Wakili Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ili arejee nchini. Lakini, nani hasa amhakikishie usalama wake ili arejee nchini?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
 
Hua unahangaika sana na Lissu mkuu,sijui tatizo nini?
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu aa hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
 
Mkuu, kama serikali haina wajibu wa kumuhakikishia kila raia usalama inakuwaje kuna watu wana bodyguards....!!

Sema kwa Lissu issue iko completed kwa vile kwa maoni yake mtuhumiwa ni serikali.
Atarudi akiwa kibabu maana file lake watapokezana tu
 
Chama chake, kama watahakikisha wanamuwekea ulinzi wa kutosha hasa vijana wa redi brigedi
 
Petro E. Mselewa , Wewe siyo wakili msomi kwa bandiko lako kuhusu rais kukosolewa ; mtizamo wako haukuwa wa kisomi hata chuo chako wanajuta kukuruhusu kuhitimu ili hali hukustahili kabisa.

Lissu, kwa sasa hajielewi kabisa. Mtu timamu huwezi ukategemea viongozi wako wa chama cha siasa tena kisichokuwa kwenye madaraka kuhakikisha usalama wako unaporudi nchini.

Ningemuona Lissu anajitambua kama angesema yaani angalau familia yake na serikali kwa sababu kuu mbili:
1. Familia imekuwa naye muda wote na ndiyo tegemeo lake kubwa
2. Serikali ; kwa vile ni jukumu la serikali kulinda watu wake; tena kauli ya kuomba ulinzi wake kutoka serikalini ungeiweka serikali katika mazingira ya kumlinda sana kuogopa kupata doa .

Sasa hapo bado hatujui aliyefanya yale kwake; je; kama ni viongozi wake wa chama chake walitaka kumtoa roho ili kuichafua serikali au kulinda madaraka ya baadhi ya watu katika chama chake?

Any way, Lissu baki tu huko , ule hela huko duniani huko singinda achana nako.
 
Unajuwa huyu jamaa anajihangaisha sana jeshi la polisi limeshasema na ni wajibu wake kulinda raia na mali zao sasa huyu anataka spesho uspesho yaani atokee mtu aseme mimi nitakulinda lissu popote utakapo kuwa sasa kila mtu akiwa anataka uspesho huo kutakuwa na askari wangapi? yeye ni nani hasda mpaka amsumbue IGP kumpangia mtu wa kumlinda?
 
Nimejipa muda kutafakari kauli ya Wakili Msomi mwenzangu na Mwanasiasa Tundu Antipas Mughwai Lissu kuhusu 'kuhakikishiwa' usalama wake ili arejee nchini kufuatia kumaliza matibabu yake nchini Ubelgiji. Akihojiwa na Mtangazaji Mwandamizi wa Sauti ya Amerika, Mwamoyo Hamza, Lissu amesema kuwa ameshamaliza matibabu yake na atarejea Tanzania yetu atakapohakikishiwa usalama wake.

Nikiri kuwa Wakili Msomi Tundu Lissu ana hoja kuhusu usalama wake ikizingatiwa shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma Septemba 7 mwaka 2017. Shambulio lile, kwa vyovyote vile, limeacha majeraha ya kutosha kwenye mwili na roho ya mwanasiasa huyu machachari wa Tanzania kupitia CHADEMA. Tukio lake litachukua muda wa kutosha kusahaulika kwake kwakuwa yeye tu ndiye mwenye picha na taswira ya kuogofya ya tukio husika kwa muda na mahali pale.

Lissu, kama alivyo binaadamu yeyote, yuko sahihi kutanguliza usalama kuliko kazi, tasnia au harakati zake za kisiasa. Hata kula na kulala hunoga pale ambapo usalama unapokuwepo. Hivyobasi, ni vigumu kubishana na hoja yake ya usalama wake na hoja yake ya kutaka kuhakikishiwa usalama huo ili aweze kurejea nchini. Ametoa na mifano ya vitisho juu ya usalama wake atakaporejea nchini. Kimsingi, ana hoja ya maana sana kwakuwa usalama huanza.

Lakini, nani hasa wa kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea nchini? Inajulikana kuwa jukumu la usalama wa raia na mali zao ni jukumu la Serikali kupitia vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama. Kila kunapokucha, Serikali hutimiza wajibu huo ingawa wahalifu wa makosa mbalimbali na uhalfu hutokea kwakuwa uhalifu huo hufanyika ima gizani au ghafla. Hakuna nchi ulimwenguni ambapo hakuna matukio ya kihalifu pamoja na uwepo wa Serikali na vyombo vyake.

Serikali, kadiri nijuavyo, haina wajibu wa kumhakikishia mtu mmoja usalama wake kuliko wengine. Usalama wa raia wote na mali zao zote hutazamwa kwa pamoja. Na hakika, Serikali iko makini katika hilo kwakuwa matunda ya kuwepo kwa amani na utulivu tunayafaidi kila kukicha. Naamini,haitakuwa rahisi kwa Serikali 'kumhakikishia' usalama wake Lissu ili arejee nchini. Usalama wa raia wote daima upo na unasimamiwa na Serikali.

Nani anayebaki ambaye ataweza kumhakikishia Lissu usalama wake ili aweze kurejea Tanzania?
eti nawewe una shahada ya sheria!!! so sadness
 
Petro E. Mselewa , Wewe siyo wakili msomi kwa bandiko lako kuhusu rais kukosolewa ; mtizamo wako haukuwa wa kisomi hata chuo chako wanajuta kukuruhusu kuhitimu ili hali hukustahili kabisa.

Lissu, kwa sasa hajielewi kabisa. Mtu timamu huwezi ukategemea viongozi wako wa chama cha siasa tena kisichokuwa kwenye madaraka kuhakikisha usalama wako unaporudi nchini.

Ningemuona Lissu anajitambua kama angesema yaani angalau familia yake na serikali kwa sababu kuu mbili:
1. Familia imekuwa naye muda wote na ndiyo tegemeo lake kubwa
2. Serikali ; kwa vile ni jukumu la serikali kulinda watu wake; tena kauli ya kuomba ulinzi wake kutoka serikalini ungeiweka serikali katika mazingira ya kumlinda sana kuogopa kupata doa .

Sasa hapo bado hatujui aliyefanya yale kwake; je; kama ni viongozi wake wa chama chake walitaka kumtoa roho ili kuichafua serikali au kulinda madaraka ya baadhi ya watu katika chama chake?

Any way, Lissu baki tu huko , ule hela huko duniani huko singinda achana nako.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom