Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,245
....Mnasahau kuwa yote mtendayo katika karne hiii yanaandikika
....Mnasahu kuwa katika jamii zetu majina ya ukoo ni utamaduni mkubwa na wa kuendelezwa kizazi hadi kizazi
.....Mnasahau kuwa tukio kubwa moja miongoni mwa wanafamilia ndiyo mwangwi na taswira wa familia hiyo machoni pa wanajamii
.....Mnasahau viapo mlivyo kula mbele ya wananchi kuwa mtalitumikia taifa letu na wananchi wake kadri ya uwezo wenu kimawazo na kivitendo
......Kifupi, mnaacha aibu kubwa katika familia zenu. Pamoja na kuwa kila mmoja anahukumiwa kwa vitendo vyake, msishangae kuona familia nzima zinahukumiwa kutokana na tamaa na ubinafsi wenu kizazi hiki na kijacho. Mnatia madoa majina masafi ya familia. Na kwa vile jamii nzima imezingirwa na matendo ya rushwa na ufisadi wa kila aina; makalipio, lawama, mafunzo, ushauri na yote yanayoweza kuwasaidia kuachana na vitendo hivyo hayafanikiwi wala kuwafikia. Pia kwa vile familia na jamii kwa kujali tamaduni zetu zinajikuta zikikaa kimya kuwasuta kwani bado mnategemewa kifamilia; basi uhalalisho wa vitendo vyenu vya utomvu umekuwa ukipata msukumo usiokusudiwa na usio pingamizi.
SteveD.