Wakili Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ili arejee nchini. Lakini, nani hasa amhakikishie usalama wake ili arejee nchini?

Mkuu, kama serikali haina wajibu wa kumuhakikishia kila raia usalama inakuwaje kuna watu wana bodyguards....!!

Sema kwa Lissu issue iko completed kwa vile kwa maoni yake mtuhumiwa ni serikali.
Sasa Lisu na yeye awekewe bodyguards?
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
Hoja yako itakuwa na nguvu tukimpata dereva wake, ambaye hadi Leo hatujui yupo wapi!
Lisu aongei tena kuhusu dereva,wala chama chake,na wewe hujagusia!
Inawezekana kushambuliwa kwa Lisu ikawa in "mchezo" vijana wanasema move, inawezekana mission ilifeli, that's why hataki kurudi, au dereva wake (kama yupo hai)
Hayo makandokando yakipata majibu, basis issue ya Lisu ni ndogo sana
 
Jiwe ana ulinzi wa hatari na hakuna hata tetesi za kutaka kumdhuru, Halafu Lissu aliyeshambuliwa kwa Zaidi ya risasi 30 arudi kichwa kichwa..

Kwenye ziara yake Walioambiwa wamlipe yule Mama million 15 fidia ya ng'ombe wakapewa na maagizo alindwe asidhurike. Ila kwa Lissu hata kutoa pole ikamshinda
 
Mwenye wajibu wa kulinda raia wake na mali zao ni serikali. Ukitishiwa maisha unamshitaki aliyekutishia, na unaweza kuiomba serikali ulinzi kulingana na aina ya tishio na mtishaji.

Kwa case ya Lisu, ukiacha tofauti za kisiasa, ni serikali yenye jukumu la kumuhakikishia ulinzi wake muda wote, kwasababu hata wao hawafahamu ni nani aliyemdhuru na haijawakamata, hivyo wanawajibika kumlinda mpaka watambue ni nani alitenda kosa hilo na kwanini, na iwachukulie hatua, kisha ijiridhishe hakuna tishio tena la usalama wa maisha yake na familia yake, kisha wanaweza kumuacha kumlinda binafsi na akalindwa kama wengine tunavyolindwa na vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi.

Ni aina gani ya ulinzi ni serikali inatakiwa ifanye tathmini kulingana na tukio la awali, na uchunguzi walioufanya, au watakaoufanya kubaini ni nani aliye nyuma ya hilo.

Serikali haipaswi kususa eti kwasababu imeshutumiwa, inapaswa iongeze mbinu ili kuhakikisha yaliyotokea hayajirudii siyo kwa Lisu tu, hii ni kwa kila raia wa Tanzania, ulinzi wa raia na mali zao ni jukumu la serikali zote duniani.
 
Petro E. Mselewa,

Uzi wako kuhusu "rais anakosea wapi kila jambo anakosolewa". Hapo ndipo usomi wako, na chuo chako ulichosoma tunavitazama kwa mlengo wa tatu (the eagle eye)
Tatizo unaandika kila linalokujia kichwani pasipo kuchuja matokeo yake.
 
Waliomshambulia hawajulikani, aheri akae huko nje wasije wakamdhuru tena. Ingekuwa wamekamatwa angalau angejipa moyo kuwa wabaya wake hawatamdhuru.
 
Petro E. Mselewa,

Uzi wako kuhusu "rais anakosea wapi kila jambo anakosolewa". Hapo ndipo usomi wako, na chuo chako ulichosoma tunavitazama kwa mlengo wa tatu (the eagle eye)
Tatizo unaandika kila linalokujia kichwani pasipo kuchuja matokeo yake.

Hapo kuna tatizo wapi Mkuu? Nimeuliza swali, nilipaswa kupewa majibu
 
Waliotakiwa kumhakikishia usalama wake hao hao ndio wanaoitafuta uhai wake, hivyo ni busara abaki huko misri hadi herode atakapotoka/tolewa madarakani
 
Petro E. Mselewa, post: 33090532, member: 116264"]

Hapo kuna tatizo wapi Mkuu? Nimeuliza swali, nilipaswa kupewa majibu
[/QUOTE]

Hebu soma vizuri uzi wako ulivyouwasilisha na urudie jambo la "motives of investigations against motives of law" na angalia hao watu wamekaa mahabusu muda gani na kesi zao zipo katika ngazi ipi kisheria na weka hatua sahihi zilizopaswa kuchukuliwa juu yao..
Kisha utaelewa kama wewe ni mwanasheria msomi au ni mzigo!

Any way, "All lawyers are liars"
 
Petro E. Mselewa, post: 33090532, member: 116264"]

Hapo kuna tatizo wapi Mkuu? Nimeuliza swali, nilipaswa kupewa majibu

Hebu soma vizuri uzi wako ulivyouwasilisha na urudie jambo la "motives of investigations against motives of law" na angalia hao watu wamekaa mahabusu muda gani na kesi zao zipo katika ngazi ipi kisheria na weka hatua sahihi zilizopaswa kuchukuliwa juu yao..

Any way, "All lawyers are liars"
[/QUOTE]
Mkuu, jambo hilo linaratibiwa na Sheria. Na taratibu za kisheria zinafuatwa. Kama ni tatizo, basi ni Sheria husika.
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
Nje ya mada, hivi kuna wakili msomi na ambaye sio msomi? Kama ndivyo, unaweza kutupa tofauti zao mkuu?
 
Shida ya Tundu Lisu ni narcissistic, anajiona ni bora kuliko wengine, yaani Serikali yetu imhakikishie yeye usalama na sisi je?

Tell him to go hang!
 
Hebu soma vizuri uzi wako ulivyouwasilisha na urudie jambo la "motives of investigations against motives of law" na angalia hao watu wamekaa mahabusu muda gani na kesi zao zipo katika ngazi ipi kisheria na weka hatua sahihi zilizopaswa kuchukuliwa juu yao..

Any way, "All lawyers are liars"
Mkuu, jambo hilo linaratibiwa na Sheria. Na taratibu za kisheria zinafuatwa. Kama ni tatizo, basi ni Sheria husika.
[/QUOTE]

Petro E. Mselewa ,

Sasa hapo ndio ufahamu kuwa tuna tatizo kubwa sana katika mifumo ya sheria, ninyi wanasheria na mahakama hadi watendaji wa ofisi zinazoshughulikia misamaha, na vyuo vikuu navyo nyimbo ni za kuigiza kutoka ulaya

Shida kubwa sana kwa Tanzania ni kwamba, hii mifumo tumeinga kwa wazungu koko; bora tutumie yetu tutafika salama.
 
Back
Top Bottom