Wakina Dada/Mama wa JF mbona mnalikimbia jukwaa la Siasa.

walioweka majukwaa tofauti wana akili zao timamu

sawa lakini ukilala ukiamka maisha yako yanaendeshwa na SIASA,angalia mwanasiasa amepandisha bei za umeme,wewe unaumia moyoni tu,wewe ni daktari uligoma kudai haki zako mwanasiasa akasema usigome nitakufukuza kazi,etc.
 
kule kuna watu wanajifanya ni controller wa jukwaa la siasa ukienda huko ukitoa mchango wale controler wanakuja kucrash tu,,,,,,,, na me huwa nikijisikia kukera watu naenda huko nawachefua natoka..............

Madame B wangu yeye anapenda siasa...

by the way wengi wanapenda mapenz ndo maana wamejaaa MMU name chitchat
 
Last edited by a moderator:
Binafsi si shabiki sana wa siasa ila huwa nikikutana na title ikanivutia huwa naingia ila sithubutu ku comment!
Kuna watu wana fedhuli kule nami najijua kichwa changu huwa kinapata moto ningepewa ban kila baada ya dkk 5!
 
Habari wanajamvi, Hii topic ilitakiwa iende kwenye Jukwaa la Siasa lakini kwa kuwa walengwa wakuu wako huku nimeona ni vema niitupe huku. Nimekuwa najiuliza swali, kwanini Wakinadada/mama wengi huwa wanatoa michango yao kwa wingi kwenye Jukwaa la MMU lakini kwenye majukwaa mengine hasa lile la Siasa hawaonekani kabisa tofauti na Wanaume/Vijana wa Kiume maana wengi wao wanacheza pande zote. Naomba walengwa waniambie, tatizo ni nii, je, ni waoga wa siasa? Na kama ni waoga wa Siasa je, hii Hamsini, Hamsini wanayoitaka kwenye Uongozi wataipata, au waendelee kupata upendeleo? Acha kunywa maziwa tu jaribuni na nyama ngumu. CC Faizafoxy a.k.a Mrembo. Mamdenyi na wengine wanaothubutu.

Mkuu kule kunataka kichwa ngumu maana kuna maudhi ya kila aina,kama una roho ndogo hukawii kurusha ngumi.
 
Kina dada sina hakika sana ila kina mama ukitaka uwapate siasani,wape pilau,khanga na vilemba vya bure hasa wa chama cha.......
 
upo kimahabati zaidi enhee..
He he he lol sielewi siasa na sina interest ya kuelewa kwa kweli najiona nitakuwa nabishania vitu ambavyo havina msingi wowote wala manufaa yoyote kwangu kama natwanga maji kwenye kinu....And why should i waste my energy doing something useless!!
 
Mimi kule huwa napita ila sichangii..kwa sababu moja tu sioni msingi wa mambo mengi yanayoleta mabishano...siasa inafunika ukuaji wa uchumi pia inagawanya watu wanashindwa kutathmini na kutumia maliasili kujikuza kiuchumi...hii ndyo sababu inayonifanya niichukie siasa..
 
Mkuu kule kunataka kichwa ngumu maana kuna maudhi ya kila aina,kama una roho ndogo hukawii kurusha ngumi.

Itabidi atafutwe Faiza awape training ya jinsi ya ktstaimili lile Jukwaa.
 
Kule hawana cha WEKA PICHA lazima ujiandae kuitwa msukule,kilaza,masalia,gamba,mchumia tumbo,bw..ge,ndom ya .....
Hayo yote ya nn wanaona bora huku MMU.
 
Na ikitokea mkatofautiana kwenye hoja ya msingi utasikia,"hivi hauna hata kaboyfriend kakukuscrew muda huu maana naona unajambajamba Tu"
Kule Ni uwanja WA fujo balaa lazima kichwa kiwe na sebule.
 
Jukwa la siasa sio huru, wapo wanaolimiliki na wamesheheni multiple IDs na matusi mithili WAMEYASOMEA.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom