Wakiondoka/wakirejea, umati uwanjani - Mapenzi, ushabiki au unafiki?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Viongozi wetu wakisafiri umati wa viongozi na wananchi wengine huenda 'eapoti' na wakirejea hupokelewa kwa mbwembe....nini kinawasukuma watu kuacha kufanya kazi na kupoteza muda na rasilimali?

mak.JPG
Mfano: Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anna Makinda akilakiwa na Wanachama wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana Muda mfupi baada ya kurejea nchini akitokea nchini Namibia kuhudhuria mkutano wa Bunge la SADC
 
Kutafuta nafasi za kuteuliwa maana ni nyingi mno hapa Bongo, Halafu zina ulaji na tena hazizingatii umekula kitabu kiasi gani, ila unajipendekeza kwa kiasi gani
 
unafiki + kujipendekeza + dhiki (njaa), kama fisi anayenyemelea mfupa(wao vyeo) !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tena cha ajabu utakuta siku nzima hawajapewa hata maji,nadhani ni mikakati ya kisiasa ,mbwembwe na kuwakoga wapinzani wao
 
Njaa zimetawala, tena wengine wameenda shule, lakini tamaa zimewatawala.:redfaces::redfaces::redfaces::redfaces::redfaces::redfaces:
 
Unafiki tu unawasumbua na kutaka kujipendekeza2 tu lengo wakumbukwe kwenye uteuzi mbalimbali si unajua hapa bongo kujuana lakini si kwamba wanamapenzi mema na huyo wanayekwenda mpokea.
 
  • Baadhi ni kujipendekeza
  • Wengi wao hawana cha kufanya (wako idle) hivyo ni katika kupoteza wakati
  • Wengine ni vibaka, wapo mawindoni
 
Kumbuka iliundwa kamati na fungu kubwa lilitengwa,we fikiri kununua hayo maua waliyobeba tu si chini ya laki 3 ,bado magari waliyokodi,na mambo mengine kemkem.Je huu si tayari ulaji wa mtu??Kaka hayo ni matumizi yasiyo na tija na maendeleo ya taifa letu.Bajeti hii ikiwa hivi kwa viongozi wote kupokelewa na hii ni mkoa wa dar,je hii fedha inayotumika hovyo ingelipia watoto wangapi shule???

Watanzania tuamke tukatae hii hali,tuseme sasa yatosha tunataka maendeleo na si sherehe zisizo na kichwa wala mguu.Kutwa nzima watu ameshinda airport badala ya kuwahudumia wananchi.Ofisi ya hawa wakina mama siku hiyo ilihudumiwa na nani????
 
Back
Top Bottom