Wakina mama mnatisha kwa kuficha hela chumbani

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
453
628
Wakina mama mnatisha kwa KUFICHA HELA CHUMBANI!

Kwa kweli wanaume wenzangu kila nikipata fursa ya kufanya usafi chumbani kwetu au kutafuta kitu fulani kwa makini, LAZIMA nitazifuma alfu 20,30 mpaka 50, zimefichwa sehemu na mama watoto! Tunazo akaunti za akiba za watoto wetu, wako sorted;).

Ila kwanini bado anazificha hizi hela ndogo ndogo kule?! Na kwanini anasahau?!
Nakubali nikizipata huwa zanisaidia sana kulipa bili kwenye local yangu (bar ya mtaani kwetu).

Nashea nanyi hiki kisa sababu nashangaa huwa haulizii wala kutahamaki! Labda anakuwa kazisahau aise! Au labda ni zangu zinazochomolewa usiku nikiwa tingasi..

Kwa kweli ule usafi wa master nilishatamka ni wangu yeye aweke mguu tu! Mnaelewa kwanini;););)..
 
Wanawake ndio hapo ninapowakubali, huwa wanajibana na kuweka akiba...ili hali ikiwa tete home inasaidia kidogo
 
Usiwe unazichukua Mkuu , wamama wana akili sana za kuweka akiba kuliko wanaume. Au unataka hata Ped awe anakuomba?
 
Dah, seems mkeo ni inventer mzuri, amebuni njia rahisi zaidi ya kukufanya ufanye usafi.

yaan unafanya usafi bila shuruti na meno 32 nje
 
Wakina mama mnatisha kwa KUFICHA HELA CHUMBANI!
Kwa kweli wanaume wenzangu kila nikipata fursa ya kufanya usafi chumbani kwetu au kutafuta kitu fulani kwa makini, LAZIMA ntazifuma alfu 20,30 mpaka 50, zimefichwa sehemu na mama watoto! Tunazo akaunti za akiba za watoto wetu, wako sorted;).
Ila kwanini bado anazificha hizi hela ndogo ndogo kule?! Na kwanini anasahau?!
Nakubali nikizipata huwa zanisaidia sana kulipa bili kwenye local yangu (bar ya mtaani kwetu).
Nashea nanyi hiki kisa sababu nashangaa huwa haulizii wala kutahamaki! Labda anakuwa kazisahau aise! Au labda ni zangu zinazochomolewa usiku nikiwa tingasi..
Kwa kweli ule usafi wa master nilishatamka ni wangu yeye aweke mguu tu! Mnaelewa kwanini;););)..

Ameshakujua wewe mwizi wa hela zake amekuzoea
 
Wana wake wengi ndiyo wanaoongoza nyumba ktk kuhakikisha mambo yanafanyika Hata kama mwanaume hana Kitu mfukoni.

Wanawake MUNGU amewapa kujali sana familia Hata siku mmoja hawezi kuacha wanafamilia bila kuhakikisha kimepikwa Hata kwa kuokoteza kwa hizo akiba zao.
 
Chumba mnatumia wawili akipotelewa na kitu anajua ni wewe tu.

Anakuchora tu wewe unajiona mjanja.

Wakina mama mnatisha kwa KUFICHA HELA CHUMBANI!
Kwa kweli wanaume wenzangu kila nikipata fursa ya kufanya usafi chumbani kwetu au kutafuta kitu fulani kwa makini, LAZIMA ntazifuma alfu 20,30 mpaka 50, zimefichwa sehemu na mama watoto! Tunazo akaunti za akiba za watoto wetu, wako sorted;).
Ila kwanini bado anazificha hizi hela ndogo ndogo kule?! Na kwanini anasahau?!
Nakubali nikizipata huwa zanisaidia sana kulipa bili kwenye local yangu (bar ya mtaani kwetu).
Nashea nanyi hiki kisa sababu nashangaa huwa haulizii wala kutahamaki! Labda anakuwa kazisahau aise! Au labda ni zangu zinazochomolewa usiku nikiwa tingasi..
Kwa kweli ule usafi wa master nilishatamka ni wangu yeye aweke mguu tu! Mnaelewa kwanini;););)..
 
hahaha! umenifurahisha sana mkuu, eti au ni za kwangu anachomoa nikiwa tinga! Wanawake wanaakili nyingi mkuu mimi sinywi wala sivuti, kuna siku nilikuwa sina kitu kabisa nikajua leo ni siku ya kumkagua fundi wa dari yetu na kumpongeza kwa kupiga miayo! Lakini cha ajabu nikashangaa huyu mwanamke sijui kazitoa wapi hela nakuta msosi wa maana mchana hadi usiku!

Hawa watu wanaakili nyingi wanajua kuna wakati hela itakata pia anaweza kutembelewa ghafla na mgeni na wewe labda huna kitu au upo kazini inabidi awe na chochote ili kuua soo.

usiwe unachukua vihela vya shem mkuu.
 
MTOA MADA kaa ukifahamu unafanyishwa usafi wa chumbani kwenu na malipo yako ni hizo hela anazokuwekea sehemu za kificho kuhakikisha kuwa umefanya usafi hadi huko mahali alikozificha. Heheheheheheee hutokaa uelewe maana anayoimaanisha mwanamke hata siku moja wee mpende tuu akihorojeka na penzi lako atakumwagia ukweli wote bin siri zake zote.
Wajanja wanasema unafikiri umepata kumbe umepatikana.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom