Wakimbizi wa Rwanda Burundi 8000 Wapewa Uraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakimbizi wa Rwanda Burundi 8000 Wapewa Uraia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by muhosni, May 17, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maokola Majogo, Waziri na Mbunge mstaafu katika kipindi cha Tutafika Channel Ten leo.

  Amesema serikali imeandikisha wakimbizi 8000 waliokuwa kambini kutoka Rwanda, Burundi, na DRC na kuwapa uraia wa tz. Amesema wametawanywa sehemu ambalimbali tz na mkoa wa Lindi pekee wamepelekwa 3000.

  Amesema hawa watu kwa kawaida huwa na pesa nyingi kuliko wenyeji na hujitahidi kuchukua uongozi wa vijiji. Kisha hunyang'anya Ardhi ya wenyeji. Kisha kutakuwepo migogoro ya Ardhi.
   
 2. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  iyo kali, yangu macho
   
 3. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MImi nimeisoma kwenye gazeti la nipashe la leo kuna hiyo habari!habar yenyewe inasema kwa ujumla wapo wakimbiz 8000 waliokamata uraia wa Tz!
   
 4. k

  kiloni JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mr MISIFA JK yuko radhi kutuuza hata sisi kwa misifa tu.
  Hayo yalikataliwa toka Kipindi cha Nyerere. Kwa hiyo wakenya karibuni katika shamba la Bibi msingoje tena makubaliano ya Jumuia ya Africa ya Masharika.
  Kikwete ni Janga la Kitaifa. Tumekwisha!
   
 5. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Bongo tambalale,mgeni anapewa uraia na ardhi bure lakini mzawa unauziwa plot Tshs 10,500/- per square meter,halafu tunakaa na kujisifu kuwa hii ni nchi yetu!!! Ujinga ulioje huu!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tanzania gives citizenship to 162,000 Burundi refugees


  [​IMG][​IMG]

  The UN has praised Tanzania for granting citizenship to some 162,000 refugees who fled Burundi 38 years ago.

  "It's the most generous naturalisation of refugees anywhere," said UN refugee agency spokeswoman Melissa Fleming.

  UNHCR head Antonio Guterres described it as a "historic moment" and urged other countries with long-term refugees to follow Tanzania's example.

  Until 2000, Tanzania had one of Africa's largest refugee populations, 680,000, from Burundi and DR Congo.

  Some 350,000 Burundians have returned home in recent years, says the UNHCR.

  A UN spokeswoman said most of those granted Tanzanian nationality were Hutus.

  They had mostly fled conflict with the Tutsi-dominated army.

  The spokeswoman said they were already integrated into Tanzanian society and were not living in refugee camps, reports the Reuters news agency.  Source: BBC | RFI
   
 7. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Ah ah ah ah jamani lazima yatokee ya south africa kwa mtindo huu.
   
 8. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Kweli nimeamini Tanzania ni shamba la bibi. Hapa ndipo tunatambua serikali ipo kivikwake na wananchi wapo kivikwao. Kwa serikali kugawa ardhi ya watanzania ni maamuzi marahisi lakini kwa mafisadi ni maamuzi magumu.
   
 9. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ninachojua mimi, Serikali ya Tanzania, Serikali ya Burundi na UNHCR wameona ni vema kumaliza tatizo la wenzetu, ndugu zetu na majirani zetu waliokimbilia Tanzania mwaka 1972 kwa kuwatengamanisha na jamii (local integration). Mimi nimezaliwa miaka ya hiyo. Wengi wao wamezaliwa hapa, wamesoma hapa, tunafanya kazi nao na tumeona nao! Ninadhani Serikali imeamua kuwatambua na kuhararisha ukazi wao, ubaya uko wapi?

  Mwaka 2003, Serikali ya Tanzania ilifanya zoezi kama hilo kwa wenzetu, ndugu zetu na majirani wasomali-wazigua kwa kuwatoa Mkuyu-Handeni na kuwahamishia Chogo-Tanga. Mbona hatuongelei juu hao? Kulikoni hawa?

  Ninaomba ubofye hapo chini, upate habari zaidi. Lakini pia unaweza kutafuta kupitia google juu ya hii habari.

  Rai yangu: Jamii isipotoshwe juu ya hili swala!

  UNHCR - UNHCR welcomes Tanzania's decision to naturalize tens of thousands of Burundian refugees

  Wakimbizi wa Somalia wapewa uraia

  http://www.fmreview.org/FMRpdfs/FMR33/35-37.pdf
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  2mekwenda na maji Ndg zanguni. KIKWETE NA MAWAZIRI WAKE NI JANGA KWA TAIFA JAMANI!! Mmmh,mmmh.hapana.
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hawa wakimbizi wana haki kisheria ya kupata uraiya wa Tanzania.
   
 12. F

  Future Bishop Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hapa tunaongelea waliokuwa wanaitwa wageni wakaazi kwa jinsi mwalimu Nyerere alivyokuwa anawaita kutoka makazi ya Katumba, Mishamo (Mpanda) na Ulyankuru (Tabora). Waliingia nchini kama wakimbizi miaka ya 1971/1972 kwa hiyo wameishi nchini kwa takribani miaka 40. Walipewa ardhi ya kutosha kulima kwani hawakuwa wanaishi kwa misaada ya vyakula vya WFP/UNHCR kwa hiyo walijitegemea. Serkali kwa kushirikiana na Shirika la UNHCR walihakikisha huduma zote za kijamii zinapatikana/kutolewa kwao. Mtaala wa elimu waliopewa ni wa Kitanzania na kwa hiyo wengi wao wamesoma shule ambazo tumesoma na wengine kupata bahati ya kuajiriwa kwenye ofisi za Serkali na mashirika ya Umma na Mashirika yasiyo ya Kiserkali.

  Mwaka 2007 ilipitishwa sensa maalum (Serkali na Umoja wa Mataifa) ya kuwaomba kuchagua kati ya kurudi nyumbani kwao (Burundi) kwa hiari au kuomba uraia wa Tanzania. Kwa kuwa idadi kubwa ya vijana walizaliwa hapa hapa Tanzania na wengi wao hawajui hata huko kunakoitwa Burundi, wengi wao waliamua kuchagua kuomba uraia wa Tanzania. Ni wachache tu walioamua kurudi kwa hiari na hasa wale waliotoka Burundi miaka hiyo wakiwa watu wazima ambapo sasa ni wazee.

  Kutokana na historia hii na kwa kuwa wamefuata taratibu za kuomba uraia wa Tanzania sioni shida kwa wao kupewa haki ya kuwa watanzania.
   
 13. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani kwani hapa serikali imefanya kosa gani? Kutoa uraia kwa watu hao mbona ni kitu cha kawaida tu kwani hao ndio wa kwanza kupewa uraia Tanzania? mbona wapo wengi tu waliokwisha pewa uraia kabla ya hao au kwa kuwa ni kundi moja kwa mara moja ndo mnatishika? Isitoshe wale ni Watanzania kama sisi tu kwa kuwa wengi wao wamezaliwa tz, kusomea na kukulia tz sasa katika mazingira hayo mlitegemea waende wapi tena? hakuna nchi nyingine wanayoijua zaidi ya tz, na naamini ni wazalendo wa nchi ya tz kuliko hata sisi tunaojiona ndio watz wa asili. Tatizo ninaliliona mimi, kama ni kweli maana sina uhakika ni habari ya kusikia tu kwamba zile kambi za katumba na mishamo walikokuwa wakiishi wamenya'nganywa na kuuzwa kwa wamarekani, hapo sasa ndio tatizo, kwa kuwa walitakiwa wabaki pale wakiendelea na kilimo, na kidogo kidogo wangekuwa wakijichanganya na watz wengine kwa kuhamia maeneo mengine, na vilevile watz wengine kuhamia huko.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,847
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280


  Kiusalama uamuzi wa serikali ni sahihi....ni bora kuwa na wahamiaji hasa walio kaa muda mrefu na kuwatambua kuliko kuendelea kuwaacha wawe wahamiaji haramu......na ni busara kuwaweka hao wakimbizi waliopewa uraia mbali kabisa na mipaka yetu na nchi husika ..ie kama hao waliopelekwa Lindi...lazima kuwe na buffle zone kati ya mipaka ya nchi zenye msongamano na zisizotabirika kama Rwanda na Burundi...itakayokua inadhibitiwa na JWTZ...ili kuzuia yaliyotekea Congo kwa wahamiaji wenye asili ya Rwanda ,banyamulenge...kutaka kuwa sehemu ya Rwanda.....,Tusikubali hata kidogo kwa wahamiaji wa rwanda na burundi kuwa sehemu za mipakani.....zaidi ya baadaye kuwa mbinu ya nchi zao zisizo na Ardhi kujipanua..pia wanaweza kuendesha shughuli za uasi ndani ya nchi yetu dhidi ya serikali zao.................

  Huo woga wa kuwa waliopewa uraia watateka uongozi wa sehemu husika ni kazi rahisi....ni kuhakikisha kuwa hawapitishwi kugombea uongozi ..lazima system ifanye kazi...na hilo walijue kuwa wamepewa uraia ila haki ya kuchaguliwa bado.....watakuwa wakipewa haki hiyo taratibu kwenye vizazi vyao vinavyokuja..ambavyo tunaamini vitakuwa na utamaduni wa nchi yetu moja kwa moja.........

  Mbinu nyingine ya kuwachanganya ni ku encourage intermarriages...

   
 15. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  sisi kilimanjaro hatuna nafasi ya kuweka wakimbizi,wapeleke kwenu huko mpanda
  hata sisi tuna matatizo yetu,
  au warudishe kwao burundi walikozaliwa
  .
   
 16. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2017
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 1,748
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisaa umeleezea vizuli
   
Loading...