha uhusiano na mataifa mengine ya Kigeni.

3. Msimamo wa Dr. Magufuli Kuhusu Chanjo ya Corona (COVID-19). Baada ya Kuibuka kwa janga la CORONA ambalo lilitesa Dunia kwa kiasi Kikubwa , Dr. Magufuli alichukua uelekeo tofauti kwa kutofuata baadhi ya mambo yaliyoelekezwa na Shirika la Afya Duniani. Baadhi ya mambo Shirika la Afya Duniani lililotaka yafanyike ilikuwa wananchi kufungiwa Ndani (Total Lockdown) na pia alikataa wananchi wake kupewa Chanjo. Dr. Magufulo alisisitiza kuwa wananchi wake hawawezi kuwa sehemu ya kufanyiwa majaribio ya Chanjo ya Corona. Wakosoaji wa Dr. Magufuli ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani, wanasiasa wa upinzani na baadhi ya Viongozi wa Dini walimkosoa vikali sana kwa madai kuwa anaifanya Tanzania kuwa kama Kisiwa na hivyo ana hatarisha uhusiano wa Kimataifa.

4. Msimamo wa Dr. Magufuli kukataa Sera ya Mapenzi ya Jinsia Moja. Hii pia ilipelekea Wakosoaji wa Dr. Magufuli kuamini kuwa anazorotesha uhusiano mzuri kati ya Taifa la Tanzania na jamii ya Kimataifa ambayo ilisisitiza kuwa mapenzi ya Jinsia moja ni sehemu ya haki za msingi ya Binadamu. Wanaharakati mbalimbali wa Haki za Binadamu pamoja na baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani walipinga vikali msimamo huu wa Dr. Magufuli kwa madai kuwa utaathiri uhusiano wa Kidiplomasia na mataifa mengine. Katika kutetea msimamo wake Dr. Magufuli alisisitiza kuwa Tanzania ni Taifa la Mungu hivyo hatokuwa sehemu ya Kuunga mkono mapenzi ya Jinsia moja.

Kwa kuhitimisha ni wazi kuwa Dr Magufuli alikuwa na msimamo Mkali haswa katika Kupokea mapokea na mataifa ya Kigeni na alikuwa tayari kuvunja uhusiano na Taifa lolote ama taasisi yoyote ambayo ingetaka kushurutisha Serikali yake kuchukua maamuzi fulani.

Tukutane katika muda mwingine kuchambua zaidi kuhusu falsafa hii ya MAGUFULISM.

Josias Charles
 
Umesema sahihi na sawa kabisa, wajinga wanawaza uhusiano wa kinyonyaji ukiwauliza wakati hao mabwana zao wakiwa hawafurahishwi na yanayotokea, vp walikosa mishahara?? Mababrabara hayakujengwa?? Miradi ilisimama??ni wapuuzi kuwanyenyekea watu , muhimu ni kubeshimiana na kuhusiana kwa faida za pande zote sio kiunyonyaji
 
Dikteta akifa ni furaha kwa wananchi!
Nafikiri wale waliofanya tafiti na kuja na findings kuwa Tz ni moja ya nchi ambazo wananchi wake wanaongoza kwa kutokuwa na furaha kipindi cha utawala wa dikteta meko nafikiri warudie tena kufanya utafiti wao, mambo huku ni mukide sahivi, watu wana furaha mpaka wanaweza kuwakopesha
 
Mwendazake kafa hujapata iteuzi, sasa anza kumsifia Samia utakumbukwa

Nashangaa bado kaganda kwa Jiwe . Hajui maujanja huyu. Mjomba badili gear sasa, geuza hayo majina yasome Mama SASHA. Ila bahati yako pia mbaya, Bi Mkubwa hapendi misifa.
 
Back
Top Bottom