Wakina mama: Chungeni sana kauli zenu

Nadhani hujaelewa msingi wa mada....si kwamba wanawake wanalaumiwa la hasha bali wanashauriwa kuwa breki kwenye midomo yao.....kuna baadhi ya kauli zinaweza kukusababishia mabalaa kwani zinachoma mno....chungeni midomo yenu.....

Hivi huwa mnadhani sisi tuna mioyo ya chuma ama sisi sio binadamu wenye hisia??? Nanyi muwe na break na uchafu wenu...
 
Hivi huwa mnadhani sisi tuna mioyo ya chuma ama sisi sio binadamu wenye hisia??? Nanyi muwe na break na uchafu wenu...

Kama hamtachunga midomo yenu kila siku tutasikia mmecharangwa mapanga na kuuwawa kwa sababu ya viburi vyenu na kauli zenu chafu......endeleeni ili tuendelee kugawana majengo ya serikali.......
 
Unatukataza kwenda bar tena? Utaenda wapi sasa mahali ambapo ni kwa watu wote? Kwanza bar hata ukikaa tu bila kuagiza kitu hawakufukuzi.
 
Ndiomana mkaambiwa muishi nasi kwa akili.... Siwezi from nowhere kukurupuka nikakurushia maneno kama hujanichokoza
 
mwanamke anaebishana na mme wake au kumtolea maneno machafu ya dhihaka uyo hana hekima na kwao akufundishwa kua na heshima kwa mme wake.Dawa ni kumrudisha kwao wakamfundishe heshima.
je kama yeye ndie anayekuweka mjini? ndie anayekufanya upate haja kubwa, uendeshe gari la kifahari, uishi "uzunguni", watoto wasome shule za kifahari, upande pipa kwenda south and the like!!!!!
 
Ndiomana mkaambiwa muishi nasi kwa akili.... Siwezi from nowhere kukurupuka nikakurushia maneno kama hujanichokoza
Kwakwel nimependa huu mchango wako kwa kusema ukweli... Kama vp nitumie number yako nikupe walau kazawadi
 
You are very right broda,nikiskia wanandoa wametupiana maneno au na ngumi huwa najiuliza,hivi hawa walipendana kweli au walilazimishwa ndoa? Unafanya vizuri kutoyapa haya nafasi kwenye ndoa yako,uzidi kubarikiwa.
Thnx for Good wishes, you too May God lead you.
 
je kama yeye ndie anayekuweka mjini? ndie anayekufanya upate haja kubwa, uendeshe gari la kifahari, uishi "uzunguni", watoto wasome shule za kifahari, upande pipa kwenda south and the like!!!!!
Kama ni hivyo mkuu hizo fujo zitaanzia wapi, kwanza hata akikuudhi una ubavu wa kurusha neno??
 
Sio wanawake tu pia kuna wanaume wanakauli mbaya harafu anaongea mbele ya watoto.
 
Sito sahau katika ugomvi Mume wangu alinambia anajuta kuowa duuu niliumia rohon ila nikasema ngoja na mie nimtaftie lakumuumiza nilimwambia yaani we unatabia za kike sana angalia usije olewa
Akanambia ntafutie bwana nikamwambia tafuta na kadi ya harusi niletee ntakupa mchango hahahaht hhahat hasira ziacheni tu jamani ukiwa na hasira waweza toa kauli mbaya sana nikimwangalia Mume wangu katoka job kavua kombati zake nakumbuka ile kauli namwambia mungu nisamehe japo na yy tuliombana msamaha kwa kila mmoja kumtusi mwenzie kwa kauli za kuumiza
 
Sijui kwanini nimefungua huu uzi aiseeee....
Nimejikuta nakumbuka neno ambalo nilikua nikilitumia sana (nahitaji private time).
Lakini chakushangaza ndipo ilikua kama nachochea kuni kwenye kijinga cha moto agghhhh...
Niliposema nitoke, basi nilifuatiwa na SMS, MMS za maneno na matusi kama mvua......
Mwisho nikaona nitafute pakua napata pumziko aiseeee.....
Ebu ngoja niishie hapa maana nahisi mapigo moyo kuanza kunienda kwa kasi
polee
 
Sito sahau katika ugomvi Mume wangu alinambia anajuta kuowa duuu niliumia rohon ila nikasema ngoja na mie nimtaftie lakumuumiza nilimwambia yaani we unatabia za kike sana angalia usije olewa
Akanambia ntafutie bwana nikamwambia tafuta na kadi ya harusi niletee ntakupa mchango hahahaht hhahat hasira ziacheni tu jamani ukiwa na hasira waweza toa kauli mbaya sana nikimwangalia Mume wangu katoka job kavua kombati zake nakumbuka ile kauli namwambia mungu nisamehe japo na yy tuliombana msamaha kwa kila mmoja kumtusi mwenzie kwa kauli za kuumiza
ah ah ah ah jamani, nacheka kama mazuri, pole sis
 
maneno huwa yanaumiza sana, shida neno lilitoka haliwezi kurudi katika kinywa, Mungu atupatie hekima na busara ili tuweze kuishi, hii sio sisi tu wamama , hata nyie wababa mna hiyo tabia ya kutusema maneno mabaya, tena kuna baadhi ya wanaume mna maneno kuliko wamama, kikubwa ni kila mtu achunge mdoomo wake, na tumuombe MUNGU atupatie busara na kukaa kimya, wakati mwingine kukaa kimya ni kuzuri, lakini ni kubaya pia mfano

mimi nimefanya kosa halafu halafu mwanaume unikalie kimya, aisee siwez kuwa normal nitakuchokoza tu useme, usije niua usiku kwa mapanga mimi tena watu wanao kaa kimya, they are bad kabisa, wanakaa na vinyongo mno. MUNGU atupatie busara zaid tuishi kwa kuvumiliana. and asante mleta uzi umenipa kitu hapa
 
ni kweli mtu aliyeumizwa halafu akakaa kimya ni wa kuogopwa siku akilitoa ni patashika..ndo maana wenzetu wazungu mtu ukiumizwa kama unackia kulia bac wanakuambia lia utoe kitu kilichojaa kifuani
 
Na baadhi ya wanaume nao wana kauli za kuchoma. Utamsikia mume wako anakwambia, ni afadhali mke wa fulani akiguswa tu anapata mimba. Wewe hadi leo umeshindwa hata mimba ya bahati mbaya! Jamani, kweli kuna mwanamke kwenye ndoa asiependa kupata mtoto?
 
Back
Top Bottom