Wakimbizi wa Kizungu kwenye ardhi ya Tanganyika

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,027
Leo nilikuwa natazama Aljazeera wakaonyesha documentary ya historia ambapo wakimbizi wa kipoland waliokuwa wanakimbia utawala wa kisoviet baada ya kulazimishwa kuaachs maeneo yao na kufanya kazi kwa kulazimishwa kuhamishwa na kusambazwa katika nchi 6 afrika na serikali ya Mwingereza.

Leo walikuwa wanaangazia wale walioletwa tanganyika kituo chao kilikuwa tengeru, wakiishi kwenye nyumba za udongo na kujichanganya na wakazi wa hapo. Hakukuwa na umeme wala maji ya bomba.

Waingereza walizuia watoto kujichanganya na watoto wa maeneo hayo ili wasije kuiga tabia na culture zao lakini ilishindikana.

Wakazi wa hapo walianza wanawaogopa hao wazungu baadae wakazoeana wakaanza kutembeleana na wanadai walikuwa wanawapenda kwakuwa wakoloni walikuwa na dharau ila hao wakimbizi walikuwa wana watreat kama watu.

Hii historia inasemekana ilikuwa imepotea ila kuna video na document za kumbukumbu juu ya hili. Na hao wakimbizi inadaiwa walikuwa wanakimbia utawala wa Nazi ila kumbe walikuwa wanakimbia utawala wa Kisoviet.

Hao watanzania walikimbilia Iran kabla ya kuletwa tanganyika
 
Vipi walipelekeana moto,bila shaka hapo tengeru kuna mabaki ya vijukuu vya kizungu vichotara
 
Mwisho wa habari yako hujaeleweka ! Hao watanzania walikimbilia Iran kabla hawajaletwa Tanganyika.
Ni watanzania au ni hao wapolish?
 
nliwahi sikia pia maeneo ya Tengeru- Arusha karibu na chuo na mifugo na kilimo kulikuwa na wakimbizi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom