Taarifa toka kwa wadau walioko Ngara ni kuwa kuna wakimbizi zaidi ya 20 wameingia kijiji kilichoko wilayani Ngara mpakani mwa Rwanda na Tanzania. Taarifa zaidi zimedokeza kuwa wakimbizi zaidi wamekuwa wakiingia kupitia kijiji hicho toka rwanda na kuelekea wilaya za Karagwe na maeneo mengine ya Tanzania. Wadau mlioko Ngara fuatilia na mtupe habari zaidi juu ya taarifa hiyo. Tunaomba pia vikosi vyetu vilivyoko mpakani huko ngara wawe makini ili hawa wanaoingia wapekuliwe wasije wakawemo maadui zetu pia.
inasadakika sababu ya kukimbia ni baada ya mkoa mmoja wa Rwanda unaopakana na DRC kushambuliwa na waasi. Baada ya tukio hilo baadhi ya wanaume wanachukuliwa usiku bila kujua wamechukuliwa na mtu gani. Haijulikani kama ni waasi wanaowachukua au jeshi. Watoa taarifa wanaeleza kuwa wakimbizi wengi zaidi wamekimbilia Burundi ingawa pia vijiji kadhaa vya wilaya ya ngara vinavyopakana na Rwanda vimepokea wakimbizi.