Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance?

IPP CARES FOR YOU Does it really care for you? nafahamu kuwa wana JF mnajua jinsi ilivyokuwa NBC ilivyofilisiwa, kama na sisi tungekuwa kwenye "civilised" countries nadhani lile kofia la NBC lingefunuliwa tujue nini kimefunikwa.
 
Kwahiyo Masha ndiyo anataka kufunua hilo "kofia" la NBC ili tuweze kujuwa alivyonufaika na Deep Green Finance?
 
Kwahiyo Masha ndiyo anataka kufunua hilo "kofia" la NBC ili tuweze kujuwa alivyonufaika na Deep Green Finance?

hiyo sio maana yangu, lakini inawezekana kuwa kufunuliwa kwa hiyo kofia kukatumiwa kuwa njia ya kuinyamazisha IPP kusema ukweli kuhusu ufisadi, just looking at all facets of the saga, tusiangalie personalities tu, let us look a bit beyond them.
 
Kwani saga la NBC limekaa vipi? Sidhani kama ndugu Mengi ni responsible for ufisadi anyways.
 
Mwanakijiji naona imefika wakati huna la maana la kufanya.... With all due respect, Mengi kakukatia ngapi?

He! wee vipi?

Hata kama wewe ndo Dingi la Sangara wote lake V taratibu baba.
Usiingie kwa pupa hapa si Lake Victoria ni JF.
Siyo kila maji Baba Sangara anatamba.
 
Kwani saga la NBC limekaa vipi? Sidhani kama ndugu Mengi ni responsible for ufisadi anyways.

Mkuu Mushi,
Ndio maana wengine wanasema tukianza kufunua kila kofia tunaweza kuona hata ambayo hatukutegemea. kuzaliwa kwa IPP kwa kiasi fulani kuna uhusiano na kuyeyuka kwa mabilioni ya NBC lakini i am not sure Mengi as a person anahusika vipi, lakini kuna IPP connection kwenye saga hiyo.
 
Masha ni fisadi na kuhusika kwake na ufisadi ni jambo ambalo nimekuwa nalisema toka wakati ule wa issue ya mwanahalisi na pia wakati wa issue ya Ridhiwani Kikwete na kampuni la kifisadi la IMMA (IMMMA).

Ugomvi wa Masha dhidi ya Mengi ni kwa sababu Thisday na Kulikoni wameendelea kushika bango ufisadi (wa deep green, kagoda nk) wakati ambapo Masha na serikali walitegemea watanzania kukaa kimya baada ya Mramba na Yona kupelekwa mahakamani.

Masha wewe ni fisadi, tena umeanza kutisha na hizi amri zako za siku saba. Kama bado unabisha basi unaweza kunipa mimi siku saba ili tukutane mahakamani. Nadhani mimi na wewe tunajuana vizuri sana na unajua kuwa najua kuwa unajua kuwa ninajua kile ambacho unajua kuwa ninakijua.

Msitari wa kuwaogopa mafisadi ulichorwa pale mlipoanza kutuma watu kuja US ili kujua wana JF..... nenda mahakamani kama hukupenda nilichoandika.

Sijui nitakua nakwenda off-point, lakini naomba kuuliza... Hivi dada angu mwafrika wa kike ni kweli walitumwa watu kwenda US kuwatafuta wanaJF? What was the outcome? Walitumia funds gani kufanikisha hili zoezi na walifanikiwa kwa kiasi gani?
 
Vigogo wawindana serikalini

• Mzozo wa Mengi, Masha

na Charles Mullinda
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KUVUJA kwa mikakati ya siri serikalini kumetajwa kuwa chanzo kikuu cha mzozo unaoendelea hivi sasa kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha na mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, Tanzania Daima Jumatano imedokezwa.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba, kauli aliyoitoa Mengi wiki iliyopita imesababisha baadhi ya maofisa wa juu serikalini kuanza kuchukua hatua za kuwasaka viongozi, wakiwamo mawaziri ambao wamekuwa wakivujisha taarifa mbalimbali ya kimaamuzi ndani ya serikali.

Chanzo kimoja cha habari kimeieleza Tanzania Daima Jumatano kwamba, hatua ya Waziri Masha kumpa Mengi siku saba zinazoisha kesho, akimtaka athibitishe madai yake kwamba kuna waziri kijana anayeongoza wizara nyeti, anayeshawishi serikali kumhujumu kibiashara, inalenga kumlazimisha mfanyabiashara huyo amtaje mtu aliyemweleza taarifa hizo ambazo kimsingi zilijadiliwa katika vikao viwili vikubwa vya ngazi ya kitaifa.

Hatua ya Masha kumuandikia Mengi barua ya kumtaka awasilishe ushahidi wa madai yake hayo, inaonekana kuwashtua baadhi ya wanasiasa ambao wameitafsiri hatua hiyo kuwa inayoweza kuwa na madhara makubwa kisiasa katika siku za usoni.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano unaonyesha kwamba, mshtuko huo ndio ambao katika siku za hivi karibuni umesababisha kuibuka kwa wanasiasa kadhaa wazito ambao ama wamejitokeza kumpinga Masha hadharani huku wengine wakitahadharisha na kutaka kusitishwa kwa malumbano haya.

Wanasiasa kadhaa wa CCM na wale wa upinzani waliozungumza na gazeti hili wanasema, lengo moja la mzozo huu wa sasa ni hatua ya baadhi ya viongozi serikalini kujaribu kumdhibiti Mengi ambaye katika miaka ya hivi karibuni vyombo vyake vya habari vimeonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhujumu kile wanachokielezea kuwa masilahi yao na ya taifa.

'‘Wakubwa kadhaa serikalini kwa kauli moja wamefikia hatua ya kuanza kumuona Mengi kuwa ni tatizo. Huyu jamaa haeleweki ana malengo gani kisiasa, kwani amekuwa nyuma ya kila jambo kubwa hapa nchini. Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, kwa kweli ni lazima ashughulikiwe ipasavyo," alisema mbunge mmoja wa CCM anayeunga mkono hatua ya Masha kumpa Mengi siku saba.

Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alisema, pendekezo la kutaka serikali ichukue hatua ya kumbana Mengi lilitolewa kwanza katika kikao kimoja cha juu cha kiserikali kinachoshughulikia masuala ya usalama nchini kabla ya jambo hilo hilo kujadiliwa tena katika Baraza la Kazi linalojumuisha mawaziri kadhaa.

'‘Kilichoishtua serikali ni kumsikia Mengi akizungumza kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kikao kimoja nyeti cha kitaifa kinachohusisha watu wazito. Sasa jamaa walichofanya wanataka kumlazimisha Mengi amtaje mtu aliyempa taarifa hizo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake," kilisema chanzo kimoja cha habari.

Chanzo kingine cha habari kilichozungumza na Tanzania Daima Jumatano kinaeleza kwamba, tayari maofisa wa serikali wanaofuatilia nyendo za baadhi ya mawaziri wameshaanza kumtaja waziri mmoja anayeongoza wizara nyeti kuwa mtu ambaye alimpelekea Mengi taarifa za kuwapo kwa mjadala huo, ambao hata hivyo bado haujachukuliwa kuwa msimamo rasmi wa serikali.

Hata hivyo, katika hatua ambayo inaweza kumnusuru waziri huyo, habari hizo zinaeleza kwamba, siku na wakati vikao hivyo vikikaa, waziri huyo ‘anayetafutwa' hakuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao kimojawapo ambacho baadhi ya washiriki wake ni wakuu wa taasisi nyeti za dola.

Hata hivyo katika hatua nyingine, kuibuka kwa mzozo huo kumesababisha kuibuka kwa nadharia mbalimbali kuhusu utendaji na uwajibikaji wa viongozi serikalini.

Kundi moja la wadadisi wa mambo, wanakielezea kitendo cha waziri kupendekeza mfanyabiashara kuhujumiwa kuwa ni hatua ya kihalifu ambayo haipaswi kuungwa mkono kwa namna yoyote na serikali ambayo imeruhusu kisheria ushindani wa kibiashara katika misingi ya haki.

Miongoni mwa watu wenye mtazamo wa namna hii ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye anasema, ni jambo la fedheha kwa kiongozi wa dola kufikia hatua ya kufikiria kumhujumu mfanyabiashara mzalendo kwa kutumia njia za kihalifu.

Hata hivyo kundi jingine la wadadisi wa mambo, pasipo kuangalia uhalali au uharamu wa hatua hii ya kumdhibiti Mengi, wanaeleza kushangazwa na hatua ya maamuzi na mijadala nyeti serikalini kuvuja.

Mmoja wa wahadhiri waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyezungumza na gazeti hili, alisema kuwa, kufanikiwa kwa Mengi kunasa siri za kikao nyeti serikalini, kunaashiria kuwapo kwa mgawanyiko mkubwa kati ya viongozi waandamizi.

"Mengi si mjumbe wa vikao nyeti serikalini, hivyo kuibuka kwake na kueleza kuwa amenasa taarifa kutoka ndani ya vikao vya juu vya viongozi waandamizi, kuna maana kwamba, yupo kiongozi ambaye ni mjumbe wa kikao hicho aliyemfikishia kile kilichojadiliwa ndani ya kikao hicho au mjumbe huyo alikifikisha kwa rafiki wa karibu na Mengi, hivyo kuwa rahisi kumfikia.

"Na hii maana yake ni kwamba, serikali haiko salama, maana nyingine ni kumfikishia ujumbe Rais Kikwete kuwa anaoshirikiana nao kuongoza wanamzunguka au wanazungukana. Lakini ujumbe muhimu kwa rais ambao mimi naona Mengi ameamua kumtumia ni kwamba baadhi ya wasaidizi wake hawafai kuwa viongozi, hawajui nini maana ya siri za serikali," alisema msomi huyo.

Mwingine mwenye mtazamo huo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alieleza kuwa Waziri Masha hapaswi kumtisha Mengi kwa kumpa siku saba ili kutoa ushahidi wa madai yake, kwa sababu hata yeye (Zitto) amepata kuzisikia taarifa hizo.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alikaririwa hivi karibuni akieleza kuwa ana taarifa kuwa waziri mmoja ndiye aliyepeleka hoja ya kutaka serikali itumie vyombo vyake kumhujumu Mengi kwa kumbambikia kodi kubwa katika biashara zake.

Habari za hivi karibuni zilizoifikia Tanzania Daima Jumatano na kuthibitishwa na baadhi ya wanasiasa walio karibu na Zitto zinaeleza kuwa, Waziri Masha alishtushwa na kauli hiyo ya Zitto hata akafikia hatua ya kumtumia ujumbe mfupi kupitia simu yake ya kiganjani akimtaka kutojiingiza katika sakata hilo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Zitto mwenyewe zinaeleza kwamba, Masha alimweleza bayana kwamba, jitihada zake za kujaribu ‘kununua' kesi yake na Mengi haziwezi kumfanya ‘amuuzie' yeye.

Mengi katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, mbali ya kumzungumzia waziri huyo, alisema kuwa alitumiwa ujumbe wa vitisho vya kuuawa kwa sumu.

Sehemu ya maandishi yaliyo katika ujumbe wa maandishi wa simu uliotumwa kutoka simu namba 0768-373967, ulisomeka hivi: '‘Ni afadhali kunyofoa roho yako upotee kuliko kukuachia uchafue amani na utulivu kwa tamaa zako za kutaka kuwa rais... unachafua sana amani ya nchi kwa uchochezi wako. Tunajua unawahonga wahariri wote na kukusujudia kama Mungu mtu. Unapenyeza sumu kali ya uzandiki watu waichukue serikali. Hivi yakitokea machafuko wewe utasalimika? Wewe ni mnafiki mkubwa, unajifanya upo karibu na ‘Government' kumbe ni mnafiki wa kutisha. Jihadhari lazima tukuue!"

Siku chache baada ya Mengi kutoa madai hayo, Waziri Masha alitoa kauli ya kumtaka athibitishe madai ya kuwapo kwa waziri kijana anayefanya njama za kutaka kummaliza kibiashara.
 
Vigogo wawindana serikalini

• Mzozo wa Mengi, Masha

na Charles Mullinda
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KUVUJA kwa mikakati ya siri serikalini kumetajwa kuwa chanzo kikuu cha mzozo unaoendelea hivi sasa kati ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha na mfanyabiashara maarufu, Reginald Mengi, Tanzania Daima Jumatano imedokezwa.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kwamba, kauli aliyoitoa Mengi wiki iliyopita imesababisha baadhi ya maofisa wa juu serikalini kuanza kuchukua hatua za kuwasaka viongozi, wakiwamo mawaziri ambao wamekuwa wakivujisha taarifa mbalimbali ya kimaamuzi ndani ya serikali.

Chanzo kimoja cha habari kimeieleza Tanzania Daima Jumatano kwamba, hatua ya Waziri Masha kumpa Mengi siku saba zinazoisha kesho, akimtaka athibitishe madai yake kwamba kuna waziri kijana anayeongoza wizara nyeti, anayeshawishi serikali kumhujumu kibiashara, inalenga kumlazimisha mfanyabiashara huyo amtaje mtu aliyemweleza taarifa hizo ambazo kimsingi zilijadiliwa katika vikao viwili vikubwa vya ngazi ya kitaifa.

Hatua ya Masha kumuandikia Mengi barua ya kumtaka awasilishe ushahidi wa madai yake hayo, inaonekana kuwashtua baadhi ya wanasiasa ambao wameitafsiri hatua hiyo kuwa inayoweza kuwa na madhara makubwa kisiasa katika siku za usoni.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumatano unaonyesha kwamba, mshtuko huo ndio ambao katika siku za hivi karibuni umesababisha kuibuka kwa wanasiasa kadhaa wazito ambao ama wamejitokeza kumpinga Masha hadharani huku wengine wakitahadharisha na kutaka kusitishwa kwa malumbano haya.

Wanasiasa kadhaa wa CCM na wale wa upinzani waliozungumza na gazeti hili wanasema, lengo moja la mzozo huu wa sasa ni hatua ya baadhi ya viongozi serikalini kujaribu kumdhibiti Mengi ambaye katika miaka ya hivi karibuni vyombo vyake vya habari vimeonekana kuwa mstari wa mbele katika kuhujumu kile wanachokielezea kuwa masilahi yao na ya taifa.

‘‘Wakubwa kadhaa serikalini kwa kauli moja wamefikia hatua ya kuanza kumuona Mengi kuwa ni tatizo. Huyu jamaa haeleweki ana malengo gani kisiasa, kwani amekuwa nyuma ya kila jambo kubwa hapa nchini. Ameshiriki kutukifisha mahali pagumu sana, hata kusababisha serikali ishindwe kufanya kazi yake sawasawa, kwa kweli ni lazima ashughulikiwe ipasavyo,” alisema mbunge mmoja wa CCM anayeunga mkono hatua ya Masha kumpa Mengi siku saba.

Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina gazetini alisema, pendekezo la kutaka serikali ichukue hatua ya kumbana Mengi lilitolewa kwanza katika kikao kimoja cha juu cha kiserikali kinachoshughulikia masuala ya usalama nchini kabla ya jambo hilo hilo kujadiliwa tena katika Baraza la Kazi linalojumuisha mawaziri kadhaa.

‘‘Kilichoishtua serikali ni kumsikia Mengi akizungumza kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kikao kimoja nyeti cha kitaifa kinachohusisha watu wazito. Sasa jamaa walichofanya wanataka kumlazimisha Mengi amtaje mtu aliyempa taarifa hizo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

Chanzo kingine cha habari kilichozungumza na Tanzania Daima Jumatano kinaeleza kwamba, tayari maofisa wa serikali wanaofuatilia nyendo za baadhi ya mawaziri wameshaanza kumtaja waziri mmoja anayeongoza wizara nyeti kuwa mtu ambaye alimpelekea Mengi taarifa za kuwapo kwa mjadala huo, ambao hata hivyo bado haujachukuliwa kuwa msimamo rasmi wa serikali.

Hata hivyo, katika hatua ambayo inaweza kumnusuru waziri huyo, habari hizo zinaeleza kwamba, siku na wakati vikao hivyo vikikaa, waziri huyo ‘anayetafutwa’ hakuwa miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao kimojawapo ambacho baadhi ya washiriki wake ni wakuu wa taasisi nyeti za dola.

Hata hivyo katika hatua nyingine, kuibuka kwa mzozo huo kumesababisha kuibuka kwa nadharia mbalimbali kuhusu utendaji na uwajibikaji wa viongozi serikalini.

Kundi moja la wadadisi wa mambo, wanakielezea kitendo cha waziri kupendekeza mfanyabiashara kuhujumiwa kuwa ni hatua ya kihalifu ambayo haipaswi kuungwa mkono kwa namna yoyote na serikali ambayo imeruhusu kisheria ushindani wa kibiashara katika misingi ya haki.

Miongoni mwa watu wenye mtazamo wa namna hii ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye anasema, ni jambo la fedheha kwa kiongozi wa dola kufikia hatua ya kufikiria kumhujumu mfanyabiashara mzalendo kwa kutumia njia za kihalifu.

Hata hivyo kundi jingine la wadadisi wa mambo, pasipo kuangalia uhalali au uharamu wa hatua hii ya kumdhibiti Mengi, wanaeleza kushangazwa na hatua ya maamuzi na mijadala nyeti serikalini kuvuja.

Mmoja wa wahadhiri waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyezungumza na gazeti hili, alisema kuwa, kufanikiwa kwa Mengi kunasa siri za kikao nyeti serikalini, kunaashiria kuwapo kwa mgawanyiko mkubwa kati ya viongozi waandamizi.

“Mengi si mjumbe wa vikao nyeti serikalini, hivyo kuibuka kwake na kueleza kuwa amenasa taarifa kutoka ndani ya vikao vya juu vya viongozi waandamizi, kuna maana kwamba, yupo kiongozi ambaye ni mjumbe wa kikao hicho aliyemfikishia kile kilichojadiliwa ndani ya kikao hicho au mjumbe huyo alikifikisha kwa rafiki wa karibu na Mengi, hivyo kuwa rahisi kumfikia.

“Na hii maana yake ni kwamba, serikali haiko salama, maana nyingine ni kumfikishia ujumbe Rais Kikwete kuwa anaoshirikiana nao kuongoza wanamzunguka au wanazungukana. Lakini ujumbe muhimu kwa rais ambao mimi naona Mengi ameamua kumtumia ni kwamba baadhi ya wasaidizi wake hawafai kuwa viongozi, hawajui nini maana ya siri za serikali,” alisema msomi huyo.

Mwingine mwenye mtazamo huo, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, alieleza kuwa Waziri Masha hapaswi kumtisha Mengi kwa kumpa siku saba ili kutoa ushahidi wa madai yake, kwa sababu hata yeye (Zitto) amepata kuzisikia taarifa hizo.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alikaririwa hivi karibuni akieleza kuwa ana taarifa kuwa waziri mmoja ndiye aliyepeleka hoja ya kutaka serikali itumie vyombo vyake kumhujumu Mengi kwa kumbambikia kodi kubwa katika biashara zake.

Habari za hivi karibuni zilizoifikia Tanzania Daima Jumatano na kuthibitishwa na baadhi ya wanasiasa walio karibu na Zitto zinaeleza kuwa, Waziri Masha alishtushwa na kauli hiyo ya Zitto hata akafikia hatua ya kumtumia ujumbe mfupi kupitia simu yake ya kiganjani akimtaka kutojiingiza katika sakata hilo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Zitto mwenyewe zinaeleza kwamba, Masha alimweleza bayana kwamba, jitihada zake za kujaribu ‘kununua’ kesi yake na Mengi haziwezi kumfanya ‘amuuzie’ yeye.

Mengi katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, mbali ya kumzungumzia waziri huyo, alisema kuwa alitumiwa ujumbe wa vitisho vya kuuawa kwa sumu.

Sehemu ya maandishi yaliyo katika ujumbe wa maandishi wa simu uliotumwa kutoka simu namba 0768-373967, ulisomeka hivi: ‘‘Ni afadhali kunyofoa roho yako upotee kuliko kukuachia uchafue amani na utulivu kwa tamaa zako za kutaka kuwa rais... unachafua sana amani ya nchi kwa uchochezi wako. Tunajua unawahonga wahariri wote na kukusujudia kama Mungu mtu. Unapenyeza sumu kali ya uzandiki watu waichukue serikali. Hivi yakitokea machafuko wewe utasalimika? Wewe ni mnafiki mkubwa, unajifanya upo karibu na ‘Government’ kumbe ni mnafiki wa kutisha. Jihadhari lazima tukuue!”

Siku chache baada ya Mengi kutoa madai hayo, Waziri Masha alitoa kauli ya kumtaka athibitishe madai ya kuwapo kwa waziri kijana anayefanya njama za kutaka kummaliza kibiashara.

I guess hilo "kundi la wadadisi wa mambo" litakuwa ni JF tuuu....

JF HOYEEEEE!!!!!!!!
 
1.
‘‘Kilichoishtua serikali ni kumsikia Mengi akizungumza kuhusu mambo yaliyojadiliwa katika kikao kimoja nyeti cha kitaifa kinachohusisha watu wazito. Sasa jamaa walichofanya wanataka kumlazimisha Mengi amtaje mtu aliyempa taarifa hizo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yake,” kilisema chanzo kimoja cha habari.

2.
Kundi moja la wadadisi wa mambo, wanakielezea kitendo cha waziri kupendekeza mfanyabiashara kuhujumiwa kuwa ni hatua ya kihalifu ambayo haipaswi kuungwa mkono kwa namna yoyote na serikali ambayo imeruhusu kisheria ushindani wa kibiashara katika misingi ya haki.

- Hapa ndio ninapoona ishu muhimu sana katika hili tatizo la Mengi na waziri, na kwamba likitatuliwa kisheria, basi litasaidia kisheria kutokuwepo na matatizo haya mawili juu ambayo ni tatizo kubwa sana kwa utawala wa kisheria na demokrasia kwa taifa letu.
 
I think it is the right time for Tanzania to consider bipartisanship. Kitu hiki kikiwepo, watanzania tunaweza epuka matatizo ya dizaini za Mengi vs Masha.

With bipartisanship, decision making will be based on values that both parties broadly agree on. Kutakua na kuoneana aibu katika kutenda mambo yasiyo ya msingi. Hii itasaidia kupunguza risk ya kuwepo kwa vikao vya mazungumzo yasiyo na tija ya kuzungumzia namna ya kuwashughulikia watu walio na mapenzi mema na nchi yao, kitu ambacho kinaweza wauma baadhi ya watu watakaokuwemo mkutanoni na kuishia ku-spill the beans, kama ilivyotokea kwenye case hii ya Masha vs Mengi. With Bipartisanship everybody will be accountable.

A bipartisan process is also less likely to accept mistaken evidence because many eyes from both parties will examine the evidence from different perspectives. Labda yote haya ni matokeo ya maandiko ya nyakati ambayo yanakaribia kutimia.... Lets wait and see
 
sikuwahi kufikir ipo sikuwatu wa aina ya mwanakijiji wanaweza kununuliwa ila kuna siku nilishwahi kuonywa kuhusu Mzee Mwanakijiji.Inakuwaje unakubali kunuliwa kirahisi hivi?

It is a good Move.Nahisi mwezi huu ni mbaya sana kwako.kuna mambo mawili matatu uliamua kujiingiza bila ya kuwa an ushahidi.Moja wapo la dr. Masau

Umekuwa ukiwalaumu watu kama Balile wananuliwa na wanasiasa ,wakati wewe uko kundi moja.Kila siku nahisi Nyani Ngabu yuko sawa kwa hili..Hivi ndivyo jinsi Tulivyo.
 
Masha inadaiwa kuwa anasemea pembeni kuwa "haijui Deep Green Finance" kwa undani na kuwa alikuwa hajui kuwa fedha walizotumia DGF kuwalipa IMMMA zimechotwa Benki Kuu!! Na kuwa yeye hajaonja hata senti moja! Anasema watu wanamtafuta tu kwa sababu ya wivu na majungu!

Ungejibu hivi toka mwanzo ningekupata vizuri, asante mkuu. Hii kwangu imetosha mana mengine yote umekumbushia tu.
 
nimezoea, I'm an equal opportunity anti fisadist!
Anti fisadi ungekuwa wewe Bwana.Kwa hili umekurupuka tu na unataka kuonesha Mengi yuko sahihi kwa kila kitu.

Dhambi ambayo Itaimaliza CHADEMA ndiyo hiyo ambayo inakusuta kwa hili na umepewa likusaidie kukumaliza.Hivi kwanini Mwanakijiji unataka kuwa kama kina Balile?
 
hahahha.. wewe hizo chuki zao dhidi ya Mengi msingi wake ni nani amekulipa? Au na wewe umenunuliwa na mafisadi vile vile kwa vile unampinga Mengi na unamuona fisadi? Ok, tukubaliane Mengi naye fisadi! so how does that help Masha?

Kwa vile wewe umenunuliwa, usidhani wote wanaweza kununuliwa.
 
Mimi nakushauri mlete hapa JF, yeye ni kijana, anajua vizuri kutumia mtandao, ajitambulisha hata kwa siku moja ili kujibu maswali ya wana JF. Kama hana cha kuficha wala hawezi kuogopa kuja JF.

Huyu yupo humu humu anachungulia anakimbia yupo tu kama wengine.Na anaona moto wake unao waka humu ila huyu FMES amechemka sana.NAona analinda masrahi ya munene wake anapalilia kibarua si na yeye Masha anachungulia huku kisha anakimbia.
 
Any way that is how things are under the carpet,but i think no one shall remain behind to this scandals.
 
Sijui nitakua nakwenda off-point, lakini naomba kuuliza... Hivi dada angu mwafrika wa kike ni kweli walitumwa watu kwenda US kuwatafuta wanaJF? What was the outcome? Walitumia funds gani kufanikisha hili zoezi na walifanikiwa kwa kiasi gani?

wao wakijua hili.... wajue kuwa.... yao mengi yanajulikana. Na tatizo lao, wengi wao ni walevi na wagoni kwa hiyo ni rahisi mno kuropoka siri zao.

Kuhusu kufanikisha zoezi lao.... naweza kusema kwa hakika kuwa wengi wao wameanguka mtihani... na kama kuna walichojua, basi ni kile ambacho kilikuwa wazi kwa kila mtu.

Eti kwa mfano mtu anataka kuhangaika kujua mwanakijiji ni nani - wakati ambapo mkjj ameweka namba yake ya simu hapa na au anawapigia watu simu kila now and then..... mambo mengine ni upuuzi mtupu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom