Wakili Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ili arejee nchini. Lakini, nani hasa amhakikishie usalama wake ili arejee nchini?

Soma hii:

Kwanini Lissu amezungumzia suala la usalama jana ikiwa IGP alishalitolea ufafanuzi?
 
Hua unahangaika sana na Lissu mkuu,sijui tatizo nini?
Damu Nzito Kuliko Maji.
Huoni Hata Jiwe Anavyoteseka, Hana Amani Kabisa Moyoni.
Kila Akifanya Ziara Ni Kutukanana Na Wananchi Tu Mikutanoni, Very Frustrated !
 
Raia no 1 ndio wa kuhakikisha usalama.Sasa na yeye kachuna kuwatafuta hao wahalifu wasiojulikana!
 
Kwa maoni yangu ni bora akae huko huko.ila ninacho kuwa na wasi wasi kwa wale waliomdhamini katika kesi inayomkabili Lissu watakuwa katika wakati mgumu sana.
 
Mawakili wote ni Wasomi. Kila Wakili ni Wakili Msomi
Sasa nini mantiki ya kuongezea neno msomi kwenye jina wakili? Kwahiyo taaluma zingine watu hawasomi? Yaani najiuliza tu eti tusikie 'daktari msomi fulani bin fulani, mhandisi msomi fulani binti fulani'. Mbona vituko!
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
I conquered with your argument. Lakini TL yeye amesema chama kmhakkishie usalama na si serikali. Lisu anajua uhai wake upo ndani ya Chama. Kwa tafsiri ya kawaida ya kusema chama kimhakikishie usalama basi Lisu huenda anamashaka na chama chake. Inawezekana kuna mazingira ambayo Lisu anayaunganisha tukio na chama. Asingekuwa anatilia shaka chama basi angeema serikali imhakikishie usalama.
 
..inawezekana pia anakiamini chama chake kuliko serikali.

..serikali ndiyo yenye vyombo vya kumhakikishia usalama, sasa kwanini TL hawasiliani na serikali badala yake anawasiliana na chama chake kuhusu usalama?
 
Katiba ya nchi inasema ulinzi wa Taifa ni wa raia yeyote, lakini ulinzi wa Raia na mali zake ni jeshi la polisi. Jeshi la polisi ni serikali, chaka hakijatajwa kama kinaweza kumhakikishia mtu ulinzi. Alichofanya Lisu kwa mtazamo wangu ni kuwa anamashaka na chama ndiyo maana anasema wamhakikishie ulizi.

Lakini haya ni mawazo yangu kutokana na doubt inayoonekana kwenye clip ya Lisu.
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
Lissu asitubabaishe. Yeye ni Mtanzania kama wengine. Yeye ana bahati alishambuliwa na akapona. Kuna wengine walifariki. Lakini hiyo haiondoi jukumu la serikali la kumlinda kila raia kwa usawa. Jinsi Lissu atavyohakikishiwa usalama wake ni sawa sawa na mimi tu ninavyohakikishiwa usalama wangu. Asilete exaggerations hapa!
 
Katiba ya nchi inasema ulinzi wa Taifa ni wa raia yeyote, lakini ulinzi wa Raia na mali zake ni jeshi la polisi. Jeshi la polisi ni serikali, chaka hakijatajwa kama kinaweza kumhakikishia mtu ulinzi. Alichofanya Lisu kwa mtazamo wangu ni kuwa anamashaka na chama ndiyo maana anasema wamhakikishie ulizi.

Lakini haya ni mawazo yangu kutokana na doubt inayoonekana kwenye clip ya Lisu.

..atahakikishiwa vipi ulinzi na watu asiowaamini?

..au atapanga vipi mipango ya ulinzi na watu asiowaamini?

..akisema serikali au polisi wamhakikishie ulinzi wako watakaohoji kuwa atalindwa vipi na vyombo anavyovituhumu kumshambulia.

..hivi leo hii Tundu Lissu akisema anasubiri kampuni ya ulinzi ya Ultimate Security wamhakikishie usalama wake utasema hana imani au anaihisi vibaya kampuni hiyo? Au utasema anaamini kampuni hiyo itaweza kumlinda?
 
Hua unahangaika sana na Lissu mkuu,sijui tatizo nini?

Wewe ndo tukuulize tatizo lako ni nini. Na je hoja yake ina Shida. Au ungependa hoja iwe labda Kuhusu kilimo na please JOM leta mbolea. Katika kila sekunde 30 anaandikwa JPm. Mbona huji na kulalamika? Grow up acha mahaba binafsi ya kupitiliza. Hapa watu wana maisha yao. Hawalipwi na hao unaowafikiria wewe.
 
Hoja yako itakuwa na nguvu tukimpata dereva wake, ambaye hadi Leo hatujui yupo wapi!
Lisu aongei tena kuhusu dereva,wala chama chake,na wewe hujagusia!
Inawezekana kushambuliwa kwa Lisu ikawa in "mchezo" vijana wanasema move, inawezekana mission ilifeli, that's why hataki kurudi, au dereva wake (kama yupo hai)
Hayo makandokando yakipata majibu, basis issue ya Lisu ni ndogo sana
Chama ndio ambacho kinaweka pale Area D ulinzi na pia ni karibu na nyumba ya naibu speaker ambayo uwa inalindwa na askari polisi ila siku ya tukio hawakuwepo
 
Back
Top Bottom