TAWA
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 3,667
- 1,566
Wilson Mkama aliyewahi kuhudumu kama Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi ccm kwa kipindi fulani huku akikumbukwa sana katika uchaguzi wa marudio kule Igunga Tabora baada ya kuachia ngazi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu Rostam Azizi. Atakumbukwa zaidi kipindi cha tambo za watu wa Lumumba almaarufu "helkopta tatu kata tatu"
Mustapha mkulo aliyewahi kuwa mbunge wa Kilosa ccm na waziri wa fedha uchumi na mipango wa taifa hili. Mwanasisa nguli na mwenye ushawishi Mkubwa ndani na nje ya ccm. Katika kipindi chake atakumbukwa zaidi kwa misamaa mikubwa ya kodi katika makampuni makubwa na hasa migodi.
Shamsi Vuai Nahodha, aliyewahi kuwa waziri Kiongozi katika serikali ya mapinduzi Zanzibar, mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuhudumu kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi nafasi ambayo aliitendea haki kwa kiasi fulani.
Wamepotea kabisa watu hawa Katika tasinia ya siasa za hapa kwetu. Wamekuwa hawasikiki kabisa. Popote walipo naomba kukumbushwa. Au ndiyo zilipendwa!?