Wakongwe wa magari msaada tafadhali

Ntu

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
951
552
Nimeenda kwa fundi (Hapa Arusha) akaniambia gari yangu (VX-Diesel ya 2000 & Manual) imekufa vifaa vifuatavyo;

1. Booster ya Break (tatizo: ukikanyanga break gari ikiwa on inafanya kama inapiga mluzi (mpaka ukanyage na break pedal ifike nusu ya kugonga kwenye bati ndipo hunyamaza), ila break bado ipo.

2. Wishbone & 3. Torsion Bar (tatizo: anasema zimepinda na haziwezi kunyooshwa, hivyo anataka nikanunue zingine mpya). NB: hii ni tairi ya mbele upande wa kushoto.

Ushauri ninaouhitaji:
a) Una ushauri gani wakitaalamu kuhusiana na matatizo ya vifaa tajwa?
b) Kati ya Dar na Nairobi wapi nitakapoweza kuvipata hivi vifaa kwa bei nafuu? Kama ukipendekeza Nairobi, Je TRA/KRA Namanga hawataniletea shida?
c) Kwa wenyeji wa hapa Arusha: Ni sehemu gani ninaweza kuvipata hivi vitu kwa bei ya mwananchi wa kawaida? Kuna “reliable fundi” ambaye una-contacts zake ambaye anaweza akacheki matatizo tajwa na aka-confirm if it’s true or not?

cc: Preta saragossa tempid Ukwaju RugambwaYT RRONDO cabhatica Mshana Jr MANI Kaizer LEGE na wakongwe wengine. Asanteni.
 
Usihofu km hujalipeleka Gereji utawasiliana nao muda si mrefu
mcheck fundi kwa namba hizo 0754-818112
 
Ntu

Nikuulize! Ukikanyaga brake pedal engine ikiwa on inakuwaje? Inakuwa ngumu au kawaida? Unaweza kutest booster kwa kupump brake pedal taratibu gari lilikiwa limezima, mpaka padel iwe ngumu kuipress, then wanasha gari huku mguu ukiwa bado kwenye brake pedal. Kama itabonyea chini yenyewe bila kuwa ngumu, then booster inaweza isiwe tatizo hapo. Check master cylinder unaweza kuta rubber imeisha au cylinder imelika kwa ndani. So unapokanyaga pressure inatoka.

Wishbone kuipinda ni mbinde kwa hali ya kawaida. Labda ajali. Ila torsion bars zinajikunja. Na hizi unaweza kuziangalia tu mwenyewe ukajihakikishia.

Kuna jamaa yangu Arusha anauza OEM parts kwa bei nzuri. Mcheki anaweza kukusaidia. 0757 713189
 
Nikuulize! Ukikanyaga brake pedal engine ikiwa on inakuwaje?
-Inakuwa kama inakuwa free hadi ukanyage ifike nusu (yaani karibu na bati la chini ndo unapata ugumu wa breki. Na unavyokanya unasikia sauti kama mtu anapuliza kitu (phyiiiiiii.....)

Inakuwa ngumu au kawaida?
-inakuwa hakuna ugumu wowote hadi utakapokanyaga na kufika nusu pedal ndio unapata ugumu wa kuhisi umekanyaga break.

Unaweza kutest booster kwa kupump brake pedal taratibu gari lilikiwa limezima, mpaka padel iwe ngumu kuipress, then wanasha gari huku mguu ukiwa bado kwenye brake pedal. Kama itabonyea chini yenyewe bila kuwa ngumu, then booster inaweza isiwe tatizo hapo.
-Haiwi ngumu Mkuu!

Check master cylinder unaweza kuta rubber imeisha au cylinder imelika kwa ndani. So unapokanyaga pressure inatoka.
-Nitafanya hivyo Mkuu.

-NI kweli Mkuu nimeziangalia nikaona zimepinda kidogo. Je hazinyoosheki?

-Shukrani sana Mkuu.
 
RugambwaYT
 
Naomba nikushauri kama utapenda kubadili hivyo vifaa zama mwenyewe Nairobi.. Kuna spare genuine na bei ni nzuri

Jr
 
Arusha huwezi kosa spear ya hiyo vx,na kwa bei ya mwananchi.Nenda na gari mitaa ya disemba,zunguka maduka kadha ulinganishe bei na uangalie budget yako.Mafundi wapo hapo hapo wanakubadilishia.Fanya kuzungukia maeneo hayo kabla ya kwenda na gari.
 
Asante sana Mkuu kwa ushauri
 
Back
Top Bottom