Wako wapi viongozi wa dini? Je hawaoni na hili au hakuna la kusema?

Kati ya watu ambao wanaliangusha na kupitia aibu taifa letu ni viongozi wetu hawa wa kiimani, hivi Mungu ndio anavyotaka tufanye kazi zake kwa utaratibu huu? Mungu ndiye aliyetutaka tukae kimya tuache kukemea vitendo viovu vya kunyemeleana na kupigana riasi?

Katika watu ambao Mungu anawachukia sana ni wale wanaokaa kimya kwa makusudi huku wakielewa kua kuna matatizo makubwa yansikumba jamii hasa haya ya kupotea na kutekwa kwa watu,watu kupigwa risasi. Hawa viongozi wetu wa kiimani wanatuangusha sana sana.


Halafu cha kushangaza zaidi ni kwamba hawa viongozi wengi wao ni wajumbe na mabalozi wa kamati mbali mbali za ulinzi na usalama nchini. Matukio haya itakua yanapangwa hayatokei kwa bahati mbaya na wahusika wanaendelea hata kutoa vitisho.

Viongozi wa dini temeni mate chini mwogopeni Mungu wetu aliye juu ambaye kila siku mnahubiri tumwabudu,msikae kimya hatuwezi kueaelewa kamwe. Mtachomwa moto vibaya ninyi.
 
Nchi hii iko na wajasiliamali wa dini, dini imekuwa chaka la waharifu na wezi na hakuna hata mmoja anayetambua wajibu wake kwa jamii zaidi ya kujipendekeza kwa viongozi wa serikali
 
Mbona Ponda jana kasema, labda wengine wanajiandaa kuja na matamko rasmi ya taasisi zao..
 
Wapo wapi mashekh, wapo wapi maaskofu, wapo wapi wachungaji.... Kwenye tukio kubwa kama hili tulitegemea tamko kutoka kwenu... Ok wacha tuwaache na uongozi wa dini zenu.... Sisi tumuombe muumba amponye mh tundu LISSU

Sent using Jamii Forums mobile app
mara nyingi walio kimbelembele katika kuzisema mamlaka ni ndugu zangu viongozi wa Kikristo.
kwa JK na Mwinyi walikuwa wanasema hovyo sana lakini kwa Mkapa na awamu hii wameufyata.
je, huu siyo "udini" (mfumo Kristo) ambao ndugu zetu Waislamu wanaulalamikia miaka yote?

mimi ni Mkristo niliyempokea Yesu tayari.
 
Jamani acheni kulaumu...

Siku za kuabudu ziko tofauti na zinaanza Ijumaa,Jumamosi na Jumapili,tuwape muda siku hizi zikipita kama hakijasemwa chochote ndio ilipaswa tuje kuandika lawama hapa.

Acheni kuishi kwa hisia.
 
Jamani si watasemea kwenye nyumba za ibada subiri siku za ibada mtawasikia,msiwahukumu msije hukumiwa
 
Pengo nasikia anaumwaga,

shehe mkuu yeye sijui hata anaitwa nani,

gwajima nasikia yuko marekani.

Mzee upako labda tusubiri hangover iishe atatoa kitu maana namkubali sana mzee upako.

Kilaini,bado yuko busy kusaka hela ya kurudisha kwenye mfuko wa escrow.

Marekana,aah sisi wasabato huwaga hatufuatilii mambo ya dunia hii,sisi tuko kiroho zaidi.

Etc etc
 
Wapo wapi mashekh, wapo wapi maaskofu, wapo wapi wachungaji. Kwenye tukio kubwa kama hili tulitegemea tamko kutoka kwenu. Ok wacha tuwaache na uongozi wa dini zenu. Sisi tumuombe muumba amponye mh Tundu LISSU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimejiuliza swali tangu Jana jioni nimebaki mdomo wazi. Ila imenisaidia kuwafahamu viongozi wetu Wa dini ikiwemo ya kwangu kuwa ni WACHUMIA TUMBO na Mungu atawahukumu kwa unafiki wenu.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Viongozi gani ?
Hao ambao huwa anawatukana kila siku ?
Acha unafiki wewe ni lini Lissu aliwatukana viongozi wa dini,kama kiongozi wa dini ni kweli sio mnafiki anaongoza dini hawazi gombana na wanasiasa lkn kama ni kiongozi mnafiki anaetetea udhalimu lazima wanasiasa wampe za USO.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom