Wakongwe wa CCM mnamuonea Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakongwe wa CCM mnamuonea Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KunjyGroup, Dec 18, 2009.

 1. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Aliyekuwa waziri mkuu Joseph Warioba
  Nkwazi Mhango
  INGAWA hii inaweza kuonekana kama kejeli, kuna ukweli usiopingika kuwa wakongwe wa Chama Cha Mapinduzi wanamuonea Mwenyekiti wa chama chao, Rais Jakaya Kikwete. Wanachofanya ni sawa na kumbembesha sungura mzigo uliomshinda tembo.
  Shutuma za hivi karibuni dhidi ya serikali chafu na dhaifu ya Kikwete zimetolewa kwa wakati kwa namna muafaka. Kwani wakongwe hawakukurupuka ingawa wamesahau kitu kimoja-mwenyekiti wao hakujaliwa masikio.
  Amejaliwa kinywa kipana na ujasiri wa ajabu hasa unaowashinda wenye akili. Ndiyo maana tunaona kama wanamuonea. Kumsaidia ni kuwahimiza wananchi wampumzishe. Maana mzigo umemlemea na unaweza kumuumiza.
  Hata hivyo, wakongwe hawakukurupuka. Wamemngojea Kikwete afanye vitu vyake ndipo walipomtathimini na kumpa ‘live’ tena kwa uwazi kuwa anazidi kulizamisha taifa hasa kwa kuliweka mikononi mwa mafisadi uchwara.
  Kwanza walimtaka asambaratishe mitandao iliyomwingiza madarakani kihalifu baada ya kugundua kuwa iligeuka mizigo na kikwazo kwake kufanya kazi. Kama ada, aliwapuuzia na kula jiwe.
  Sasa wanamtaka afanye maamuzi magumu ili kuinusuru nchi na utawala wake.
  Ila wamesahau kitu kimoja. Kikwete si kiongozi wala mtawala. Watani wake humuita msanii na asipinge ikimaanisha kukubaliana na sifa hii ambayo kimsingi ndiyo inayofanya kazi kwa sasa baada ya taratibu zote za uongozi na utawala kuwekwa kapuni.
  Hivyo hapa wenye kushauriwa kufanya maamuzi magumu ni wananchi hasa wapiga kura kuondokana na mazoea na kuishi kwa matumaini kama waathirika.
  Kwa wanaokumbuka Kikwete alivyokuwa akikesha akipiga kampeni hadi kuzimia kwa muda kule Mwanza akihutubia, watakubaliana nasi kuwa Rais wetu, pamoja na udhaifu mwingi, ameonyesha kipaji kimoja cha ajabu-kutosikiliza la muadhini wala mteka maji msikitini! Ni kichwa ngumu!
  Wakongwe wamesahau kitu kingine; Mwenyekiti wao ni bingwa wa kutoa ahadi na bingwa wa kutozitekeleza ukiachia mbali kuachia mambo yajiendee ilhali yeye akiwa ughaibuni akitumbua. Vijana wa mjini wanasema-kutesa kwa zamu.
  Kitu kingine walichosahau wakongwe ni ukweli kuwa wakati akijinadi, Kikwete alionyesha wazi kutokuwa na sera zaidi ya mitandao ya kuchafuana na kusaka ngawira.
  Rejea kutumia waandishi nyemelezi wajiitao waandamizi wakati si waandamizi kitu bali wadandizi na wasaka ngawira ambao wazungu husema: They can say anything for a buck.
  Ukimuondoa Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyestuka mwaka 1995, wengine walisema: ngoja yamshinde tumpe vipande vyake.
  Nyerere alijua mambo yaliyokuwa yakifanyika nyuma ya pazia kati ya Kikwete na wale wezi aliowastukia na kuwapa ‘live’ kuwa walikuwa wamejilimbikizia mali nyingi itokanavyo na ujambazi wa kisiasa na ufisadi. Kwani hamkuwaona wakiadhirika baada ya laana ya gwiji huyu kuwaandama?
  Wakongwe walisahau kuwa Rais Kikwete ni mjanja, mjuaji na mtoto wa mjini ambaye ameweza kuuingiza mjini umma na asichelee lolote. Hawakujua amejaaliwa kinywa kipana na masikio haba ukiachia mbali kutojaliwa kuona mbele hasa alama za nyakati.
  Hapa ndipo yanapoibuka madai makali ya akina Mateo Qares, Juma Nkangaa, Salim Ahmed Salim, Joseph Butiku, Joseph Warioba, Philip Mangula na wengine wenye majina na waandamizi katika chama.
  Kitu kingine ambacho wakongwe wamesahau ni ukweli kuwa CCM si yao tena. Ilikuwa yao zama zile za miiko na maadili ya uongozi.
  Ya sasa ni ya wafanyabiashara nyemelezi, walamba viatu, wapambe na mafisadi uchwara wanaouza watu na nchi yao bila kujibakiza hata wao.
  Ni ya vipofu wasiojua kesho bali leo tu ambao hawana aibu kusema kuwa Kikwete ni maarufu kuliko chama. Hivyo ni mtaji wa chama badala ya chama kuwa mtaji wake.
  Siku zote wazee ni hazina ya jamii kama watatumika vizuri. Hii ndiyo maana wameamua kumkabili Kikwete wakati huu mzuri kwa jamii na mbaya kwake-kuelekea kwenye uchaguzi
  mwakani.
  'Timing' hii ni nzuri kama itatumika vizuri hasa kwa umma kusikiliza maonyo ya wakongwe ambao hata mambo yakienda vibaya vipi hawawezi kulala njaa.
  Hawa hawasukumwi na tumbo wala utumwa wa kutumiwa na mafisadi kama walivyobainisha kusema kuwa Rais ni mtumwa wa mafisadi.
  Hawa wanasukumwa na fikra, busara na uoni wa mbali. Hawa si watu wepesi wanaoweza kununulika kwa shilingi mbili. Si watu wa kuweza kununuliwa na mafisadi uchwara waliotamalaki chamani wakimgeuza Kikwete ‘muungu mtu’ wasijue kila jambo chini ya jua lina mwisho.
  Kama alivyosema mzee Qares: Hawa hawana hasara nchi ikisambaratika. Watachomoa pasi za kusafiria na kurejea uraia wao. Hawa ni sawa na ndege kwenye mti. Ni kupe kwenye mgongo wa ng'ombe.
  Wakongwe wameamua kuwakabili mafisadi waliomzunguka Kikwete na Kikwete mwenyewe kwa kujua wazi kuwa hawa hawana ubavu wala tishio kwao.
  Kwa sababu hawana tofauti na vyangudoa ambao mara nyingi huangalia mfukoni. Unapoishiwa nao wanatoweka. Angalia walivyompiga teke Benjamin Mkapa waliyekuwa wakimuabudia. Hata Kikwete atapigwa teke siku madaraka yakiondoka mikononi mwake.
  Kuna jambo hata hivyo wakongwe wamezingatia- mfano hai wa Afrika Kusini ambapo Thabo Mbeki alipigwa chini ili kuikoa nchi na chama. Ukiangalia nchi hizi mbili zenye uhusiano wa kihistoria,
  zina mambo yanayofanana. Afrika Kusini baada ya kung'atuka baba wa taifa mzee Nelson Mandela, ilianza kuendeshwa kibabe.
  Tanzania kadhalika baada ya kung'atuka Mwalimu Nyerere mambo yakaanza kuwa shaghala baghala.
  Kuzikwa kwa Azimio la Arusha na kuzaliwa Azimio la kijambazi la Zanzibar ambalo tofauti na la Arusha halikuwa na sera zaidi ya uroho. Azimio la Arusha liliasisi sera ya ujamaa. Je, la Zanzibar zaidi ya ufisadi liliasisi nini?
  Utandawazi nao uliruhusiwa kuingia nchini bila kuwekewa vizuizi na bila kufahamu kuwa utageuka utandawizi au chambelecho Profesa Issa Shivji; 'mtandao wa wezi' umeshika kani na kuangamiza uchumi wa nchi badala ya kuuboresha.
  Maandamano ya wafanyakazi karibu katika kila sekta yameshtadi yakiakisi kutoridhishwa na sera zilizopo.
  Ahadi zinazotolewa kutotekelezeka kutokana na mazingira yenyewe kutoeleweka, hivyo maisha bora kwa kila Mtanzania yamekuwa ni ndoto.
  Je, kwa haya na mengineyo, upo uhalali wa kumlaumu Rais Kikwete? Yeye amerithi mfumo mbovu, kuurekebisha si kazi yake peke yake bali ni kazi ya Watanzania wote.
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri kama mwandishi wa makala angekuja na hoja, tuna macho na masikio. Tunachokiona kinaongea kwa nguvu kuliko vyote. Kwa mara nyingtine tunaona janja ya kutumia media divert attention.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  daaaah kweli maneno yako mazito na yanahitaji tafakari ya kina.lakini kaka yangu mtoto wa kikwere hawezi kuliona hili...ye anaona nchi iko poa tu
   
 4. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  duh najua jk hawezi on ahili wala anaeingia madarakani kama asipoacha kupewa utukufu, yani ufupi ni kuwa waliopo madarakani wanalindwa na kuenziwa , na kudanganywa km miungu watu!!so si rahisi waone na kelewa
   
 5. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama sikosei, hiyo mnamwonea iliandikwa 'mnamuonea' kwenye inverted commas.
   
 6. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kwa kweli mjomba ni ndefu mno, alafu kinachouma zaidi kwa upande wangu nimepoteza muda wote kuisoma bila ya kuelewa ulikua unalenga nini au unataka kusema nini?

  Maana umemfagilia JK, alafu ukamngo'n'ga baada ya kugeuka, na alipotoka ukamu-attack kabisa.

  Hao wazee wa chama ndio umewaita machangudoa kabisa wasio na muelekeo na wenye tamaa. Sasa hata sijui kwa kweli point yako ilikua ni hipi?

  Its OK to amuse your self by writing if you felt bored, but write some sense please if you gonna make people read.

  Sir honestly I demand an apology for wasting five minutes of my life reading this pathetic article; actually I feel robbed five minutes of my happiness.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  People,

  Hii ni satire, anaposema wanamuonea JK na kumtwisha sungura mzigo uliomshinda tembo anamaanisha JK ni hopeless, na hizi jitihada za kumshauri ni hopeless.Kitu cha muhimu ni kumuondoa tu.

  Mbona muandishi kawa clear kwenye hilo? Au kutumia neno "mnamuonea" in a satirrical form kunawachanganya watu?
   
 8. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  was there a neccesity to write over 2000 words? just to convey a simple massage haya mambo haya.

  The Headline has nothing to do with the article, our critics' summary ndio tusema if the headline was north, the article north east hiyo summary yake south. Yaani ni mtu aliesoma the first paragraph, si mlaumu jamaa anachosha mapema.
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Magazeti mengi, habari hamna, or rather waandishi hawajui kuzitafuta na kuziandika.Waandishi wanataka kufanya hekaya nyingi bila investigative journalism.

  Yaani bongo ukienda bush kuna habari kibao za kuandika, wananchi wanavyonyanyaswa unconstitutionally kulazimishwa kutembea na karatasi za kulipa kodi, kama mkoloni au South Africa under apartheid, mpaka wakina mama wanavyopata tabu kujifungua. Ni aibu, ukitaka kupata stories kama hizi saa nyingine mpaka uende New York Times ndipo unapata deep stories kuhusu nchi yetu wenyewe.Kama hatuna magazeti.

  Halafu wakipata story moja wote hiyo hiyo, hamna hata variation in coverage!

  Ukiangalia articles za magazeti yetu nyingi utaona ziko short on facts na tilalala nyingi.

  Mimi hata sijisumbui kupoteza muda kusoma hizi articles, unascan kidogo tu unaona muandishi anataka kujifanya George Bernard Shaw if not Shakespeare mwenyewe wakati hamjui hata Andanenga, achilia mbali Kafka na Goethe, unaskip, unatafuta article moja tu ya Jenerali Ulimwengu Allafrica.com anakupa mchezo wote, with facts, concepts and insiders scoop, unawaacha hawa waashi waliokosa kazi na kuvamia taaluma ya uandishi wajifunze kuchonga meza katika vichwa vya watu.

  Ukisoma articles hizi mimi simlaumu muandishi, nakulaumu msomaji, kama kuna mtu wa kulaumiwa.

  Some people actually enjoy this old testament like circuitous vogon poetry.

  Blame Mwanakijiji aliyeipopularize :).
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Labda ndio maana hatuna waandishi wenye sifa za kimataifa. Kwa sababu waandishi wengi wanapenda side shows nyingi na parallel ideas ambazo zinaondoa focus ya msomaji kwenye main idea.

  Hata kwenye mahojiano bado tunapenda kwenda nje. Kwa mfano babu yake Companero aliulizwa kuhusu kushindwa kwa ujamaa. Yeye akaanza kusema: 'Historically, when the British left......."

  Mtu amepewa dakika mbili za air wave na yeye anaanza kutoa somo la historia kwanza badala ya kusema A,B,C za kushindwa kwa ujamaa.
   
Loading...