Wakili Mwale na wenzake waomba wafungwe wamechoka kusota mahabusu

  • Thread starter Mwanahabari Huru
  • Start date

Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,530
Likes
27,511
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,530 27,511 280
WAKILI Maarufu jijini Arusha, Median Mwale na washitakiwa wenzake watatu wamemtaka Naibu Mkurugenzi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Oswald Tibabyekomya atumie mamlaka aliyonayo kuwafunga kuliko kuendelea kuwatesa kwa kesi isiyofika mwisho kwa zaidi ya miaka sita sasa.

Aidha mshitakiwa Mwale aliieleza mahakama kuwa mawakili wa Serikali juzi walimdanganya jaji David Mrango kuwa akiwaachia huru hawatakamtwa tena lakini walipotoka nje walikamtwa hivyo akaomba taratibu za usomaji wa mashitaka zifanyike kwa mujibu wa sheria kwani licha ya upande wa jamhuri kudai suala hilo ni dogo lakini wanaweza kubadilika.

Waliyasema hayo leo mbele ya hakimu Mkazi, Nestory Barro, wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha mara baada ya wakili Mkuu wa Serikali, Tibabyakomya na Wakili mwandamizi wa Serikali, Shedrack Kimaro kuwasomea mashitaka 42 yakiwemo ya kula njama, kutatisha fedha haramu, kugushi nyaraka na kukutwa na mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu.

Kwenye mashitaka hayo wakili Mwale anakabiliwa na mashitaka 29, raia wa Kenya, Don Bosco anakabiliwa na mashitaka mawili, Eliasi Ndejembi akikabiliwa na mashitaka sita huku Boniface Mwimbwa akikabiliwa na mashitaka 11.

Mara baada ya kusomewa mashitaka hayo ambayo hawakutakiwa kuyakubali au kuyakana, Ndejembi alimuomba hakimu ampe ruhusa ya kusema jambo ambapo hakimu alimpa ruhusa.

"Mimi si mtaalam wa sheria lakini sarakasi zimeshaendelea mara nyingi ni bora waamue watufunge kuliko kuendelea kututesa magereza familia zetu zinateseka. Tuna taarifa umepandishwa cheo tunaomba utumie mamlaka yako kutufunga kuliko kututesa mahabusu miaka yote hii" alisisitiza mshitakiwa Ndejembi.

Wakili mwale aliunga mkono hoja ya mshitakiwa mwenzake huku akifananisha shauri hilo na timu za mpira za Simba na yanga huku alitokea mfano kuwa kila wanapoifunga yanga wanaibuka na sababu za kukataa ushindi wakitoa sababu zisizo na msingi kutaka mchezo uanze upya.

"Kesi imeanza mwaka 2011, kimsingi shitaka ni moja ila maelezo yanawekwa mengi, leo tunarudi kusomewa shitaka kwa mara ya nne, hata jana jaji, (David Mrango) wakati akitoa uamuzi wake aliwaambia kama mnafuta shitaka kuja kutunga ushahidi sitakubali lakini kama mnaifuta ili washitakiwa watoke gerezani nakubaliana na nyie washitakiwa wawe huru," alisema wakili Mwale.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa ni heri shauri hilo likasikilizwa kama wanafungwa ni sawa kuliko wanavyoendelea kusota magereza Kwa zaidi ya miaka sita sasa huku shauri likishindwa kumalizika huku akisisitiza kuwa haki inayocheleweshwa ni sawa na haki iliyopita.

Hata hivyo Wakili wa mkuu Serikali, Tibabyekomya, hakujibu hoja hizo ambapo alisimama na kusema upelelezi wa shauri hilo umekamilika hivyo hakimu Mkazi Baro ameliahirisha mpaka mpaka novemba 3, mwaka huu.
 
Malyenge

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Messages
5,888
Likes
2,168
Points
280
Age
48
Malyenge

Malyenge

JF-Expert Member
Joined Jan 16, 2012
5,888 2,168 280

Katika vitu vinavyokera nchii hii ni kesi kuchukua muda mrefu. Shenzy kabisa!
 
Forum statistics

Threads 1,238,022
Members 475,830
Posts 29,310,031