Wakimbizi toka Rwanda waingia Wilayani Ngara

parachute

Member
Oct 19, 2012
75
39
Taarifa toka kwa wadau walioko Ngara ni kuwa kuna wakimbizi zaidi ya 20 wameingia kijiji kilichoko wilayani Ngara mpakani mwa Rwanda na Tanzania. Taarifa zaidi zimedokeza kuwa wakimbizi zaidi wamekuwa wakiingia kupitia kijiji hicho toka rwanda na kuelekea wilaya za Karagwe na maeneo mengine ya Tanzania. Wadau mlioko Ngara fuatilia na mtupe habari zaidi juu ya taarifa hiyo. Tunaomba pia vikosi vyetu vilivyoko mpakani huko ngara wawe makini ili hawa wanaoingia wapekuliwe wasije wakawemo maadui zetu pia.


inasadakika sababu ya kukimbia ni baada ya mkoa mmoja wa Rwanda unaopakana na DRC kushambuliwa na waasi. Baada ya tukio hilo baadhi ya wanaume wanachukuliwa usiku bila kujua wamechukuliwa na mtu gani. Haijulikani kama ni waasi wanaowachukua au jeshi. Watoa taarifa wanaeleza kuwa wakimbizi wengi zaidi wamekimbilia Burundi ingawa pia vijiji kadhaa vya wilaya ya ngara vinavyopakana na Rwanda vimepokea wakimbizi.
 
Kuna shida gani tena Rwanda wakuu?
Hawa watu hawatosheki na madhila waliyoyapitia?
 
...."wapekuliwe wasije wakawemo maadui zetu". Maadui wa Tanzania ni nani?
 
Kwanini wanajiita wakimbizi wakati Rwanda sasa hivi hali ni shwari? Au kimenuka tena?
 
Kwanini wanajiita wakimbizi wakati Rwanda sasa hivi hali ni shwari? Au kimenuka tena?

kuna aina nyingi za ukumbizi, nchi inaweza kuwa na amani lakini baadhi ya wanachi wake wakakimbilia nchi jirani endapo wataona/hisi maisha yao yapo katika hatari fulani.
 
Nahisi hawa watakuwa wanatoka maeneo ya Goma (DRC). Rwanda wanapitia tu ...
 
Tanzania tuwe makini sana nawenzetu hawa wa afrika mashariki maana tunaongea amani wenzetu wana geuka hivi Nkunda yuko wapi?tulikia akina bemba mahakaman,maswala haya yakufumbiana ndo matokeo ya wakimbizi
 
Nadhani ni matumizi mabaya ya neno "WAKIMBIZI"! nadhani angetumia neno Wahamiji kutoka Rwanda wasio na vibali ndio wameingia Tanzania vinginevyo atwambie kuna tatizo kubwa linalotishia raia wa Rwanda nchini kwao.
 
kuna aina nyingi za ukumbizi, nchi inaweza kuwa na amani lakini baadhi ya wanachi wake wakakimbilia nchi jirani endapo wataona/hisi maisha yao yapo katika hatari fulani.

Shukrani kwa maelekezo mkuu! Sasa hao walioingia Ngara wanadai kukimbia kitu gani mchini mwao Rwanda? Au kuna mapigano ya kikabila maana wenzetu wale watutsi na wahutu mpaka leo hawapatani kabisa.
 
Nadhani ni matumizi
mabaya ya neno "WAKIMBIZI"! nadhani angetumia neno Wahamiji kutoka
Rwanda wasio na vibali ndio wameingia Tanzania vinginevyo atwambie kuna
tatizo kubwa linalotishia raia wa Rwanda nchini kwao.



we kweli ni GT??? soma kwanza uzi?? je wakimbizi nini maana yake???? wewe ndie hujui maana sahihi?
 
Kagame can fool some countries for sometimes but not the whole world for ever. Soon Kagame ataumbuka na ujanja wake unaweza kuishia The Hague. Time will accurately tell.
 
Chizi haponi jamani labda kime nuka tena, mkuu endelea kutujuza
 
we kweli ni GT??? soma kwanza uzi?? je wakimbizi nini maana yake???? wewe ndie hujui maana sahihi?

Kuna vipimo vingi vya U'GT' sijui umetumia kipimo gani hicho kinachokupa mashaka?

Rejea maelezo haya hapa chini:

1.Post ya kwanza ya Uzi huu imewekwa javini saa 17.01 hours

2. Nimeijibu post hiyo saa 18.33 hours

3.Mwanzisha mada kaifanyia editing post ya kwanza (labda baada ya kusoma post yangu) saa 19.40 hours.

Ukifuatilia matukio hayo matatu hapo juu na muda yalipotokea, utagundua kuwa huna budi kupitia upya vipimo vyako vya U'GT' na ikidi uende kwa wataalamu wa kupima U'GT' wapime U'GT' wako pia.
 
hao ni wahaamiaj na uwa wanaingia kila siku ni kawaida sababu ardhi rwanda ni kidogo na wanakuwa na mifugo hivo wanakuja na pesa,wanauziwa ardhi na viongoz wa kijiji,pia wengine wanaona maisha ni magumu kule lakin wanaona fursa ambazo zipo kagera hivyo wanaamia kabisa kutafuta maisha ni kama unavyoona wahaamiaj toka eritrea,somalia,ethiopia,congo,rwanda na burundi walivyorundikana kampala,hiyo yote kutafuta maisha tu,waacheni
 
Mlioko Ngara msisite kuwakaribisha wabantu wenzetu wanashida jamani.

Nani anaependa kukimbia kwao bila sababu za msingi jamani?

Vita haina macho jamani hawa wanaokimbia wanajua kwasababu walishang'atwa na nyoka sasa hata unyasi ukiwagusa .....
 
Habari za kuaminika ni kuwa wakimbizi zaidi ni wanawake na vijana ambao wamekimbia makazi yao nchini Rwanda kufuatia WAUME zao kuchukuliwa au kuvamiwa na wanajeshi usiku wa manane kwa nguvu na kupelekwa kusiko julikana japokuwa wao wamesema kuwa wanapelekwa DRC kwenda kuongeza nguvu ktk kikundi cha M23 hizo ni taarifa zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na wahusika wenyewe ndo wameweza kutoa hizo taarifa. Na hofu kubwa kwao ikawa kuwa endapo wataweza kurudi nyumbani basi maisha yao yapo hatarini maana hili suala tayari ni kama udhalilishaji wa nchi kitaifa na kimataifa. Maana itakuwa inaonyesha kuwa rwanda inahusika moja kwa moja kuisaidia M23 kitu ambacho Rwanda inakipinga kwa nguvu zoote UKWELI NDO HUO:israel:
 
Back
Top Bottom