Wakili mwandamizi wa Serikali (Senior state attorney upatikana kwa umahiri wa kazi au ni kwa muda mrefu kazini?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
483
1,000
Nimekuwa nafuatili Sana kesi zilizofunguliwa Kisutu, Mahakama Kuu na Mahakama ya Mafisadi. Mara nyingi Mawakili wa serikali uongozwa na wakili ambaye utambulika Kama "Senior state attorney", kwa kiswahili kisicho rasmi Ni wakili Mwandamizi wa serikali.

Kwangu Mimi maana ya " senior" ni mtu mkubwa kicheo au ni daraja la juu kwenye taasisi na kutoka hapo upandishwa kuwa Mkurugenzi au mkuu wa Idara. Hoja yangu mimi imejitikita kutaka kujua Hawa Mawakili ufikia kuitwa "Senior " kutoka na vigezo gani? Je, nikutokana na promosheni za miaka waliyokaa kwenye cheo kimoja bila kujali amefanya vitu gani? Je uajiriwa moja kwa moja katika cheo hiki? Upendekezwa na timu flani ya watu? Na Kama upendekezwa je vigezo vya usahili huwa ni vipi?

Naomba wale ambao mnajua wanapatikanaje Hawa watu mtusaidie kwa sababu aidha hatuna watu sahihi waliopewa hivi vyeo au mfumo mbovu unaotumika ndio unaozalisha aina hii ya watu au upo upendeleo wakuwapata watu wasio na sifa nakuwapa hizi nafasi au vinginevyo.......kinachotokea mahakama ya Mafisadi kwamba wakili wa serikali anashindwa hata kuuliza maswali na ndiye Kiongozi wa jopo la mawakili kinafikirisha sana kuhusu uwezo wa uelewa na umairi wa watendaji Hawa. Nakumbuka walikuwepo akina nchimbi nao walikuwa wa sampuli hii hii, tatizo lipo wapi?

Niombe tujadili may be kupitia mjadala huu na kwakuzingatia wote tumesoma humu kinachotokea kwenye kesi ya Ugaidi inayoendelea Waziri wa Sheria, Katibu mkuu wake na DPP atajifunza kitu. Tukumbuke Hawa seneor ndio wawakilishi wetu kwenye kesi hata za nje vinginevyo ukachukua waalimu vyuoni ambao pia Naamini hawana uzoeefu.

Tujadili kadhia hii ya kitaaluma tunayoiona tulisaidie Taifa.
 

Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,622
2,000
Ujinga na upumbavu ulioko serikalini ni kwamba mtu anaitwa senior ama principal kwa muda aliokaa kazini na sio kwa kazi alizofanya.

Serikalini hupandishwi daraja ama cheo cha ukuaji kwa sababu ya performance bali miaka uliokaa kazini.

Hata uwe ndezi vipi unajua after may be 5 year nakua senior, after 12 nakua principal na mambo kama hayo.

Siku serikalini wakianza kupandishana madaraja kwa kufuata utendaji kazi watafika mbali sana.
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,128
2,000
Ni cheo unapandishwa , senior state attorney au nadhani anaweza kuwa principal. Am not sure Ila ni cheo Cha kikazi unapanda baada ya kufanya kazi kwa muda muafaka na utendaji wako pia.
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,128
2,000
Ujinga na upumbavu ulioko serikalini ni kwamba mtu anaitwa senior ama principal kwa muda aliokaa kazini na sio kwa kazi alizofanya.

Serikalini hupandishwi daraja ama cheo cha ukuaji kwa sababu ya performance bali miaka uliokaa kazini.

Hata uwe ndezi vipi unajua after may be 5 year nakua senior, after 12 nakua principal na mambo kama hayo.

Siku serikalini wakianza kupandishana madaraja kwa kufuata utendaji kazi watafika mbali sana.
Kuna watu wamekaa na cheo kimoja miaka mingi aisee na sio sababu ukikaa miaka mitano unapandishwa tu lakini unayosema nayo yamo sana. But kupanda cheo inategemea na utendaji pamoja na elimu. Huwezi kuwa principal na hauna Masters pia. So hata kama ni upendeleo Ila while iwepo pia plus muda wa kazini pamoja na utendaji mzuri although hapo kwenye utendaji nakubaliana nawe, unakutana na ndezi tu unamgaragaza Mahakamani vizuri kabisa na unaona kabisa no mweupe mno.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom