Elections 2010 Wakili wa mdai wa Dr. Slaa ni mgombea udiwani wa CCM!

Je wajua kwamba wakili A.Kitururu anaye mtetea Mporwa mke wa Dr Slaa ni mgombea udiwani wa CCM kata ya ubungo.Je CCM mnataka wananchi wajifunze nini?.
.

Je wajua kwamba wakili Mabere Marando aliyetetea chadema kesi ya pingamizi dhidi ya kikwete ni kada wa chadema. Je chadema mnataka wananchi wajifunze nini?
 
La muhimu kama walioana kisheria je waliachana kisheria ??? Je taratibu za kukimbia na sababu aliziripoti ,kuna hati zinazoonyesha kulikuwa na matatizo kati yake na mumewe ,aliwahi kuyaripoti iliamuliwaje huko alikoripoti ?? Hakuna hata moja kati ya hilo ,mke na aliemchukua mke wote watakuwa wamefanya au wamemfanyia uhuni huyo masikini wa Mungu , ila sasa kama jamaa ameamua kuamka na baada ya kumjua mbaya wake ,kila kitu kitakuwa shwari hapo sheria zitakapochukua mkondo wake ,ninachowaomba msiwe mnamtetea Slaa tu bali muwe mnatoa maauzi yenye kutoa haki kwa wote wawili au watatu ,kisheria ,bila ya upendeleo ,yaani hapa hapa JF tunaweza kujua ni nani mwenye makosa ambae hukumu itabidi itwalishwe juu yake ,hapa hapa JF ,tuache tabia ya CCM kulindana kwa kuwa tu ni mwenzetu na kumnyonga mnyonge asiestahili :mad2:

demu kamuacha jamaa basi.... huyo mtu alikua wapi tangu all those monthss? hivi ningemchukua mimi josephine, mahimbo angeenda kidai bilioni?

hivi mke wa lipumba hakuwahi kuolewa kweli?
 
Du! ndo mana hakuwa na comfo bwana, inaelekea kalazimishwa na "mampira" hakuwa tayari kabisa!
.

Inaelekea na Mabere Marando alilazimishwa kumfungulia kesi ya pingamizi kikwete hakuwa tayari kabisa na Marando
 
Hivi huyu bwana ameporwaje mke wake? Mimi bado hii kitu haijaingia akilini!
.

Jibu la kweli analo Dk Slaa mwenyewe. Hata kama CCM wanampakazia lakini ana wajibu wa kuijulisha jamii kwamba hakupora mke wa mtu au la. Hii ndio njia pekee ya kujisafisha kwa wananchi.
 
Another great mistake kwenye anga za sheria hii itachukuliwa ni kesi ya kisiasa zaidi.
Rejea sheria ya ndoa, hii sio kesi ya kisiasa. Na kama Dk Slaa anafanya mchezo badala ya kujibu hoja itamfikisha pabaya na hata kumchafua zaidi. Huwezi kuwa na kesi ya ndoa ya kujibu mahakamani ukamwambia hakimu ni CCM wamenipakazia. Hii inawezekana tu hapa JF lakini sio mahakamani.
 
Afadhali umeuliza mkuu maana hata mimi ninavyojua mke wako siyo mali yako ni mwenza wako na ni binadamu aliyevuka umri wa miaka 18 hivyo ana uwezo wa kufanya maamuzi yake. Sasa ukisema kitu kuporwa ni kwamba kinachukuliwa kwa nguvu na kitu kinachoporwa hakina utashi wa kujua kinaporwa. Tukija kwa upande wa binadamu labda mtoto mchanga anaweza kuporwa lakini si mtu mzima mwenye akili zake timamu, unless anatekwa. Tamko kama hizi ni udhalilishaji wa wanawake na pia ni kudanganya umma kwani ni kitu ambacho hakiwezekani.
.

Kwa mujibu wa sheria, Ndoa iliyounganishwa kisheria ni lazima ivunjike kisheria. Kama Dk. Slaa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye ndoa yake haijavunjika kisheria ana kesi ya kujibu mbele ya mahakama. Jamani tuache ushabiki ambao hautaki kuzingatia sheria inasemaje? wote tunampenda Slaa lakini ili kumsaidia ni lazima tuseme ukweli.
 
Dr Slaa hana kesi ya kujibu hapo hasa yule mwanamke akikubali kuwa alimuambia Dr Slaa sijaolewa, kwani ili kujua kuwa fulani kaolewa au hakuolewa ni ngumu mpkaka aidha upate cheti chake au mwenyewe akueleze, na kwa kuwa mapenzi sio kitu cah kulazimishana na hawa wote ni watu wazima basi Dr Slaa hajambaka huyu dada, kosa ni la huyu dada kwa tamaa zake au kushindwa ndoa yake na Mahimbo ndio akaenda kwa Slaa, Mi naona Dr Slaa hana kesi ya kujibu ila kwa kuwa hii ni siasa basi ndio maana imepelekwa mahakamani.Ngoja tuone kwani Mawakili wakubwa kama Marando na Lissu wapo na huyu Kitururu ni junior sana kwenye tasnia ya sheria, kazi anayo na kama kaichukua hio kesi ili apate udiwani basi atakosa kila kitu.
 
kaaaazi kwelikweli, kaporwa mke , ndo kajua sasa au keshapewa mshiko? si hasa za bongo bwana. nshachoka, natamani utawala wa kidikteta japo miezi sita watu wachapwe viboko ndo tutanyooka
.

Sidhani kwamba mume halisi wa Josephine kajua sasa,i anaweza kuwa amechukizwa na kitendo cha mke wake kujitangaza hadharani kwamba ni mke wa Dk. Slaa kabla hawajamalizana kisheria. Lakini pia inawezekana hapo mwanzo alikuwa anasikia tetesi tu kuwa Dk . Slaa anatembea na mke wake bila ushahidi lakini tangazo la Dk Slaa pale Jangwani linatosha kupata ushahidi wa kufungua kesi mahakamani
 
Inavyoelekea Josephine hamtaki tena huyo jamaa.
.

Ni kweli inaelekea Josephine hamtaki tena huyo jamaa lakini hawezi kujitoa kwamba sio mume wake kisheria. Kama hamtaki alipaswa kufuata sheria. Hali hii ni kama ya kukomoana kati ya mume na mke. Josephine kaporwa na Dk. Slaa bila utaratibu wa kisheria ni haki ya mume kujibu mapigo. Kama hamtaki mume halisi na anazo sababu za kuimbia mahakama ni kitu gani kilisababisha kuanza mapenzi nje ya ndoa? Ni kwa nini Dk.hakuliona hili?
 
Kwa mujibu wa sheria, Rose Kamili ni mke wa ndoa wa Dk. Slaa, ni busara zake tu yule mama hajafungua mashitaka. Dk. Slaa anasema hakufunga ndoa na yule mama lakini sheria inasema watu wa jinsia tofauti (mwanamke na mwanaume) wakiishi pamoja kama mke na mume kwa miezi 6 automatically sheria ya ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawatambua watu hao kuwa ni mume na mke. Kitendo cha Dk Slaa kusema hakufunga ndoa na Rose Kamili ni habari za mtaani na sio za kisheria. Nina mashaka hapo baadaye Kamili anaweza kufungua kesi dhidi ya Josephine na Dk. Slaa. Kamili anaonekana amesita kufungua mashitaka dhidi ya Dk Slaa kwa sababu za kisiasa, akipita ubunge Hanang hatafungua mashitaka na akishindwa anaweza kufungua kwani kwa sasa anaweza kuwa anacheza kete ya kisiasa kwa kutompinga mgombea wa urais wa chama chake cha chadema.
 
Fanyeni kila mnaloweza ,najua mnaweka dharau sana na kutudharau wengine kuwa hatujui kitu na nyie waChadema ndio mnaojua na kujifanya ni watu wa mahakama ,ila mkae na kukumbuka msije mkalaumu kuwa hamkupewa tahadhari ,wakati hakimu atakapogonga meza ,Mkuu hapa amenasa na zaidi kesi hii ya uzinzi kwa kiongozi mkuu wa Chama na pia mgombea uraisi. Sijui niseme huku ni kuchamba kwingi kwa Slaa au ni kuhadaika na giza akanya njiani ?

Hivi Slaa alipomnadi yule mwanamke alikuwa anauonyesha nini umma wa WaTanzania ,kama CCM inaatufanya WaTz wajinga ,Slaa anatufanya mambutwai au , ipendeni Chadema kiroho lakini msiziruhusu tabia za akina Slaa kuwatawala akili zenu ,lazima kuwe na mipaka.
 
Hivi hata hawala nae ni mke wa ndoa?
Nina ulakini na hivyo vyeti vya huyo Mahimbo ikibainika kagushi tunakula nae sambamba hata kwenye picha hiyo alowakilisha hazifanani na huyo wife to be wa Dr.
 
Fanyeni kila mnaloweza ,najua mnaweka dharau sana na kutudharau wengine kuwa hatujui kitu na nyie waChadema ndio mnaojua na kujifanya ni watu wa mahakama ,ila mkae na kukumbuka msije mkalaumu kuwa hamkupewa tahadhari ,wakati hakimu atakapogonga meza ,Mkuu hapa amenasa na zaidi kesi hii ya uzinzi kwa kiongozi mkuu wa Chama na pia mgombea uraisi. Sijui niseme huku ni kuchamba kwingi kwa Slaa au ni kuhadaika na giza akanya njiani ?

Hivi Slaa alipomnadi yule mwanamke alikuwa anauonyesha nini umma wa WaTanzania ,kama CCM inaatufanya WaTz wajinga ,Slaa anatufanya mambutwai au , ipendeni Chadema kiroho lakini msiziruhusu tabia za akina Slaa kuwatawala akili zenu ,lazima kuwe na mipaka.
lalalalal! Ipendeni CCM kiroho lakini msiruhusu tabia za akina JK (kupita na waandishi wa habari, wasanii wa kike kisha kuwazawadia ukuu wa wilaya na ajira BOT) kutawala akili zenu, lazima kuwe na mipaka!
 
.

Je wajua kwamba wakili Mabere Marando aliyetetea chadema kesi ya pingamizi dhidi ya kikwete ni kada wa chadema. Je chadema mnataka wananchi wajifunze nini?

Najua. CHADEMA inataka watanzania wajifunze kuwa kesi ya pingamizi kwa Kikwete na Kesi ys kukimbiwa na mke, zote ni kesi za kisiasa
 
Kwa mujibu wa sheria, Rose Kamili ni mke wa ndoa wa Dk. Slaa, ni busara zake tu yule mama hajafungua mashitaka. Dk. Slaa anasema hakufunga ndoa na yule mama lakini sheria inasema watu wa jinsia tofauti (mwanamke na mwanaume) wakiishi pamoja kama mke na mume kwa miezi 6 automatically sheria ya ndoa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawatambua watu hao kuwa ni mume na mke. Kitendo cha Dk Slaa kusema hakufunga ndoa na Rose Kamili ni habari za mtaani na sio za kisheria. Nina mashaka hapo baadaye Kamili anaweza kufungua kesi dhidi ya Josephine na Dk. Slaa. Kamili anaonekana amesita kufungua mashitaka dhidi ya Dk Slaa kwa sababu za kisiasa, akipita ubunge Hanang hatafungua mashitaka na akishindwa anaweza kufungua kwani kwa sasa anaweza kuwa anacheza kete ya kisiasa kwa kutompinga mgombea wa urais wa chama chake cha chadema.

Sheria itawatambuaje kuwa mume na mke bila uthibitisho wa marriage certificate? hiyo sheria inahitaji kwenda mbele zaidi..
 
.

Kwa mujibu wa sheria, Ndoa iliyounganishwa kisheria ni lazima ivunjike kisheria. Kama Dk. Slaa alianzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanamke ambaye ndoa yake haijavunjika kisheria ana kesi ya kujibu mbele ya mahakama. Jamani tuache ushabiki ambao hautaki kuzingatia sheria inasemaje? wote tunampenda Slaa lakini ili kumsaidia ni lazima tuseme ukweli.
siyo wote humu ni maamuma wa sheria mkuu.
tema kipengele kinachosema hivyo ili ujibiwe kwa kipengele
gadem
 
Sijajua vizuri kinachoendelea ni kitu gani! Lakini uzoefu unaonesha CCM inaweza kuwa imeanzisha au inachochea kuwepo kwa kesi hii (Niko tayari kukosolewa). Lakini dhana yangu hii haiondoi wazo kuu kuwa Dr. Slaa yuko katika tuhuma. Kwa nchi za wenzetu mazingira ya kisiasa yangetumika kumwokoa Dr. Slaa mahakamani kama ilivyokuwa kwa Jacob Zuma. Hata hivyo ninachokiona hapa ni kuwa nchi kama yetu (zetu) inatatizwa na uhaba wa elimu ya uraia na elimu ya jumla kiasi kwamba ni rahisi kwa chama au kundi la watu kuhamisha (divert) mawazo ya msingi ya wananchi kwa mambo yasiyokuwa na uzito ukilinganisha na mada husika iliyo mezani. Nitatoa mifano. Nakumbuka ushindi wa Taifa Stars dhidi ya Burkina Faso ulisababisha watu fulani waseme umewasaidia kupunguza machungu ya Bajeti wakati huo waziri wa fedha akiwa Zakhia Meghji. Nakumbuka Kikwete aliwahi kulalamika katika kikao cha CCM Znbr kuwa kuna watu walikuwa wanampakazia asingeishi muda mrefu kama angekuwa Rais kutokana na ubovu wa afya yake, inakisiwa uzushi huu ulimchafua kwa wananchi kuwa ni "kiwembe" kwa mademu. Hadi leo naona kuna harufu ya madai hayo ikichangiwa na matukio ya Kikwete (Sasa ni Rais) kuanguka mara kwa mara. Nakumbuka Salim Ahmed Salim alizushiwa kuwa HIZBU, kuwa Mwarabu, kumuua Mzee Abeid Karume na kuwa nje ya nchi muda mrefu. Sasa ni Dr. Slaa.

SAMAHANI KWA POSTI NDEFU (NI POST YANGU YA KWANZA BY THE WAY)

Sijakaa duniani muda mrefu (umri wangu ni chini ya miaka 40) lakini nimebahatika kuiona angalu Tanzania changa na mabadiliko yake, nimepata kumwona laivu Rais wa kwanza wa hii nchi (si kitu kidogo hiki). Nachotaka kusema ni kuwa mabadiliko katika Tanzania yaja, haijalishi atakayekuwepo (si atakayeyaleta) ni Dr. Slaa au la. Awe Tundu Lissu, awe Mrema Lyatonga, awe Kikwete, awe Dr. Slaa, awe Profesa Baregu, awe Anne Kilango, maadiliko yaja japo taratibu lakini ni kwa kasi kubwa kwa wanaopenda kutazama vizuri, kufuatilia historia na saikolojia za binadamu. Ishara mojawapo ni kitendo cha watu kuweza kumyumbisha Rais hadi akalazimika kuwa na vikao na kamati teule nyingi ni ishara ya woga kupungua japo inaweza kuwa ni dalili ya udhaifu wa Rais, kitendo cha watu kuzomea wagombea hasa wa chama tawala (Sisemi CCM, nasema chama tawala) ni ishara nyingine ya mwamko. Kitendo cha CCM kuvurugana sana wakati wa uchaguzi wa ndani mbele wa wananchi wote (hasa wa vyama vya ushindani/upinzani) ni dalili ya CCM au aina fulani ya CCM kuwa inafikia tamati. Mabadiliko yaja.

Tusubiri kidogo.
 
Kweli wakuu mnisamehe bure tu mi kwa elimu yangu ndogo tena ya standard 7 sijafanikiwa kuona kosa na mkosaji apo kwenye hiyo kesi.halafu nauliza.ivi mke aliondoka au alimtoroka?na alikwambia anakwenda wapi?watoto nao?then ikawaje au ukachukua uamuzi gani?je uliripoti japo kwa mshenga wako?wachungaji je?mi naona kuna haja ya huyu jamaa kufunguliwa kesi ya udhalilishaji dhidi yetu sisi wanaume vinginevyo ni sacatric.waheshimiwa jf naomba kuwasilisha hoja.
 
Si ndio nyinyi Wakristo munaosema ndoa hazivunjwi? Leo tena mambo yamekuwa vipi? Au mkuki kwa nguruwe lakini kwa binaadamu huwa mchungu?

Mimi nauliza tu jamani!!!!!!!!!!!!!

Ndio wakristo hasa wakatoliki wanasema ndoa ni pingu za maisha lakini hii aina maana kwamba ndoa haiwezi kuvunjwa. Katika Kanisa Katoliki kuna mahakama ya ndoa na ndoa inaweza kuvunjwa kama kuna sababu za msingi na kanisa kuridhia. Hata hivyo ndoa sio utumwa. Hata kama umefunga ndoa kanisani unaweza kwenda mahakamani na ndoa ikavunjika na katika sheria za nchi hii ni halali kabisa ila tatizo litabaki kwenye dini kwenye vitu kama kuzuiwa kupokea baadhi ya maskramenti. Ndio maana mme wa huyu mama wa "Dr. Slaa" akwenda KKT alikofunga ndoa kulalamika. Kakimbilia mahakamani. Lakini wote tunajua kwamba hizi ni politics at play. Hakuna Kitu!! 1995 walimwandama Mrema na 2005 walimwandama Lipumba, safari hii ni zamu ya Dr. Slaa. Nadhani mwalimu Nyerere anageuka kaburini alikolala!!
 
Back
Top Bottom