Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.
Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.
Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.
Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.
Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.
Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?