Wakili Msando atoa neno zito kwa Serikali

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wakilii Maarufu nchini,Albert Msando ameitaka serikali kubadili mfumo wa uendeshaji wa shule zake za Msingi ili kuleta tija ya elimu iliyobora na kuendana na uwiano ulio sawa na shule binafsi zenye mchepuo wa kiingereza zilizoonekana kutoa elimu iliyobora na kuwa kimbilio la wazazi kupeleka watoto wao.

Msando ambaye pia ni kanda wa chama cha Mapinduzi( ccm)alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki wakati alipohudhulia Mahafali ya 11 ya shule ya Msingi Yakini yenye mchepuo wakiingereza iliyopo Kisongo Nje Kidogo ya jiji la Arusha na kueleza kuwa elimu inayotolewa kwa shule za msingi na sekondari za serikali bado ni duni.

"Ni Kweli kabisa wala sio jambo la kuonea aibu elimu zetu zinazotolewa kwa shule za msingi na sekondari za serikali bado ipo chini na ni duni huwezi ukalinganisha na ile inayotolewa kwa shule binafsi "Alisema Msando.

Akiitaka serikali kuachana na mfumo wa kutoa elimu kwa wasiojiweza(kipato duni)badala yake iweke kipaumbele cha elimu iliyobora kwa shule zake zote jambo ambalo anaamini litasaidia taifa kuondokana uwepo wa wahitimu wasiojua kusoma na kuandika

Amesema kuwa pamoja na kwamba kila serikali inayoingia madarakani inakipaumbele chake ,ikiweno awanu ya tano yenye kipaumbele cha kujenga uchumi kupitia viwanda,ipo haja kwa serikali kuweka kipaumbele pia cha elimu iliyo bora .
Hata hivyo Msando aliwataka wazazi kuhakikisha wanawekeza kwenye elimu kwa kumpatia mtoto elimu iliyobora itakayomsaidia kujiajiri ama kuajiriwa kwa haraka zaidi na.hatimaye kuchangia kukuza uchumi wa taifa.

Awali meneja wa shule hiyo ya Msingi Yakini,Christian Kimaro alisema kuwa shule yake imekuwa na mafanikio makubwa ya ufaulu kutokana na mikakati mikubwa ya uendeshani waliojiwekea.

Pamoja na mafanikio ya kielimu na kuiwezesha shule hiyo kushika nafasi mbalimbali za juu kiwilaya na Mkoa kila mwaka ,amesema zipo changamoto kadhaa zinazoikabili shule hiyo ikiwemo jengo la Maktaba.

IMG-20190916-WA0003.jpeg
 
Inatosha Siku kwa Maovu yake
Sisi ni zaidi ya hao nyuni wa Angani tusichukuliane Poa
Walimu tunapambana
Over
 
Huyu kachanganyikiwa nini, ukiwauliza ccm wenzake kuhusu mambo wanayojivunia kuhusu Magufuli wao ni elimu bure kwa wanyonge.
Kuiponda elimu bure ni kumponda Magufuli, sasa wameanza kugeuka au ndio wameanza kujitambua?!
Sasa naelewa inawachukua ccm muda mrefu kuelewa, huwa naona wanapongeza humu kumbe wanakuwa hawaelewi.
 
Wakili Msomi.....Kwa uelewa wangu,unatakiwa kuwa Pro serikali at any cost,hata kama kiwango kinachotolewa ni cha chini.
 
Naona Msando amevimbiwa sasa. Lakini sio mbaya, unadhihirisha kuwa kanda ile wapo wapo ccm tu kwa sababu maalum. Mtanyooka tu
 
Hivi Msando bado ni Wakili Msomi au akishatoka upinzani usomi unaisha? maana kipindi yupo upinzani alikuwa anatambulishwa kama Wakili Msomi lakini kwa sasa anatambulishwa kama Wakili Maarufu...!!!
 
Ameongelea jambo muhimu sana, ni lazima serikali ijikite ktk ubora wa elimu itolewayo zaidi ya hivi sasa ikiwa inafarijika na wingi wa shule na idadi ya wanafunzi.
 
Back
Top Bottom