Wakoloni weusi waliowatoa wakoloni weupe 1961 Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakoloni weusi waliowatoa wakoloni weupe 1961 Tanganyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sitakuwafisadi, Jan 23, 2011.

 1. s

  sitakuwafisadi Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO unadhani tulipata uhuru mwaka 1961 !!?? mkataba wa uhurukatiya serekali ya wakoloni uingereza na wapigania uhuru wa tanganyika uliandikwaje?? mkataba huu upo wapi na uliandikwaje?? je wakoloni waliondoka kweli??

  [​IMG]


  [​IMG]

  Mkataba wa uhuru kati ya wakoloni wa uingereza na viongozi wa tanganyika ya enzi hizo .Mashujaa wetu mtemi Mkwawa, Mirambo, Isike, Makunganya, Mangi Meri, Bwana Heri na wengineo ambao damu yao ilikuwa chachu iliyosababisha kupatikana kwa Tanzania huru...JE UNADHANI NCHI YETU ILIPATA UHURU KWELI kama nikweli tulipata uhuru kutoka kwa mwingereza HATI YA MKATABA WA UHURU IPO WAPI NA INASEMAJE JE ILIWAHI KUVUNJWA....?..UPO WAPI NA UNASEMAJE NANI ANAHATIMILIKI YA TANZANIA NA VYOTE VILIVYOMO mito maziwa bahari ... See Morembuga misitu dhahabu almasi tanzanite wanyama samaki milima ..?.


  Mashujaa wetu mtemi Mkwawa, Mirambo, Isike, Makunganya, Mangi Meri, Bwana Heri na wengineo ambao damu yao ilikuwa chachu iliyosababisha kupatikana kwa Tanzania huru...JE UNADHANI NCHI YETU ILIPATA UHURU KWELI kama nikweli tulipata uhuru kutoka kwa mwingereza HATI YA MKATABA WA UHURU IPO WAPI NA INASEMAJE JE ILIWAHI KUVUNJWA....?..UPO WAPI NA UNASEMAJE NANI ANAHATIMILIKI YA TANZANIA NA VYOTE VILIVYOMO mito maziwa bahari ... See Morembuga misitu dhahabu almasi tanzanite wanyama samaki milima ..?..
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Welcome!!!!!

  Moja ya vitu vibaya, kansa mbaya tuliyonayo ni kutokuwa wakweli hasa pale tunapoona ukweli huo utapingana na au kukinzana na pale tunapopapenda katika ukweli hili ni rahisi kwa anayempenda Kikwete kutomuona kuwa JK si kiongozi bora, ni rahisi kwa anayempenda Slaa kutomnyooshea kidole pale anapokosea! this has been our kind of habit.

  Sikuamini sikumoja nilipokutana na mjerumani fulani akasema watanzania mna tabia ya unafiki na maisha yanu siyo yale unayoyaamini au kutaka wewe! tunaficha ukweli panapotakiwa ukweli tunakuwa kimya wakati mwingine kwa sababu ya uoga!!

  We are strong in the things that we stand for, and we are weak in things that we fail!! kama output is a chief judge ya ku-evaluate peformance ya mtu, basi ni rahisi sana kupata majibu, regardless of what was the conditions or reasons of your failure!

  Machifu:

  This was great and memorable time ever happened, and it will never happen again. Uzalendo wa machifu wengi , hekima zao, legacy zao zilikuwa nzuri na zimesahaulika

  Kurithisha wajibu wa vijana kutoka kizazi kimoja kwenda kingine , kuwaza kuhusu vizazi vijavyo, kulinda mipaka, kufanya mambo kwa manufaa ya jamii hakika vitakuwa ngano katika miaka mingi ijayo, tunalilia kipindi hiki. Kumbuka kuna machifu walichemsha kwa kuuza utu wao na thamani yao kwa sababu ya ujinga!

  uzalendo wa aina yake wa baadhi ya machifu ulizaa uzalendo wakijamii wa watu kupenda jamii zao!!! kwa kulinda tamaduni zao.

  USA leo japokuwa ni li-nchi la kila mtu, still wanasema, wanahadithia na kuzungumza na kufuatilia mambo aliyoyafanya washigton miaka 200 iliyopita! they are abiding with their customs whether is written or not, american are proud of their nations!

  Leo hakuna taifa linaloitwa TANZANIA we dont have identity, we dont have nationalism, kila unayekutana naye ni fisadi!!


  Nyerere Era

  Kutoka mwwaka 1961-1966, Tanzania ili-experience what we call real freedom, kama kutawaliwa na wazungu kulikuwa sio uhuru. Ni katika kipindi hiki kulikuwa na vyama vingi vya siasa,watu walikuwa huru kutoa mawazo, kukosoana n.k

  Mwaka 1967 Nyerere alikataza vyama vingi na kutoka hapo, uhuru wa habari ulikuwa mdogo, Nyerere alikuwa hakosoleki, hashauriki. Nyerere ndiye aliyeweka misingi yote MIBOVU AMBAYO leo hii watu wanalia kuwa haifai!

  Personally Nyerere was contented, he was not greed, na alitaka kutengeneza Tanzania ya aina yake, kuanzia vijiji vya ujamaa, azimio la Arusha, nk depicted that he had good intention for this Nation.

  But he fail to admit that his tactics and plans had failed and was supposed to look for another alternative..ANY GOOD LEADER WOULD DO SO!! Inspite of personal good qualities of being leader Nyerere was never a good leader and results speak loauder than any words.

  Nyerere failed to raise up any other leader who would imitate his ideology, this is a prome example of any poor leader,
  Nyerere alikuwa much know..do I need to say more
  Nyerere was god-like man and he loved to be one--zidume fikra za mwenyekiti was unspeakable violation of human rights
  Nyerer is author and finisher of constitution we have today

  Nyerere was not asking citizens consent in many decisions that would affect all citizens.

  -Nyerere did not ask Tanzanians for all operations of pan-africanism in africa e.g wars and use of publi fund
  -Nyerere treachourously engaged in Idd Amin wars which he was sure he is the source of the problem by keeping Obote In Tanzania
  -Nyerere did not ask public opinion in Zanzibar -Tanganyika Union
  -etc.

  Today all leaders of CCM are just imitating the very same style of leadership that Nyerere adopted, is rearely to see the current government is asking public for some decision..we can discuss this deeply I am afraid time would not allow!

  The biggest mistae that Nyerere did was to think that everyone in CCM is clean like him, he fail to manifest leadership quality. He feeded Tanzanians with good and romantic words, he was the hero and only prophecy that Tanzanians ever had till today. Lisetning his speeches while we dont have people living in his ideology is a good examples that he failed to LEAD!. period!

  Kupiga kura za kivuli na kichwa cha mtu is another historical shame that those we are seeking of installing him as a saint they will have to answer this  If today we are suffering from CCM regime then the source is Nyerere. KATIBA hii na kasoro zake zote zilikuwa chini ya NYERERE HATA VYAMA VINGI VILIPOKUJA MAPUNGUFU YA KATIBA YALIJULIKANA NA NYERERE WAS THERE TO LETS THINGS MOVE ON... kama kuan waliotenda dhambi kubwa nchi hii Nyerere hakosi.. msifieni mnaomsifia

  wakati kataiba inaanzishwa mwaka 2000 Nyerere knew for sure INA MATATIZO GANI, uchaguzi wa Mkapa alikuwepo na aliona tume ya uchaguzi kuwa ilichaguliw ana CCM na haikuwa ya kitaifa..alifanya nini????

  Hakuna number ya walioenda jela kwa rushwa this time, wengi wanamsifia lakini hakuna recodi ku-cmpare na hawa wa leo...

  I know I am about to answer your question..


  CCM and Opposition Today

  CCM is only imitating and do exactly even more tha he founder..you can differentiate Kikwete and Nyerere is their personal behaviour but not in CCM ideology!!!

  Tanzania has never been free..if definition of freedom is having black president in the state house then I am afraid we need to find the definition of this very word.

  Tanzania has a country have been free from the british .....Tanzanians have never been free from CCM!!

  While the agony of freemarket is hunting us tirelessly the we are not FREE not from oppression of CCM but also oppresion from other nations especially western and now eastern, they have channled their desire in this country simply because CCM is not to protect Tanzanians wealthy but to grab them

  Though now pointing fingers to Nyerere will not solve our problems denying that he is unfit for being a father of nation that alone will help us to cancel this platonic relationship with Nyerere and whence we will stand alone to focus building NEW NATION.... which certainly not Tanzania is Tanganyika!
   
 3. s

  sitakuwafisadi Member

  #3
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jambo Lililo Wahi Kuninyima Usingizi Ni Viongozi Wakisiasa Kuamua Watanzania Zaidi Ya Milioni 44 Waishi Sawa na Utashi Wao Wakisiasa Yaani Wanacheza Siasa Ndani Ya Umasikini Wawatanzania .Taaluma tena haina thamani Tanzania DAKTARI hataki kukaa hospitali tena Mhandisi hataki tena Uhandisi Professor Hataki tena kufundisha MAISHA MAZURI YAPO KWENYE SIASA wanasiasa matajiri walimu waliowafundisha masikini wa kutupwa.!!.
  Usually
  when people are sad they don't do anything they just CRY over their
  condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)..UMASKINI TANZANIA
   
 4. M

  Mindi JF-Expert Member

  #4
  Jan 24, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Waberoya, Hapo ulipozungumzia kuhusu machifu ndio kwenye pointi yenyewe. Machifu hawakuwa perfect, walifanya makosa mengi tu. lakini walifanya mazuri sana pia. jinsi ulivyowasifia na kulinganisha na nchi nyingine kama USA ambao wanathamini michango ya viongozi wao wa zamani, ulitakiwa useme hivyo kwa Nyerere pia.

  Nakubali Nyerere amefanya makosa mengi, lakini nioneshe kiongozi mkubwa, na mahiri, ambaye hakufanya makosa. Nyerere alikuwa na kazi ya kujenga taifa, na ndiye aliyeanza ngwe. nadhani Wajerumani ndio waliounda Tanganyika, wakaweka ile mipaka. wakaandaa taifa likae mkao wa kunyonywa. akaja Mwingereza naye akaimarisha mizizi hiyo. sasa kuunda taifa huru kutokana na hicho kilichokuwepo haikuwa kazi rahisi. mwingereza alifanya kazi nzuri sana ya kujenga saikolojia ya ukoloni, ili mtu ajidharau na kujiona hafai. kulikuwa na "wasomi" ambao waliabudu utamaduni wa magharibi, kama ilivyo leo hii. nao walikuwa wachache sana. tukubaliane kwamba Nyerere alianza kazi ya kujenga taifa huru katika mazingira ya namna hii. watanganyika wengi walipenda kuibia wenzao, kuishi katika "expense" ya wengine. idol ilikuwa kuwa kama mkoloni alivyoishi.

  Lakini Nyerere alifanya jitihada kubwa sana kubomoa misingi aliyoikuta. ndio maana ya kuzama sana kwenye ideology, kubomoa misingi ya ukoloni wa kifikra, utumwa wa kifikra. viwanda alivyojenga, systems alizojenga, networks za kuleta uhuru katika bara la Afrika, watanzania walikuwa proud kuwa watanzania. pamoja na weakness zake zote, unazungumziaje waliomfuatia, je walifanya jitihada kujenga utaifa katika mazingira mapya ya wind of change iliyokuwa inapita katika dunia? actually wamebomoa misingi ya taifa, mali za taifa, tunu za taifa. kuuza mashirika, viwanda mpaka nyumba za serikali.

  hatuna shukrani wala busara kumlaumu Nyerere, bali kujilaumu wenyewe kwa kukubali kuendelea kuwa na viongozi wezi, ambao wanakiri kabisa kwamba wataendelea kutuibia na kubomoa taifa letu, na sisi tumekubali kula matapishi hayo. hatustahili kuitwa watanzania
   
 5. M

  Mindi JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Hata kama hati hiyo imechanwa, kama vile mtu anaweza kuwa hana birth certificate lakini huwezi kusema kwamba sio binadamu mwenye haki zote za binadamu, kadhalika haki zetu kama nchi ziko pale pale, na wajibu wa watanzania kutetea tunu za utaifa wao ziko palepale.

  Wakati tunashabikia mtu kukwepua fedha serikalini au katika shirika na kutajirika haraka, tunasahau kwamba tunaua taifa letu. wakati tunashabikia makosa ya akina Nyerere ambao walifanya mazuri yao na mabaya yao, sisi wenyewe hatuangalii makosa yetu. angalau Nyerere alichagua kupigania uhuru wa nchi, sasa sisi tunafanya nini kupambana na hawa wanaoharibu nchi yetu? hili ni swali ambalo kila mtu ajiulize na kujijibu. wapo wanaofanya jitihada, mfano wale ambao wanatoa "siri" za serikali na kuwatonya akina Slaa na wengine ili wazimwage, hatuwajui lakini wanatoa huduma nzuri sana kwa taifa.

  Wapo wengine wanaojitokeza hadharani na kukemea maovu serikalini na katika jamii. hawa wanaweza kuwa viongozi wa dini au watu wenye nafasi za uongozi au watu maarufu. wanafanya hivi huku wakihatarisha usalama wao na familia zao, na hata riziki zao. wapo waandishi wa habari ambao wamejitoa mhanga kuhakikisha kwamba machafu yanayofanywa na viongozi yanawekwa hadharani ili uma ujue na kuamua inavyotakiwa wakati ukifika. kama Tunisia wameweza kuing'oa serikali ya kifisadi, Tanzania inawezekana pia, pamoja na tofauti zetu na Tunisia.

  Ni juu yetu sisi wote kila mtu kuamua atafanya nini kuchangia katika mapambano haya, overtly or covertly. tuheshimiane tusianze kushambuliana sisi kwa sisi. maadui wa taifa wanafurahi sana wanapoona wapambanaji wanashambuliana wao kwa wao badala ya kuwashambulia maadui wa kweli wa taifa.

  Tuanze na wale waliojipambanua kuwa watasimamia uporaji wa taifa hili. chama cha CCM kimesema wazi katika tamko lake la kamati kuu kwamba kitasimamia uporaji wa mali za nchi hii. tuanze na hawa.
   
 6. s

  sitakuwafisadi Member

  #6
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HPIM0259.JPG soksi.JPG chupi.JPG UMASIKINI NCHINI KWETU SIO HAKI YETU NIWAKUPANDIKIZWA tuukatae huo mti ndio ule uliokua ukitumiwa na wakoloni kama chombo cha kunyongea watanganyika kwasasa tanzania bara upo jijini mwanza jirani kabisa na geti la kuingilia benk kuu tawi la mwanza. hapo katikati hizo nisoksi zamtumba huko mwisho hizo nichupi za mtumba SWALILANGU NIKWELI WATANZANIA HAWAMUDU KUNUNUA HATA CHUPI MPYA WALETEWE MTUMBA AU SOKS ZA MTUMBA.??.................UMASKINI TANZANIA
   
 7. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MAUDHUI ya leo ni mwendelezo wa makala niliyoiandika wiki mbili zilizopita ikiwa na kichwa cha habari kisemacho: Karne ya 21 bado tumebaki kuwa korokoroni wa wakoloni. Nimekwishaandika sana udadisi wangu kuhusu matatizo ya nchi zetu za Afrika na wakati mwingine inafikia pahala ninafikiria kwamba huenda ninawachosha wasomaji wa makala zangu.

  Lakini hata nikinyamaza, bado mawe yatasema. Kwa sababu ninachokiandika hakitokani tu na udhaifu wa kibinadamu, au utashi wa kutaka kusema tu, bali msukumo wa wito wa kudadisi na kujadili ninayoyaona yana maslahi kwa wananchi wenzangu na mustakabali wetu kama raia wa Afrika.

  Hivi ninavyoandika tayari zimekwishaanza harakati za Watanzania wenzetu kuusaka uongozi wa nchi yetu mwaka 2015. Na dalili zenyewe zinaonyesha kabla hatujafika huko (2015).

  Wakati TANU inajipambanua kama chama cha kudai uhuru, walikuwapo watu wa aina nyingi. Walikuwapo Watanzania kama akina Mwalimu Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes, Rashid Kawawa, Oscar Kambona, Anuur Kasum, Bryson na wengine ambao walijitoa muhanga kupinga udhalimu wa wakoloni wakiamini kwamba sisi wenyewe tungeweza kujitawala kwa akili zetu na mikono yetu na kwa kutumia rasilmali zetu.

  Lakini katika harakati zao, walikuwapo pia waswahili wenzetu ambao kazi yao kubwa ilikuwa kuwakatisha tamaa na kuwaambia kwamba; “ah, akina Kinjekitile, Mkwawa, Mirambo na wengineo waliwashindwa wakoloni, hivi nyie mtaweza kuwaondoa?” Walikuwapo pia Watanganyika wenzetu, ambao kazi iliyokuwa ikiwapa kula, ilikuwa ni kuchunguza na kuripoti kwa wakoloni kila walichokuwa wakikipanga akina Mwalimu Nyerere.

  Wadaku wale, kutokana na tabia ya kujipendekeza kwa wakoloni, ama kutokana na ujuha wa kutokujitambua, au njaa tu ya kuhitaji kushiba leo, walikwenda mbali zaidi na kutunga mambo ya uongo kuhusu wakombozi wetu ili wao wapate uhalali na kibali mbele ya watawala na hatimaye waendelee kupata ugali wao hata kama waliishi kitumwa. Wao walibatizwa sifa ya ‘uzalendo’ na wakoloni lakini akina Mwalimu Nyerere wakaitwa wasaliti.
  Dunia tunayoishi leo haiko salama, kwetu. Tunadanganyika kwamba tunayo demokrasia lakini ukweli ni kwamba, tunaishi dunia ya kiinimacho. Kuna usanii mkubwa unaendelea ambao tungeujua undani wake tungefikiria mara mbili. Hivi leo tunaweza kudanganyika sana na harakati za majina ya watu kutaka kurithi uongozi wa nchi yetu baada ya muhula wa mwisho wa Rais aliye madarakani. Tunaweza kubweteka kabisa na harakati hizi tukidhani tatizo letu kubwa la kiukombozi litatatuliwa na majina. Katika mkutano wake na wanahabari mwaka 1995, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema: “Kama suala lingekuwa ni majina tu, tungeweka majina kadhaa katika kapu moja hivi na halafu tukamuomba hata ‘mtu asiyeona’ akachukua jina na hilo likawa ndo jina la kiongozi wetu.”

  Tukumbuke kuwa pamoja na upungufu wa kibinadamu na kimkakati aliokuwa nao Mwalimu Nyerere katika utawala wake, dhamira aliyokuwa nayo katika kujenga jamii ya watu huru, wanaostahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wao na uzoefu alioupata hasa kwa kipindi chake kigumu. Ni viongozi wachache sana nchini wanaoweza kumkaribia kiuongozi. Ni viongozi wachache sana nchini na hata Afrika walioweza na wanaoweza kuwatazama usoni wakoloni wastaafu na kuwaambia “sera zako sikubaliani nazo kwa sababu zitadhuru watu wangu”, halafu wakoloni wastaafu wale wakaelewa na wakaendelea kushirikiana nao na kuwaheshimu.

  Uongozi wa nchi yetu leo unatafutwa kwa mizengwe, vitimbi na fitna za kuchafuana na kupakana matope. Watu wanachafua wengine ili wao wabaki nafuu halafu wakubalike kwa wananchi. Katika mchezo wa siasa chafu za aina hii, watu wema kabisa ambao wangekuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu wanajikuta wamepigwa na bumbuazi, wameshika tama kwa sababu hawana ujuzi, umaridadi wala hulka ya kushiriki katika ujinga na uchafu wa kudhalilisha na kuchafua Watanzania wenzao. Wanakubali yaishe na wanakaa kando.

  Kudhani kwamba Watanzania, au Waafrika, hawawezi kujengewa mazingira wakawekeza wenyewe kwa manufaa yao, miaka 50 baada ya uhuru wao wa kisiasa, ni kukaribisha nadharia kwamba kumbe hata kujitawala wenyewe hawawezi. Narudia kusema, endapo Watanzania, au Waafrika, hawawezi kuwekeza katika madini, wakayanchimba na kunufaika nayo zaidi, hadi machimbo yauzwe kwa wawekezaji wa kutoka nje kwa wakoloni wetu wastaafu; endapo Watanzania hawa hawawezi kutumia ardhi waliyorithishwa na Mwenyezi Mungu katika kunufaika na kilimo cha chakula na biashara, miaka 50 baada ya uhuru, hadi waitwe wawekezaji hata wanaokuja kuwinda tu; endapo watanzania hawa walishindwa hata kuendesha viwanda vya nguo za kuvaa vilivyokuwa vikitumia pamba waliyokuwa wakilima wenyewe, hadi wakauziwa wawekezaji wakageuza vikawa magodown ya kuuzia mitumba toka nje; endapo Watanzania hawa hawawezi kuendesha nchi kwa bajeti inayotokana na jasho lao na rasilmali zao nyingi – hadi ijaziwe na misaada ambayo pia watawala wanaichezea; endapo Watanzania hawana uwezo wa kuweka vipaumbele katika elimu na badala yake rasilmali nyingi zinaingizwa katika anasa za kuendesha maisha ya watawala – huku wafadhili wakiangalia tu; basi kuna hitimisho moja muhimu: Hatuwezi kujitawala.

  Inawezekanaje kwamba wanaoshindwa kuchimba dhahabu katika ardhi yao kwa ufanisi ni Watanzania hao hao, hadi inabidi waitwe wawekezaji toka nje waje kuwakalia kichwani? Wanaoshindwa kutumia ardhi yao vyema kwa kilimo cha chakula na biashara ni Watanzania hao hao – hadi wanaitwa wawekezaji wa kuja kuwahamisha katika ardhi ya babu zao, wengine kwa ajili ya kuwinda tu; kwamba wanaoshindwa kujitegemea katika kodi ya kuendesha nchi ni Watanzania hao hao – hadi asilimia karibu 30 ya bajeti inategemea wafadhili – na bado haileti tofauti; kwamba wanaoshindwa kutoa fikra, mawazo na sera bora za kutatua matatizo ya ndani ya kiuchumi ya nchi ni Watanzania hao hao – hadi siku zote wanakuja wageni kuwaambia ni nini cha kufanya; kwa kifupi, wanaoiangusha Tanzania (au Afrika) ina maana ni wananchi wake wale wale walioshindwa kwa karibu kila jambo kiasi cha kuwaalika wageni kuja na suluhisho.

  Twende katika mantiki. Watanzania (au Waafrika) hawana uwezo wa kuchimba na kutumia madini yao hadi waje wawekezaji kutoka nje; Watanzania (au Waafrika) hawana uwezo wa kutumia ardhi yao kwa ufanisi na kwa faida hadi waje wawekezaji kutoka nje; Watanzania ( au Waafrika) hawana uwezo wa kupanga vipaumbele vyao kuhusu elimu, afya, uchumi, n.k., hadi waje wataalamu kutoka nje kuwashauri; Watanzania (au Waafrika) hawana uwezo wa kuendesha bajeti yao kwa kujitegemea, hadi ijaziwe na fedha za wafadhili kutoka nje ambazo pia hawazitumii kwa ufanisi.

  Na kama tunathamini mantiki: Na kama kweli imebainika kwamba Watanzania (au Waafrika) hawa hawawezi kabisa kutekeleza, kwa ufanisi, hayo yote yaliyotajwa hadi watafutwe wawekezaji kutoka nje (ambao zamani waliitwa wakoloni, mabeberu au makaburu) je, kuna mantiki gani kuamini kwamba Watanzania (au Waafrika) hawa hawa wanaopewa dhamana ya kuongoza nchi eti wanaweza kuongoza kwa ufanisi? Kwani wao wanakuwa na damu ya wawekezaji kutoka nje kule wanakotoka wanaoweza? Je, endapo mashirika ya umma yaliuwawa kutokana na kukosekana ueledi, utamaduni na hulka ya ufanisi; na hivyo ikabidi watafutwe wawekezaji (wakoloni wastafu) kuja kutuokoa kuayendesha kwa ufanisi, ni kitu gani kinatufanya tuamini kwamba Watanzania (au Waafrika) wale wale wanaotokana na sisi na jamii yetu na damu yetu ile ile eti wanao uwezo wa kuendesha nchi yetu (zetu) kwa ufanisi?

  Je, endapo tukiamua kufuata mantiki hii – kwamba, kwa kuwa tumekuwa tukiwaita wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza pale tuliposhindwa kuwekeza kwa ufanisi; katika madini, ardhi, umeme, uchumi, mawazo, n.k. Eti sasa watafutwe wawekezaji kutoka nje ili waje kuwekeza katika uongozi wa kuendesha nchi kwa kipindi fulani (Tax free) kama tufanyavyo kwa uwekezaji mwingine ili kuongeza ufanisi, kutakuwa na tatizo gani?

  Je, endapo wananchi wote nchi nzima, wanaweza kukosa akili ya kuendesha maisha yao kwa kutumia kwa ufanisi rasilmali zao walizokabidhiwa na Mwenyezi Mungu, hao viongozi wenye vipaji vya nadra vya kuongoza nchi kwa ufanisi wanakuwa wameponaje na ugonjwa huu wa ukosefu wa ufanisi? Na je, endapo viongozi hawa, wanaotokana na wananchi wale wale wasioweza kutenda kwa ufanisi, kweli wanao uwezo wa kuongoza kwa ufanisi, tunapimaje ufanisi huo kama hautusaidii sisi tunaoongozwa lakini tunaona unawasaidia wao binafsi na wawekezaji wao? Na je, kwa kuwa viongozi tayari wameonyesha imani kubwa kwa wawekezaji wa nje, na dharau kwa wananchi wake wa ndani, ni kwa nini basi wasikubali tu kwamba madhali na wao ni sehemu ya jamii ile ile inayoshindwa kuwekeza kwa ufanisi, basi na wao pia wakae pembeni ili nchi iongozwe na wawekezaji wa kutoka nje wanaojua kuendesha mambo kwa ufanisi? Hii ni mantiki tu ya mbayuwayu!
  RED ALERT:
  Maoni yangu nadhani hata serekali imeshabinafsishwa tayari kwasababu kila kitu kinaendeshwa kwa muongozo kutoka kwa washauri wataalam
  Consultancy toka marekani/Uingereza nk.,.

  Source:GAZETI MWANANCHI-Saturday, 18 June 2011 18:15
   
 8. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakoloni weusi, kina JK, Mwema, Nahodha, Makinda, Pinda
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Vurugu za Mbeya, Arusha na sasa Tabora siyo tu zinawanyima usingizi bali zime-confirm kuwa mwisho wa udhalimu umefika na sasa watanzania wameamka. Kibaya na chakutisha, benki za nje zimeendelea kupokea fedha nyingi zenye majina ya vigogo pasi kufich,a na muda si mrefu wata-anza kuachia madaraka kwa kujiuzulu, kuachishwa na na wako ambao wako tayari kufia humu ndani. Kwa wale ambao wanaonekana wasafi ndani ya CCM bado wako kwenye wasiwasi wa kuaminiwa na jamii. Hivyo muda si mrefu tutawasikia wakihama vyama ama kuungana na mafisadi


  Nasema hivi....Nasema kuwa CCM wanaondoka na fedha za taifa hili...AMKA!!!i...hawa CCM .si wahindi ..si wachina..si waarabu ni weusi wenzetu . Ni wale wasaliti wa utaifa na taifa hili.....ni wasaliti wa mababu zetu na utu wetu ndio wanaiba na kuondoka na fedha ...Seriously!
  Na wataiacha maskini

  CCM ni aibu yetu....tumeiweka aidha ulipiga kura au haukupiga kura...CCM inatakiwa iondoke aidha kwa kupiga kura au bila ya kura!

  Mabomu hayasaidii..
  risasi zinaleta hamasa..
  Virungu vinasisimua mwili..
  kifo ni ushujaa
  !


  Tarumbeta kuu na ipigwe na kutoa sauti.....

  waambie kaskazini CCM inatosha!
  waambie kusini Tanzania bila CCM inawezekana!
  waambie magharibi CCM sasa basi
  Mashariki na iseme kwa heri CCM!!


  Vilima na milima iseme Karibu Tanzania mpya karibu leo... leo.. leo!

  watoto wetu na waimbe...karibu Tanzania mpya leo..leo ..leo!

  akina mama pigeni vegelegele vijana pigeni mbinja Tanzania mpya inakuja leo...leo..leo!

  Akina baba amkeni..barabara zilizojaa madimbwi zinatusubiri..polisi nao wataungana nasi kuipokea Tanzania mpya..leo..leo..leo!

  wapinzani unganeni..raha ya nchi mpya..mtoto mpya ni furaha ya wote....tayarisha nepi na manukato TANZANIA mpya inakuja leo..leo..
  leo!


  Akina mama vilio vya kuzalia sakafuni vitaisha.......wazee mliokuwa mkisubiria haya mtalia kwa furaha mkisema

  Freedom at last .......Freedoma at last..Thank God we have freedom at last!!


  CCM Tuachieni Tanzania yetu!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Soon and very soon Mbuyu unangooka...Moto huu hautazimika KAMWE....Mkoloni mweusi FUNGASHA VIRAGO, UTUACHIE NCHI YETU!
   
 11. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu, yaani nimehamasika vya kutosha..)) Freedom freedom freedom.....))
   
 12. escober

  escober JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  well said wabe we are waiting for that day (siku ya ukombozi)
   
 13. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I like it. Yaani huu wimbo nimeupenda sana, Hongera mtunzi, Tunaanzisha safari ya kumng'oa mkoloni mweusi.
   
 14. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Freedom today and not tommorow!wa watanzania tuamkeni!!tudai haki zetu,hawa wehu wasigeuze nchi kuwa mali yao waliorithi kwa babu zao!Nchi ni yetu watanzania!TUAMKENI USINGIZINI.
   
 15. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha Wabe, kuna mda nmesoma hyo post yako nkajiona kama nasoma Zaburi.... Hamasisho zuri, na uzuri zaidi ni kuwa "MIMI" ni sehemu ya uhuru huo na Tanzania mpya (mtoto mchanga)
  Aluta.....
   
 16. A

  AzimiolaArusha Senior Member

  #16
  Nov 14, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45  Hii kali, watawala someni alama za nyakati!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mmmmmh Engeneer B @ work

  Freedom is coming today
   
 18. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #18
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wabe ubarikiwe! Kweli wewe mtunzi kaka, soon and very soon we wil get our freedom back!
   
 19. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #19
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  well said mkuu...but how?

  maana hawa tulio nao hawa (the sugu's & lema's of this world) ambao mimi naona walau wanajitahidi kutuonyesha kitu fulani kivitendo tunaishia kuwaponda na kuwa-brand eti ni "opportunists", vilaza, name it!

  tunaweza tusikubaliane na methods zao lakini kama wanachokifanya kina uwezo wa ku-ignite some kind of uprising against the corrupted establishment (you have correctly cited recent Mby & Arusha incidents - i think unajua kibri yao wameitoa wapi hawa watu!), why not give the credit where it is deserved?
   
 20. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #20
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Freedom Is Here Already ni sisi tu kuikaribisha, it has been long time comin.

  Kama una account Facebook weka status watu wahamasike
  Twit watu wajue..
  BBM it tuupokee uhuru..
  Social Network yeyote sambaza ujumbe, tulichokingoja longtime kimewadia sasa tukipokee...

  Na siku zote mgeni huanza kulakiwa barabarani, Twendeni barabarani tukamlaki uhuru.
  Najua majirani wenye wivu na wachawi (Polisi) watajaribu kutukwamisha kwa kutupiga mabomu, risasi na virungu, tusiviogope haviumizi kama njaa na ugumu wa maisha tulonao. Maumivu ya virungu ni muda mchache lakini maumivu ya njaa ni miaka, ukosefu wa elimu ni kizazi.
  Risasi zinaua lakini hata hizo dawa feki wanazotulisha zinaua vile vile. Chagua moja kufa ukitafuta haki yako na mwanao au kufa kitandani pamoja na nduguzo?


  Hata mama akiwa labour husahau uchungu the instant anamuona mwanae kazaliwa safe, na sisi vidonda na makovu ya risasi yatapoa pale Uhuru tutakapouchukua.


  Tuamke Sasa Hivi Jioni Tuwe Huru.
   
Loading...