Wakoloni walifanya haya yanayofanyika leo lakini Waliondoka

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Upinzani hauwezi kufa kwa kuwafunga na kuwakamata viongozi wa upande wa upinzani hata siku moja... Badala yake ndivyo unavyostawi na kukomaa kwasababu dhamira yao ni njema kwa nchi yao. Hiyo kazi aliifanya mkoloni Mjerumani na Muingereza kwa watangayika lakini mwishowe waliondoka wakati ulipowadia!

Kutumia mbinu hizi za kikoloni kwa wenyewe kwa wenyewe inabaki kuwa historia ya upumbavu wa Mwafrika, na kuendelea kudharaulika na walimwengu wengine waliostaarabika!!

Trump aliposema African needs to be recolonised alikuwa sahihi katika mazingira haya. Rule of Law ni msamiati adimu kwa watawala wa kiafrika na ndipo chanzo cha umasikini wa akili, mali na kipato ulipolalia!
 
Nilijua unawapongeza wakoloni walifanikiwa kututengenezea nchi vyema lakini sisi tumeshindwa hata kuendeleza jambo lolote...
Yamebaki maneno na marumbano ya kipuuzi
 
Yaani nilifikiri atapongeza chuo cha ufundi nguo cha Songea kilichoachwa na wakoloni.
Nilifikiri utapongeza reli ya mtwara mpaka msumbiji tuliyoipotezea sababu ya kuogopa makaburu.
Nilifikiria utazungumzia uwanja wa ndege wa mafia uliosaulika japo ndio njia pekee na salama ya kufika kule,
Nilifikiria utaitaja kilwa iliyokuwa juu kwenye miundombinu lakini sasa ni giza.
nilifikiri ungetaja reli ya tanga moshi tukumbuke miaka ile tuliyokuwa tunaenda moshi kupita korogwe.
 
Ccm eleweni kuwa mtafunga,mtatesa na mtaua wapinzani ila hamtaua mawazo ya wapinzani
 
Hizi sasa ni kauli za kukata tamaa!!!like tunasibiri hatma iamue,tunangoja rehema za Mungu.
 
Back
Top Bottom