Wakipinga kuvurugwa Upinzani Bungeni; CHADEMA watoka nje!

Sasa Naamini hatukuwahi kuwa na upinzani Bungeni kabla Ila sasa ambapo Chedema Imeonyesha upinzani Dhahiri hadi Sisiem wameona wabadili na kanuni za bunge Letu wananchi wa Tanzania, kuna mengi Hawabadili Ila wameona hili la kubadili kanuni ni mhimu waanze nalo kwakuwa ndilo lenye maslahi kwao, pili Hakuna upinzani imara uliofanikiwa kwa kuunganisha vyama kwa vyama angalieni hapo jirani zetu kenya pamoja na kuchukua dola kwa muungano wao wa vyama hawakufanikiwa kitu zaidi ya kuongeza machafuko tuu hata muungano ya kivyama Zanzibar ni Furaha za muda tuu ila nasema kwa nia njema sio sipendi zanzibar wakiungana hapana ila naamini muungano wa kivyama hauwezi dumu sababu kila chama kina mwelekeo na matakwa yake ambayo naamini ni tofauti na chama kingine kama kuna muungano basi uwe ni wa wanachama wote na wakubaliane kuua chama kimoja, kitakachotokea Zanzibar ni kufa kwa chama kimojawapo au cuf ama ccm Muda ndio utaamua angalieni kwa makini Hongera Chadema kwa kupinga kanuni wa upinzani kuungana kwa lazima Bungeni, Naungana nanyi kwa hilo japo si mwananchama.
 
Watarudi tu Bungeni hawana jipya lolote hao Chadema.

Hakika Uroho wao wa mabaraka na ubaguzi wao ndio unaowasibu lakini hawana ubavu wa kukataa posho.
 
Ndugunyangu labda hukuangalia mjadala mzima!! kuhusu hoja wameshindana na CDM was right kilichotokea CDM hawkutoka wakati wa kujadili hoja wametoka wakati wakupitisha hoja So wamepinga kuipitisha hoja kwa vitendo thats why wakatoka wakawaacha ccm na vibaraka wake wakitukana ovyo mwishowe kupitisha hoja kwa ndiyoooo kama mazuzu!!! so ukisema CDm walikimbia tatizo that is not true..isitoshe ww hukupiga kura ss tuliyo piga kura tukawatuma tumeona sawa:clap2: Au ulitaka wakae ndani washuhudie upuuzi ule nonononooooo!!!!GO GO chadema Tuko nyuma yenu
Ndugu, yawezekana kura yako ni bora kuliko zetu wengine... yawezekana pia ukawa unaona tofauti na wengine tunavoona. Lakini twapaswa kuangalia jana walitoka kesho wanarudi... je tabia hii ikiendelea yule mkulima aliyeko Nyamisati na Butuguri atazielewa hizo sababu na zitamshawishi kuendelea kubaki CDM? Lazima tutazame mbali zaidi kuliko ya tunapoona... "Mtu mmoja alipewa chai ya moto akawa anaipuliza ipowe, akaulizwa vipi wewe akajibu napoza chai, baadae kukawa na baridi akawa anapuliza viganja vyake akaulizwa tena vipi wewe? akajibu napasha viganja vyangu vipate joto!" yule mhifadhi akamwambia huwezi kunidanganya toka nyumbani kwangu!!" Maana aliona hayawezekani... Nasisitiza tunapaswa kuona mbali zaidi ya tunapoona ILA KWA SABABU VYAMA VYA SIASA TANZANIA VINA VITENGO VYA PROPAGANDA HAKUNA SHIDA NA TUENDELEE NA HIZI TOKA INGIA ZETU LABDA ZITATUINUA ZAIDI!
 
Watarudi tu Bungeni hawana jipya lolote hao Chadema.

Hakika Uroho wao wa mabaraka na ubaguzi wao ndio unaowasibu lakini hawana ubavu wa kukataa posho.
mkuu mbona unaongea kama umevuta bange?
 
wako sawa coz CUF wanaonekana kupania kuingamiza CHADEMA.
na kuangamia kwa chadema ni harusi kwa MAFISADI na chama chao.
 

Nashindwa kuelewa hawa chadema wanamatatizo gani maana wao katika sera zao wanasema kuwa wangeliunda serikali ya pamoja sasa wao wanakataa kuunda kambi ya upinzani ambayo miaka yote wao walikuwa wakishirikishwa, hawajuwi kuwa maendeleo haya letwi na chama kimoja, au wanataka kuondosha amani ya nchi yetu. maana huko ndio wanako elekea.

ndugu yangu kuwa na mtizamo mzuri co kwamba awataki wataunda kambi moja wakati cuf co wapinzani jamani muwe mnafikiri kabla ya kutenda
 
Nasikitika kusema wabunge wa CHADEMA, kwa mlolongo wa matendo yao,hawako kwa maslahi ya nchi hii......wako kwa maslahi yao binafsi na ya chama chao....ni watu wa kukurupuka,wasio heshimu mawazo ya wenzao na waliokosa mikakati sahihi ya ku-deal na wapinzani wao.....zaidi ni waongo kama CCM na CUF,ni wafitini na wachochezi sana.....kwa matendo yao si watu wa kuamini....lolote na liwe mradi wao washinde....hatufiki!!!! Bunge haliwezi kukaa kutimiza mapenzi ya CHADEMA watakalo ndo liwe,nasikitika kusema UPINZANI WENYE MASLAHI NA WATANZANIA HAUJAZALIWA TANZANIA........tuna wenye njaa na tamaa tu katika vyama vya siasa......nazidi kujihurumia na kuwahurumia watanzania,kwakuwa sasa nimeona hakuna mwema.......nakaribisha matusi.......ila sitashabikia nisichokiamini kwa kuogopa kutukanwa JF

Not sure kama nakuelewa hapa.....! just confusing yourself, hueleweki unataka kusema nini hapa! Husupport CDM na maamuzi yao, unakandia (kiaina) CCM & CUF.....! umeelewa ajenda nzima kwenye tukio la jana wewe?

Dada Michele,

Naona umebobea katika kutoa ushauri zaidi katika masuala ya urafiki. Siasa sio fani yako...!

How could you comment such words? Unaijua siasa wewe? Siasa ya upinzani daima huw ainaelekezwa katika jitihada za kutawala nchi yaani ubinafsi wa chama kimoja katika kushawishi wananchi ili wakipigie kura kuweza kuiongoza serikali.

Ni haki ya CHADEMA kutoka nje ya bunge ili kuonyesha msimamo wao au kuonyesha kutorishika kwao endapo itaonekana jitihada zao zinaingiliwa na CCM
....unajua watu wengine wanakasumba za ajabu, tukio la jana wangefanya wabunge ya Russia, Ukrane, UK, India, Malaysia etc ect on the same grounds wangesema, yes hizo ndo demokrasia za kweli na ukomavu kisiasa. Lakini kwa sababu hayo yamefanywa hapa kwetu wanabeza, bila kuangalia msingi hasa wa hicho kilichotokea jana!

Probably they are consistent in telling the truth..?,

Anyway binafsi sina Chama ila am patriotic na nina machungu na nchi yangu... Na ninajua kwamba CCM ndio Cancer ya hii nchi ni sumu mbaya kabisa na bila CCM kufa hakuna mabadiliko..., Hivyo basi Chadema might not be perfect lakini they are the best we have..., hata kama ni dawa na ninapenda Dakika Tatu, lakini nikikosa hiyo Paracetamol will have to do....

Kwahiyo we need upinzani (ambao ni Chadema) as well as system kubadilika ambayo ni Katiba ya kuweza kuwabana future viongozi.., The bottom line is CCM must go.., they are too big for their own good
.... I second you on this one bro....!

Am also patriotic,hakuna chama perfect....and i agree CCM has to go, no doubt.... what i oppose is their approach of handling CCM.....
....patriotic? not you with your such confusing & mixed up comments! How can you agree that CCM must go and yet you are behind it? Hypocrisy at its best....Lol!

Let them do what they have to do, CDM will grow stronger.

Wabunge wanasahau hawawezi kuendelea kufanya siasa kwenye matatizo ya wananchi!

Its not abt CDM this is all about the peoples' movement and wishes!
Nimeipenda hiyo kny pink......! yes, tumechoshwa na wanasiasa kutegemea mtaji wa kisiasa kwenye matatizo yetu....this has to end and sure it is going to end.....soon and very soon!

Kutoka nje ya Bunge ni Haki ya CDM nawaunga mkono kwa 100%.
Watu hapa wanaropoka kwa ufinyu wa upeo na pengine uwezo haba wa kutafsiri shule waliyo nayo.
Kila mara CDM wakigomea jambo na kutoka nje wanapanda Chati Kimataifa na kufanya Bunge la Tanzania lijulikane.
Wabunge wa Upnzani wakigoma pia wananchi wagome giza linatoweka na nuru inaingia.
Hiki ni pindi cha HIGH AWARENESS WORLD WIDE hii ni move ambayo CCM hawawezi kuizuia kwani ipo ndani ya chama chao pia.

Kelele nyingi hapa JF ni za woga wa mabadiliko ambayo waoga wanahisi yatagusa ulaji haramu walioukumbatia dearly.

Kama MH Obama alivyosema juzi juu ya Misri kwamba Once changes had occured there is no going back and most important dont even think of using old tricks to solve new problems as results of movement for change.


Shangazi yangu Anna kama alivyokuwa Baba yake enzi za mkoloni akiwa Halmashauri ya Njombe anaweka KAUZIBE isiyo na maana kwa maslahi ya Wachache ndani ya CCM.

Baba yake Anna, nadhani bado yupo hai, aliwahi kupinga pendekezo la DC mzungu wa Njombe kujenga shule ya sekondari miaka ya 1950 akidai Wanyalu hawako tayari kusoma shule kwani ni watu wa kukata mkonge tu. Kishaibu Makinda alikuwa Dead wrong leo hii tuna Wanyalu wasomi wengi kila kona ya dunia katika kila fani. Yeye Mzee Makinda anaota moto wa milingo na bastola yake pembeni Kule kijijini Yakobi.

Homuboi, huyu mama tunakazi naye akirudi kule kwetu labda agombee jimbo lingine! So usihofu, propaganda zao walizofanya mwaka jana hazitakuwa na nafasi tena mwaka 2015!

kinachonisikitisha mimi ni kuona hao wabunge toka Tanganyika ie NCCR, UDP, TLP wakicheza ngoma ya Wapemba (CUF), katika mradi wao wa kuhakikisha kila Mpemba anakuwa kiongozi nchini.

Ni aibu kubwa kwa kina Kafulila na Cheyo kubariki mradi huo wa CUF. Wamefanikiwa kule Zanzibar, sasa ni sehemu ya serikali, huku bara wanataka kuingia hata kwenye upinzani nako wachukue madaraka.

Tanganyika tukatae, tuungane na chadema kukataa upuuzi huu, wapigakura tuwashikishe adabu wabunge mamluki wa CUF na CCM, wakirudi majimboni, tuwakane, kwani wametusaliti.

Ni aibu kuwa na wabunge wa aina ya hao wa NCCR, TLP na UDP. Tanganyika tukatae huu utapeli kutufanya sisi mazuzu.

CCM wanaeleweka, kama wamemkabidhi RA uongozi wa nchi watashindwa vipi kuikabidhi Tanganyika kwa Wapemba!

Nikiambiwa mbaguzi potelea mbali lakini siko tayari kufa na tai shingoni
....Mkuu Nsesi mwaveja sana kwa hii post yako, mwenye macho haambiwi tazama! Umeweka maneno mazito sana kwa wenye macho ya ''NDANI''
 
Hiki na huu ndio mwanzo wa kifo cha CDM,nasikia hawarudi tena bungeni ?
 
Mzimu wa cdm utawaua ccm mwaka huu si ulisikia hata mwenyekiti wao alivyojikanyaga! Chadema kanyaga twende!
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!




22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
INGELIKUWA NI WASUSAJI WA KIUKWELI BASI WASINGELIRUDI KAMWE BUNGENI! Sidhani kama tuliwachagua na kuwatuma bungeni kwa ajili ya kutokatoka Bungeni na kisha kurudi. Sidhani kama kwa mtu yeyote mwenye kuifikiri na mpambanaji wa kweli anaweza kuwaunga mkono kwa hilo.
MIMI NASEMA SIWAUNGI MKONO NA KITENDO KILE WALICHOKIFANYA NI UPUUZI MTTUPU. WAMEONESHA KWAMBA WANAYAKIMBIA MATATIZO BADALA YA KUYAKABILI. WANGELIBAKI PALE NA KUJENGA HOJA, MAANA HOJA HUJIBIWA KWA HOJA. JE MTU NYUMBA YAKE IKIINGIA SIAFU HUWA ANAIKIMBIA? KWA MTINDO HUU WANAOENDA NAO CDM WANAJIMALIZA WENYEWE... MAANA WANASEMA WASWAHILI MKATAA WINGI MCHAWI. IKIWA SABABU NI UBINAFSI BASI WAKAUNDE KABUNGE KAO NJE YA BUNGE LA JMT. MAANA WATAENDELEA KUTOKA BUNGENI KILA WATAKAPOKINZANA NA HOJA ZA WENGINE, TUTAENDELEA KUWASIKILIZA NA MWISHOWE TUTAWACHOKA KWA MAANA TULICHOWATUMA BUNGENI NI ZAIDI YA WANACHOKIFANYA. HATUKUWATUMA BUNGENI KWENDA KUGOMBEA MADARAKA... TUNA SHIDA NA MATATZO MENGI... WAACHE MAMBO YA KITOTO WAJUE WAPO PALE KWA AJILI YA WATU WANAOWAWAKILISHA NA WASIDHANI KWAMBA WOTE WALIOWACHAGUA NI WANACHADEMA BASI NA WAITENDE ILIYO HAKI KWA WALIOWACHAGUA.

Uliwachagua?Pigia kura?
 
sidhani kama hiyo hatua inaleta tija yoyote kwa wananchi wa kawaida

Tumeshajua CCM ni wababe na wameshika mpini, pia tukumbuke kuna akati hata tanu walishiriki uchaguzi wakijua si huru wala haki ili kuwa-surprise wakoloni.... basi tujifunze kutolerate differences

CHADEMA wangebaki, waungane na wapinzani na waanze ku-lobby kufikisha agenda yao na hata ikibidi kufanya vikao vya mara kwa mara... kumbukeni wanasiasa wote ni wanafiki hivyo basi kubadilika isingekua tabu as long as keki imewekwa mezani na kila mtu anajua mwenzake kapata kipande ngapi

Hacha busara za kwenye usuluhishi wa ndoa za mkeka.
 
nimegundua kuwa wewe ni mshabiki mzuri ambae nadhani una urafiki na Kibonde (au watu wenye akili kama za kibonde) au unatumia muda mwingi kumsikiliza kibonde bila ya kufanya tafakari ya unachokisikia.

sasa naomba nikueleweshe kidogo. umezaliwa umezikuta sheria zinazokuongoza, hukuzitunga wewe lakini kwa kuwa umezikuta huna budi kuzifuata. walichokifanya CHADEMA leo ni kutoshiriki kupitisha kanuni Kandamizi lakini ikipitishwa bila ya wao kuwepo wakija wakaikuta ipo hawana jinsi itabidi waifuate. ugomvi wao haupo kwenye kuunda kambi moja na wenzao ila upo kwenye MISINGI ya KIMTAZAMO wa watu hao wanaotakiwa kushirikiana.na hadi naandika post hii tayari wamesharudi ukumbini.

kwahiyo natumai umenielewa ukiwaona kesho kwenye kikao wala usishangae na kupiga kelele.. Senkyu!
am loving ur jibu
 
wanaolala bungeni ndo wanasubiria posho, mishahara:
CDM wanaangalia maslahi ya wananchi wao, na nchi kwa ujumla.
Fikiria kwanza

Ha ha ha ha, Mkuu Ki tochi umenikumbusha picha ya Kapt. Komba (CCM) kwenye Mwananchi ya leo, kanaswa akiuchapa usingizi Bungeni, eti anafuatilia mjadala kwa makini!!!
 
NILIDHANI JF NI KWA WATU WENYE ELIMU, kumbe hata chekechea, hausgal, mama ntilie,wote wamo. KaZ KWEL KWEL!

Please Pasco, civilized and restraint. Hao uliowataja nao ni watu na pengine ni raia wema wa Tz. Usipuuze wala kubagua mtu maana ktk ukombozi kila mchango na mawazo unahitajika wa kila mtu, tasnia nk.... ili mradi awe na nia njema ya kujenga sio kubomoa
 
Time is an intelligent master. That's why things don't remain static nor unchanged.

Seemingly CCM are (luckly for Tz) not aware of this fact of history.

Mubarak and his echelon condemned a great nation of Egypt to a systematic repression under the farce "Emergency Law" for over 30 years, but today before our very own eyes we're seeing an upturn and desired change there. Surely Tz cannot consider herself isolated and abated. For a fact most of the detested things wrapping the daily outrcy in Tz are not dissimilar to Egyptians' ones.
 
Back
Top Bottom