Wakili wa Babu Seya: Rais Magufuli amenisurprise sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,300
2,000
Wakili Mabere Marando aliyekuwa akimtetea mwanamuziki mkongwe nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, amesema uamuzi wa Rais John Magufuli kuwasamehe umekuwa ni ‘surprise’ (jambo la kushtukiza) kwake.

Babu Seya na Papii Kocha ambaye pia ni maarufu kama Mtoto wa Mfalme walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuwabaka na kuwalawiti watoto 10 wa kike ambao walikuwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.

Tayari walishatumikia kifungo hicho kwa miaka 13 na miezi minne.
Wakili Marando ambaye aliwatetea katika rufaa yao ya pili Mahakama ya Rufani alisema uamuzi wa Rais Magufuli umemshangaza na ameupokea kwa furaha kubwa.

Marando ambaye alifanikiwa kuwatoa kifungoni watoto wawili wa Babu Seya, Mbangu na Francis katika rufaa hiyo alisema hakutarajia uamuzi kama huo.

“Asante sana, asante sana, asante sana, namshukru sana Rais Magufuli kuwasamehe, kwa kweli sikutarajia hili. Hii imekuwa ni surpirise, asante sana,” alisema Wakili Marando ambaye alikuwa hajapata taarifa za uamuzi huo hadi alipoulizwa na mwandishi wetu.

PIC%2BMABERE.jpg
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,459
2,000
Unakataa magufuli hana frastruatioan?
Hana. Ukiwa na frustrations, some of your body parts will defy orders from the central system. Hata misuli ya kuzuia usiharishe hadharani itakaidi amri kutoka juu. It happened, to the embarrassment of many, at chato stand in 2015.
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,280
2,000
Hana. Ukiwa na frustrations, some of your body parts will defy orders from the central system. Hata misuli ya kuzuia usiharishe hadharani itakaidi amri kutoka juu. It happened, to the embarrassment of many, at chato stand in 2015.

Kwa hiyo pele bandalin alikuwa anaudanganya umma? Au misulu yakule kuhalisha haikuzilika?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom