Nelson Masaduki
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 346
- 380
CCM imejivunia watu.Wote walikuwa upinzani. Nasubiri kuona Wema Sepetu, Nyalandu, Lowassa, Lissu, Sumaye, Kingunge kujiunga CCM. Ukitazama kwa makini utaona kwamba, upinzani uliobaki ni upinzani wa kupinga mazuri yanayofanywa na kuungana na watu walioko nje kuikosoa serikali hata katika mazuri yanayofanyika. Kama upinzani ungefanya kama wakati wa JK, kumkosoa mabaya anayofanya, basi tungesema upinzani unakua.
Leo tunahamasisha kumkwamisha Mh. ambaye anayafanya yale ambayo tulikuwa tunayapigia kelele kama wapinzani. Tumeongea sana kuhusu kupunguza safari, kubana matumizi, kuondoa posho zisizo za msingi, kutunzarasilimali za nchi, kupigania Utanzania wetu, kuwajibisha watumishi wabadhilifu na kuacha kuhamisha hamisha watumishi pale wanapokosea, kufanya maamuzi magumu na kupigania hali za wanyonge.
Kwa kiwango kikubwa, naona mengi anatekeleza na ndio kwanza mwaka wake wa pili huu. Tumuunge mkono, upinzani ubaki kidogo kukosoa wanapokosea sio kupinga mazuri.