Wakili wa Mnyika azidi kuchachamaa; Mlalamikaji Hawa Ng'umbi hastahili Msamaha wa kulipa sh 15M | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakili wa Mnyika azidi kuchachamaa; Mlalamikaji Hawa Ng'umbi hastahili Msamaha wa kulipa sh 15M

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Apr 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145  Na Esther Mbussi
  [​IMG]

  WAKILI Edson Mbogoro anayemtetea Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Hawa Ng’umbi, amesema mlalamikaji huyo hastahili kupewa msamaha wa kulipa Sh milioni 15 kama dhamana ya kesi aliyoifungua.

  Shauri hilo lilikuja Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza ombi dogo la Ng’umbi la kutaka Mahakama imsamehe kulipa Sh milioni 15, kwa ajili ya washitakiwa watatu aliowashitaki ikiwa ni Sh milioni tano kwa kila mmoja.

  Katika kesi hiyo, washitakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mnyika na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo.

  Akikazia sababu kwa nini mlalamikaji asisamehewe kulipa kiasi hicho cha fedha, Wakili Mbogoro alidai Ng’umbi alitakiwa aieleze Mahakama anataka apunguziwe kiasi gani cha fedha na kwa nini apunguziwe kiasi hicho.

  Naye Wakili wa Ng’umbi, Issa Maige, aliiomba Mahakama imsamehe mteja wake fedha hizo kwa kuwa sheria ya uchaguzi haikuweka kigezo cha uwezo wa fedha na kwamba ni cha kufikiriwa.

  Jaji Upendo Msuya aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, alisema atalitolea uamuzi ombi hilo Aprili 18, mwaka huu.

  Ng’umbi aliiomba Mahakama hiyo impatie msamaha wa kutolipa Sh milioni 15 kama dhamana ya kesi aliyoifungua kwa sababu hana uwezo wa kulipa kiasi hicho.

  Ng’umbi alifungua kesi hiyo Namba 107/2010 Machi 22, mwaka huu, akitaka mahakama itengue matokeo ya ushindi wa Mnyika.
   
 2. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Alienacho huongezewa asiyenacho hunyang'anywa hata kile alichonacho. Yametimia
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu mama ovyo kabisa...yaani mbwembwe zote zile wakati wa kampeni anakosa 15m?
   
Loading...