wako wapi akina Mwanri,kingunge, Makalla and the likes?

Mkira

JF-Expert Member
May 10, 2006
425
119
Hawa jamaa ukisoma maneno waliyoyasema mwezi wa SEPTEMBER KUHUSU WAPINZANZI UTASHANGAA SANA!

MARA BAADA YA DR SLAA KUJA NA ORODHA YA MAFISADI, HAWA JAMAA WALIKANA KATA KATA NA KUSEMA WAPINZANI WANASEMA UONGO NA KWAMBA CHAMA CHA CCM KINA MTANDAO MKUBWA NA FEDHA ZA KUTOSHA ETI KAMWE HAKUNA WIZI WA FEDHA HUKO BOT!

TENA BAYA ZAIDI MWANRI ALISEMA CCM WATAZANGUNKA NCHI NZIMA KUWAAMBIA WATANZANIA WAACHANE NA MANENO YA UPUUZI WA WAPINZANI? HIVI KAMA HAWA JAMAA NA CCM WANGEFANIKIWA KUSIMA JUHUDI ZA KUWAFICHUA MAFISADI NCHI YETU BAADA YA MIAKA MITANO AU KUMI IAJAYO INGEKUWA KATIKA HALI GANI.

HIVI KWELI MTU KAMA MWANRI, MAKALA, MAKAMBA NA MZEE WAO CHINGUNGE LEO HII WATAAMBIA NINI WATANZANIA??

KWELI NIMEANIMINO MSEMO USEMAO " WITHOUT RESEARCH DON'T SPEAK!"


NI VEMA WAPUMZIKE INAWEZEKAMA HAWAKUTEGEMEA KAMA WIZI HUO UNAWEZA KUFANYIKA BOT? AU KAMA WALIKUWA WANAJUA BASI WAO NI SAWA NA WAUAJI WA WATANZANIA.


BAADA YA WATU WACHACHE KUPONDA HELA ZA RICHMOD, WALIPAJI NI SISI GHARAMA ZOTE KWA KUTUMIA BUNGE LAO ZINAHAMISHIWA KWA MWANANCHI!

PIA KUHUSU WIZI WA BOT, HAZINA WAO MZIGO MKUWA WA KURUDISHA HELA NI WAO KUAMUA KWA KUPITIA WABUNGE WAO(HIVI WABUNGE WA CCM WANAISHI NCHI NYINGINE NA SI TANZANIA?).

MFANO SUALA MALIPO YA LESENI ZA MAGARI MFANO TOKA 20000 HADI 150000/= HIYO YOTE ILIKUWA NI MIKAKATI YAO NA AKINA LOWASSA WAO KUWAUMIZA WANANCHI ILI KUFIDIA HELA WALIZOIBA. TUMEUMIZWA SANA KWA KUPANDISHIWA KODI ZA KILA AINA!

WAKATI UMEFIKA TUAMKE NA TUKATAE GHARAMA ZA KULIPIA MAGARI, MADAWA HOSPITALINI TUZIKATAE AU ZIPUNGUZWE!

JANA KUNA MGNJWA MMOJA HUKO TEMEKE HOSPTILA ALISHWA KUPATIWA HUDUMA KWA SABABU NDUGU ZAKE HAWANA HELA YA KULIPIA KIPIMO SH 20000/= TU!!!!!!!

HAKIPO KATIKA HOSPITALI YA SERIKALI(TEMEKE) LAKINI MTU TENA WA KAWAIDA TU ANA CHO KATYIKA KAKIBANDA KAKE!! ANACHAJI KATI YA ELFU 20 NA 30.

HUO TU NI MFANO WA ADHA ZINAZO WAPATA MASIKINI, UKWELI NI KWAMBA HATUNA HOSPITALI BALI MAJENGO TU, NA HAPO BADO HUJAMHONGA DAKITARI!


HELA ZA SERIKALI KWA AJILI YA HUDUMA ZA AFYA, MAJI WANAKULA WATU WACHACHE!

NI NANI ANAYEWEZA KUJA HAPA KUTUMBIA KUWA HUDUMA ZA AFYA SERIKALINI NI BUREE!!!!!

HOSPTILAI NYINGI HAZINA ZANA ZA KUTENDEA KAZI LAKINI CHA AJABU WATU BINAFSI WANAVYO JE HIYO INAINGIA AKILINI???!!!.

HELA WALIZOIBA ZIRUDISHWE NA TUKATE SULA LA MTU KWENDA HOSPITALI NA KUCHANGISHWA TUILEZE SRIKALI KUWA HAINA MAHOSPITALI BALI MAJENGO! ILI WAJUE KUWA HELA ZA WATANZANIA ZINATAKIWA KUWAHUDUMIA WOTE NA SI MANYANG'AU WACHACHE!
 
Njia za mwongo ni fupi sana hivyo hawa wameachwa uchi sasa unafikiri wanatamani hata kuyakumbuka maneno yao?

Hili ni funzo kwa viongozi haswa wa CCM kuwa tutawahesabu kwa maneno na matendo yao .
 
Njia za mwongo ni fupi sana hivyo hawa wameachwa uchi sasa unafikiri wanatamani hata kuyakumbuka maneno yao?

Hili ni funzo kwa viongozi haswa wa CCM kuwa tutawahesabu kwa maneno na matendo yao .

Nadahani Makamba yuko Mbioni kumwaga,na ukimya wake ni ishara inayokuja Mapema.
 
Vyama vya siasa huwa na kitengo cha kueneza Propaganda(au maneno sahihi kueneza uongo dhidi ya adui/mpinzani).Hata ktk mchakato wa kuchaguana ktk ngazi mbalimbali za uongozi/urais wengi walichafuana ili wapitishwe.Mara HIZBU,kala rushwa n.k.
Hili ni fundisho kuwa kumbe hata propaganda nayo in mwisho wake ambao ni aibu na fedheha.

Walitumia nguvu nyingi kuzima hoja za wapinzani,kumbe hawakujua wanazima matarajio ya watanzania na JALALI amewaweka peupeeeeeeeeee,Njia ya mwongo ni fupi.
 
Vyama vya siasa huwa na kitengo cha kueneza Propaganda(au maneno sahihi kueneza uongo dhidi ya adui/mpinzani).Hata ktk mchakato wa kuchaguana ktk ngazi mbalimbali za uongozi/urais wengi walichafuana ili wapitishwe.Mara HIZBU,kala rushwa n.k.
Hili ni fundisho kuwa kumbe hata propaganda nayo in mwisho wake ambao ni aibu na fedheha.

Walitumia nguvu nyingi kuzima hoja za wapinzani,kumbe hawakujua wanazima matarajio ya watanzania na JALALI amewaweka peupeeeeeeeeee,Njia ya mwongo ni fupi.


Mkira asante kwa hii mada .Wanaweza kusema ndiyo siasa lakini je heshima yao mbele ya jamii na familia zao inakuwaje baada ya ukweli kuja kuonekana baadaye ?Hata hili hawalijali pia ?
 
Mkira asante kwa hii mada .Wanaweza kusema ndiyo siasa lakini je heshima yao mbele ya jamii na familia zao inakuwaje baada ya ukweli kuja kuonekana baadaye ?Hata hili hawalijali pia ?

Mkuu Lunyungu,
Hebu jaribu kuvaa viatu hivi mwenyewe uone inakuwaje, jifanye Mwanry, Makamba, Makalla, Tambwe, Akwilombe nk. Unadhani hata mtaani kunapitika kirahisi? Kwamba uliokuwa unawatetea kwamba ni njaa inawasumbua ndio hao wanaonekana watetezi wa nchi!
Hii fedheha sijui wataiweka wapi ndugu hawa.
Kumbuka hapo tunasubiria ripoti ya akina Zitto na ile ya EPA!
Unadhani mpaka hapo Makamba atatoa wapi kauli?
 
wana JF,

These guys did a very stupid Job as propagandists! by definition propaganda is the use of 'persuasive communication techniques to influence human behavior or perception. Katika propaganda the target is the emotional part of a human being and not the rational part or logic!

Sasa hawa wenzangu na mie akina Kingunge and company wao wamezoea kuimba kama kasuku! A true propagandist will use the facts to persuade or to appeal to the emotional side of his audience and get a sympathetic response towards a certain issue. this is pure science na siyo kuropoka tu majukwaani!

nakumbuka mfano wa mama mmoja aliyekuwa na ndizi mbili za kugawa miongoni mwa watoto watatu huku akitaka kipenzi chake apate ndizi kamili. she gave one banana each to the two less favoured children, yule kipenzi chake akaanza kulia " nyamaza baba...hebu nyie wawili mgawieni mwenzenu basi...." wale watoto wawili waliona wamependelewa ( emotional )even though the third one ended with a complete banana (they didnt realize!- logical!) and they remained with a half banana each! Lakini wote walifurahia wakarudi kucheza!! now that is propaganda!!!!

Kuna mbinu mbalimbali za propaganda:
1. Uchafuzi wa majina: hii mbinu inalenga kuwafanya wanachi wamkatae mtu fulani au chama fulani bila kuzingatia ushahidi uliopo. Kwa mfano ni mara ngapi tumeambiwa Wapinzani tanzania siyo makini, ni wazushi, ni waongo, malaya, hawafanyi utafiti? hata tume ya mwakyembe iliambiwa hivyo. JK juzi alikuwa anaongea na wazee wa Dar es salaam. Kawageuza wazee wetu kuwa chekechea. Kawadanganya wazee waziwazi na hakuna hata mmoja kati yao aliyewaambia 'wewe kijana usitufanye siye wajinga nasi tunafuatilia mambo' No!Hivi hawa wazee wa Dar es salaam ni akina nani haswa? what qualifies one as 'mzee wa dar es salaam'? hapa wanataka ionekane kwamba huyu jamaa ana baraka za wazee! kiini macho! mfano mwingine ni pale aliposimama mudhihiri mudhihiri na kutoa hoja bungeni ya kumsimamisha Zitto...na bunge nalo likachukuliwa msukule na kupiga kura kukubaliana na hoja ya mudhihiri. Nia ni kumfanya zitto aonekane mzushi mbele ya wananchi. Of course the opposite happened! At that time i wish we had our own Cromwell to send the MPs packing!

2. Kujibandika sifa kwa maelezo ya kupamba: kwa mfano..'tunapigana vita ya rushwa kisayansi'what does this really mean? wakubwa wangapi wameshakamatwa na kushtakiwa kwa njia hii? mfano mwingine: Ndege yetu inapaa. je ni ndege gani hii? nani nahodha? abiria wake ni nani? watanzania walio wengi wamo ndani ya ndege hii? Mafanikio ya sasa yameletwa na sera madhubuti za chama cha mapinduzi. sawa. Je na ufisadi wa sasa umeletwa na sera za chama gani?

3. Kujihusisha na dhana/ watu adilifu ( kujibandika lebel ya uadilifu!) Kwa mfano mpaka leo hii kikatiba tanzania bado ni nchi inayojenga ujamaa. je hii ni kweli? ama kila wakati kiongozi akihutubia lazima atanukuu maneno ya 'baba wa taifa mwalimu nyerere' ama utasikia 'tunamuenzi mwalimu nyerere'..hii yote ni katika kuchezea hisia za watu kuhusu mwalimu ili CCM wahurumiwe! kuwapumbaza wananchi! Je ni kweli kwamba CCM inamuenzi mwalimu? Majukwaani sawa...kwa vitendo NO! kwamba bado kuna wananchi 'watakipigia kura chama cha Nyerere hata iweje'. Bado tuna hii issue ya 'mr clean' ambaye alizunguka dunia nzima akitambia ukaribu wake na Nyerere ( by the way is there a link bn kubadilika kwa mr clean anf the year 1999 when Nyerere died?) Pia sasa tunashuhudia hao hao waliomteua Lowassa wakikumbushia 'hata nyerere alimuona hafai!'

CCM bado inatumia alama ya Jembe na Nyundo kumaanisha kwamba ni chama 'kinachomilikiwa, kinaendeshwa na kipo kwa ajili ya wakulima ( kwa maana ya peasants ) na wafanyakazi (kwa maana ya labourers) wa Tanzania. Is this true? Kumbe ilisha tekwa nyara zamani na wafanyabiashara wakubwa. ( we are not talking about wamachinga here!). Angalia sakata zima la kima cha chini cha mishahara linavyopigwa dana dana hata haieleweki! Wananchi wanapandishiwa mshahara kwenye matangazo vyombo vya habari tu (propaganda) lakini ukweli ni kwamba walio wengi hakuna kilicho ongezeka na CCM na serikali yake vimeatupa wapambane peke yao na waajiri! chama cha wakulima na wafanyakazi indeed!!!

4. Kuungwa mkono na watu maarufu: hivi sasa mzee kichaka anatarajia kufanya ziara tanzania. hapo basi JK ataonekana wa maana kwa sana kwa vile yuko bennet na mzee kichaka! wapi na wapi. hiyo itapunguza bei ya umeme kwa mwananchi? hiyo itapunguza makali ya maisha kwa mwananchi? JK atajipatia ujiko wa kupambana na rushwa na ubadhirifu serikalini kwa kubadili baraza la mawaziri!!! je kuna anayeuliza kwa miaka miwili ya richmond JK alikuwa wapi kuchukua hatua? ama na yeye ameshtukizwa tu kama sisi? tutegemee kuona magazeti yetu yakiwa yamesheheni vichwa vya habari ' bush ampongeza kikwete kwa kupambana na ufisadi'......

5. Kujifanya mwanchi wa kawaida i.e. kuzuga: viongozi wetu wa sasa hata hili limewashinda. ukiangalia hata picha walizopiga kwenye kampeni za 'kupanda miti', mtu anaenda kavalia suti, inabidi atandikiwe khanga ili apigie magoti, a host of hangers on ready with shovels, and gloves...na wengine kupiga makofi! hakuna hata mmoja wao hawa anaweza kwenda kula kwa 'mama lishe' hata kwa kuzuga! hakuna hata mmoja anaweza kujiunga na wanachi mtaani kusafisha taka na mitaro, hakuna hata mmoja anaweza kusimama kijiweni somewhere kula supu ya mkia! hata walio na mashamba hakuna hata mmoja anaweza kushika jembe and do the actual digging! hakuna anayepeleka viatu vyake kwa fundi vikashonew!!!hakuna hata mmoja mwenye mtoto/mjukuu wake shele ya msingi mwembechai! hakuna hata mmoja ambaye naweza kuagiza itu gengeni. bei za gengeni ndio zinakupa ukweli wa ukali wa maisha kwa wanachi!!These guys are completely out of touch with the ordinary even their propaganda machine has completely forgotten this aspect!!One credit though ni kikundi cha capt john komba ( Tanzania one theatre) ambao wametumia muziki wa taarab kuwarubuni makabwela kuendelea kuiabudu CCM! yana mwisho wake haya!

6. Bendera fuata upepo: nakumbuka enzi hizo bado nikiwa UDSM, kulitokea kunji wote tukatimuliwa. CCM wakaidaka. Halmashauri kuu ikatoa tamko la kulaani wanafunzi kwa kumtukana matusi ya nguoni mzee ruksa! this set a condemnation domino effet for the entire country
. Kila NEC ya mkoa ikafuata, kila NEC ya wilaya ikafuata, the so called jumuia za chama nazo zikafuata, wananchi huko vijijini na mitaani nao wakafuata kuwalaani wanafunzi. hakuna mtu aliyekuwa anajali 'ni kwanini hasa wanafunzi waligoma? je ilikuwaje mpaka ikafikia hatua kuweka kunji? hayo yakasahaulika!!!na sasa tiyari naona msululu wa watu unampongeza lowassa kwa kujiuzuru (really?), na unampongeza kikwete kwa kuunda baraza 'jipya' la mawaziri ( what other choice did he have?). Je JK mwenyewe alihusika vipi na Richmond? Hii ni issue ambayo naona kuna watu wanataka ifunikwe kabisa!!

7. WOGA: Tanzania ni nchi ya amani na utulivu na CCM ndiyo chama pekee kinachoweza kudumisha amani hiyo! wengine wote wakichaguliwa..vurugu na mauaji. Bado nakumbuka kampeni za urais mwaka 1995. Television ya ITV ilitumiwa kuwarubuni wananchi kwamba wakichagua upinzani basi, Tanzania itageuka kuwa kama Rwanda!!(remember mauaji ya kimbari ya rwanda 1994, harrowing images were still fresh in the minds of most Tanzanians). Wakaitumia zanzibar na baadaye 'mwembe chai' (hivi nani aliwajibishwa kwa mauaji ya mwembe chai?)

Wananchi wa Tanzania siyo wajinga na walishabaini toka mwanzo 'usanii wa JK na serikali yake.' Kama alivyosema abraham lincoln "You can fool all people some of the time, and some of the people all the time but you can not fool all the people all the time".

Kazi kwenu mnaoamini CCM itaendelea kuwepo kwa miaka mia mbili ijayo!
 
By the way whereia Aggrey Mwanri? ilivumishwa atapewa uwaziri kulikoni?
 
Akina Makamba wako wapi?

Amepangishiwa nyumba nzuri ya kifahari na CCM huko Regend street(ya Daudi Mwakawago).

Lakini Makamba ana mji wake mzuri tu huko Tegete je huu si UFISADI NDANI YA CCM?
NI KWANI NINI ASIKAE KWAKE ILI HIZO HELA WAWALIPE MABALOZI/ NA WENYEVITI WA VIVIJI WA CCM. CHAMA KINA RUZUKU KUBWA LAKINI MGAWANYO NI WA KUPENDELEA MASIKINI HANA CHAKE LAKINI INAPOFIKA WAKATI WA UCHAGUZI NI HAO HAO WENYE VITI NA MABALOZI WANAOKISAIDIA CHMA KUSHINDA!

MAFISADI ONDOKENI MKIACHE CHAMA CHA MAPINDUZI ILI MUUNDE CHENU CHA MAFISADI NA KIONGOZI WENU ALIYETANGULULI KUWAANDALIENI MAKAZI YENU MAFISADI
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom