Wakimbizi mkoani katavi hawatapewa vitambulisho vya uraia, hiyo ni kwa mujibu wa rais wa wanyonge jpm

buhoro ksl

Senior Member
Apr 17, 2019
175
250
Miongoni mwa sababu alizotoa ni kushamiri kwa vitendo vya kihalifu, vikihusisha ukabaji na wizi wa siraha.

Sababu nyingine ni kutokana na wakimbizi hao kuwaleta na wenzao ambao hawakupewa uraia Hapo awali .Kwa mtazamo Wangu rais amefanya Jambo jema Sana kwani Hawa ndugu zetu wamekuwa siyo watu wasuri, japo unaweza kuwakaribisha kwa mikono yote, lakini bado watakuumiza tu, mfano angalia mikoa wanaoishi Hawa ndugu zetu kigoma,tabora na katavi Hali ni tete.
Mimi nimebahatika kuishi mikoa hiyo, unakuta mrundi bado anamashamba kwao Burundi halafu na huku kwetu ana mashamba, sasa unafikiria serikali
yetu inatumia vigezo gani kuwapa wakimbizi uraia?
Kwakweli ni jambo ambalo huwezi kukubaliana nalo.

Ndukiiii!🏃🏃🏃🏃
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,370
2,000
Kuna wakati kikwete aliwapa uraia zaidi ya 100 hivi nadhani alikosea
 

LOVE U JF

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
2,099
2,000
Waliopewa uraia ni wabantu wenzetu leo kama tunajivunia kuzisaidia nchi za kusini mwa afrika kujikomboa kuna tatizo gani kuwatambua watu ambao tuko nao toka miaka ya 1970 ?
Kwa swala la uharifu ni jamii gani ipo salama au magereza za huko wanafungwa wao tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom