Wako wapi Wilson Mukama, Shamsi Vuai Nahodha na Mustapha Mkulo!?

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,664
1,565
Wilson Mkama aliyewahi kuhudumu kama Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi ccm kwa kipindi fulani huku akikumbukwa sana katika uchaguzi wa marudio kule Igunga Tabora baada ya kuachia ngazi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu Rostam Azizi. Atakumbukwa zaidi kipindi cha tambo za watu wa Lumumba almaarufu "helkopta tatu kata tatu"

Mustapha mkulo aliyewahi kuwa mbunge wa Kilosa ccm na waziri wa fedha uchumi na mipango wa taifa hili. Mwanasisa nguli na mwenye ushawishi Mkubwa ndani na nje ya ccm. Katika kipindi chake atakumbukwa zaidi kwa misamaa mikubwa ya kodi katika makampuni makubwa na hasa migodi.

Shamsi Vuai Nahodha, aliyewahi kuwa waziri Kiongozi katika serikali ya mapinduzi Zanzibar, mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuhudumu kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi nafasi ambayo aliitendea haki kwa kiasi fulani.

Wamepotea kabisa watu hawa Katika tasinia ya siasa za hapa kwetu. Wamekuwa hawasikiki kabisa. Popote walipo naomba kukumbushwa. Au ndiyo zilipendwa!?
 
Zama zimebadilika, sio kila homa ni Malaria. yajayo yanafurahisha zaidi. Upo tayari?.
 
Shamsi nafikiri bado ni mbunge wa jmt, Mukama miezi kadhaa nyuma nilimuona akihojiwa channel 10 nafikiri na Makwaia Wa Kuhenga.

Mkulo ndio sijamsikia kabisa. mwanasiasa mwingine aliyepotea kabisa ni Dr. Ibrahim Msabaha, sijui yuko wapi?
 
mkama yupo anapatikana sana mitaa ya Rengent estate mikocheni ana v8 yake ileile alokuwa anatumia alipokuwa Katibu Mkuu ila haipepei bendera tu
 
Wako kwenye makumbusho ya siasa
Naam. Waliko pia Ngereja, Rost tamu l'azizi, Matilida Burian, Paulo Kimiti, Geturuda Mongella, Leticia Nyerere, Fatma Saidi Ally, Dr. Ulimboka, Ask. Kilaulaini, Zamoyoni Mogella, Mohamed Mwameja, Padri Mwaisapile, Fande Tibaigana, na wengine weeeeengi tu. Ni kifo tu KITAWATOA kwenye haya Makumbusho.
 
Leticia Nyerere alishafariki siku nyingi
 
Wilson Mkama aliyewahi kuhudumu kama Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi ccm kwa kipindi fulani huku akikumbukwa sana katika uchaguzi wa marudio kule Igunga Tabora baada ya kuachia ngazi aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu Rostam Azizi. Atakumbukwa zaidi kipindi cha tambo za watu wa Lumumba almaarufu "helkopta tatu kata tatu"

Mustapha mkulo aliyewahi kuwa mbunge wa Kilosa ccm na waziri wa fedha uchumi na mipango wa taifa hili. Mwanasisa nguli na mwenye ushawishi Mkubwa ndani na nje ya ccm. Katika kipindi chake atakumbukwa zaidi kwa misamaa mikubwa ya kodi katika makampuni makubwa na hasa migodi.

Shamsi Vuai Nahodha, aliyewahi kuwa waziri Kiongozi katika serikali ya mapinduzi Zanzibar, mbunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuhudumu kama waziri wa mambo ya ndani ya nchi nafasi ambayo aliitendea haki kwa kiasi fulani.

Wamepotea kabisa watu hawa Katika tasinia ya siasa za hapa kwetu. Wamekuwa hawasikiki kabisa. Popote walipo naomba kukumbushwa. Au ndiyo zilipendwa!?
Si ungekwenda itv wakutafutie?
 
Shamsi nafikiri bado ni mbunge wa jmt, Mukama miezi kadhaa nyuma nilimuona akihojiwa channel 10 nafikiri na Makwaia Wa Kuhenga.

Mkulo ndio sijamsikia kabisa. mwanasiasa mwingine aliyepotea kabisa ni Dr. Ibrahim Msabaha, sijui yuko wapi?
Wastaafu wengine hutumia busara na kuamua kukaa kimya.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom