Wakili wa Babu Seya: Rais Magufuli amenisurprise sana

Bavicha shida sana, hamueleweki. Aliposema yule fisadi wenu mlishangilia, Magu ametenda unakebehi eti frustration.
Alisema mwenyewe akiwa na frustration anafanya mambo bila kujijua,sasa mwenyekiti wenu mnamshangilia kama mazuzu akiwa frustrated nanyi mtakuwa insane hamjitambui
 
Una uhakika gani kama walibaka?

Justification ya Rais aneseme kama wamekubari kosa na hawakuua albino kwanini wasisamehewe?. Ingawa ilikua ni kwa wale waliokatika kesi ya mauuaji ila inawezekana taswira hii pia ilitumika ktk upande huu, maana hakukua na maelezo ya yaliyotolewa kuhusiana na hawa.
 
Wakili Mabere Marando aliyekuwa akimtetea mwanamuziki mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, amesema uamuzi wa Rais John Magufuli kuwasamehe umekuwa ni ‘surprise’ (jambo la kushtukiza) kwake.

Babu Seya na Papii Kocha ambaye pia ni maarufu kama Mtoto wa Mfalme walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuwabaka na kuwalawiti watoto 10 wa kike ambao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.

Tayari walishatumikia kifungo hicho kwa miaka 13 na miezi minne.
Wakili Marando ambaye aliwatetea katika rufaa yao ya pili Mahakama ya Rufani alisema uamuzi wa Rais Magufuli umemshangaza na ameupokea kwa furaha kubwa.

Marando ambaye alifanikiwa kuwatoa kifungoni watoto wawili wa Babu Seya, Mbangu na Francis katika rufaa hiyo alisema hakutarajia uamuzi kama huo.

“Asante sana, asante sana, asante sana, namshukru sana Rais Magufuli kuwasamehe, kwa kweli sikutarajia hili. Hii imekuwa ni surpirise, asante sana,” alisema Wakili Marando ambaye alikuwa hajapata taarifa za uamuzi huo hadi alipoulizwa na mwandishi wetu.

View attachment 647675
Acha uboya wewe MTU ametumikia TiSS alafu eti useme kuwa hakupata taarifa as if Rais aliyangazia chumbani msahama. Mabere ni jasusi mmbobezi na ajanua vema kuchambua taarifa.

Next time acha ubazazi
 
Wale wauaji nao pia wamesamehewa kwa kuwa hawakuua Albino, kwani Albino na asie Albino wana tofauti gani?
 
Una uhakika gani kama walibaka?
Hivi mahakamani kuu na Rufaa kote walishinikizwa kufanya maamuzi? Labda Wakili wao Marando atakuja kusimulia Siku moja kama maadili ya uwakili yanaruhusu. Ukweli unatakiwa ujulikane ili watz waelewe kuwa Kuna Watu wabaya wanaoweza kutumia madaraka yao vibaya kiasi Cha kukufufunga mtu miaka yote hiyo pasipokuwa na jinai.
Ni vigumu kuamini na pia kama walitenda kosa kweli, tena jinai ya kulawiti watoto wetu wa shule ya msingi basi kuwasamehe ni sawa ila isiwe kwa masilahi ya kisiasa bali kwa kuwa jamii imejiridhisha kuwa wamejutia kosa lao na wamemrudia Mungu. Lakini kwa jinsi watu walivyoshangilia yaweza kuwa maamuzi yametolewa kwa public pressure na masilahi ya kisiasa.
You're kwa yote Kuna Jambo nyuma ya hili na ni vizuri likawekwa bayana kwa umma wa Watanzania.
Naona kutoa hoja wajuvi wadadavue.
 
Back
Top Bottom