Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance?

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,191
0
We dare talk openly here, hebu mwaga kuku kwenye mchele wengi tujue na sisi, tehe tehe tehe teh.

Just wait for the tone .... message itaachwa hapa wazi and clear. Huyu Masha ni fisadi na haya mambo ya kutoa siku saba yamevuka kipimo cha kawaida cha uvumilivu.

tik tak tik tak tik tak .......
 

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,191
0
Bi. Mdogo, nilidhani hutomtolea uvivu; sasa kesho nadhani watanunua magazeti yotemaana kesho EPA itawekwa pembeni kidogo na watu kudili na ndugu yetu huyu. Natumaini watu wenye hekima watakuwa wamemkalisha chini kumpa ushauri.

yaani we acha tu,

Hapa hapewi breki... unajua madikiteta wanaaanza hivi. Wanaanza kwa kufungia magazeti na baadaye utasikia wamefunga vituo vya TV na kisha kupeleka watu Siberia kwa makosa yasiyojulikana.

Masha asikilize ushauri anaopewa la sivyo hiyo ndoto ya uraisi aliyonayo itaisha kabla usingizi kwisha.
 

Waga

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
322
195
Masha ni fisadi na kuhusika kwake na ufisadi ni jambo ambalo nimekuwa nalisema toka wakati ule wa issue ya mwanahalisi na pia wakati wa issue ya Ridhiwani Kikwete na kampuni la kifisadi la IMMA (IMMMA).

Ugomvi wa Masha dhidi ya Mengi ni kwa sababu Thisday na Kulikoni wameendelea kushika bango ufisadi (wa deep green, kagoda nk) wakati ambapo Masha na serikali walitegemea watanzania kukaa kimya baada ya Mramba na Yona kupelekwa mahakamani.

Masha wewe ni fisadi, tena umeanza kutisha na hizi amri zako za siku saba. Kama bado unabisha basi unaweza kunipa mimi siku saba ili tukutane mahakamani. Nadhani mimi na wewe tunajuana vizuri sana na unajua kuwa najua kuwa unajua kuwa ninajua kile ambacho unajua kuwa ninakijua.

Msitari wa kuwaogopa mafisadi ulichorwa pale mlipoanza kutuma watu kuja US ili kujua wana JF..... nenda mahakamani kama hukupenda nilichoandika.


Dada mkali huyu dah, tubgepata wanawake kama wewe angalau 1000 tu walahi tungeweza kuthibitisha kuwa wanawake nao wanaweza!!!!! N'way hongera sana dadangu kwa kutoa ndondo ya nguvu namna hii nina uhakika Mheshimiwa Masha akipotea njia aingie humu na kuona hii nondo kweli atajiona ni mchovu na kibalua chake kipo hatarini kuota mbawa, anhaaaaa FMES atamprintia ampelekeee hahahaha maana mwanzo nilimwambia kuwa nahisi kuna mgongano wa kimaslahi juu yake na makampuni ya mengi ndo mana anamuona Masha yupo sahihi akasema hakuna kitu kama hicho kuja kuangalia post zake amethibitiosha kuwa Masha ni swhiba wake wa nguvu doh komaa mwanangu FMES komaa bwana maana kama unajipatia ugali hapo wala usiache kumtetea lakini atakapokuja kuaibika ujue mtaaibika wote na sijui utatueleza nini hapa JF
 

Nikifufukammekwisha

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
260
0
wao wakijua hili.... wajue kuwa.... yao mengi yanajulikana. Na tatizo lao, wengi wao ni walevi na wagoni kwa hiyo ni rahisi mno kuropoka siri zao.

Kuhusu kufanikisha zoezi lao.... naweza kusema kwa hakika kuwa wengi wao wameanguka mtihani... na kama kuna walichojua, basi ni kile ambacho kilikuwa wazi kwa kila mtu.

Eti kwa mfano mtu anataka kuhangaika kujua mwanakijiji ni nani - wakati ambapo mkjj ameweka namba yake ya simu hapa na au anawapigia watu simu kila now and then..... mambo mengine ni upuuzi mtupu.

Walikwenda shopping tu Marikani... Si wanamuiga baba?

Pesa ya kununulia majenereta ya ICU kwenye mahospitali mara zote huwa hawana na wanafunga masafari kwenda nje kuomba misaada kwa kutumia vigezo butu kwamba Danganyika ni nchi masikini, ila safari zisizo na tija huwa zinapata mapesa kirahisi mno...
 

omarilyas

JF-Expert Member
Jan 24, 2007
2,130
1,195
DEEP GREEN + MASHA KUMLILIA LOWASSA + MASHA KUWATEMBELEA MAFISADI GEREZANI + MASHA KUMFILISI MENGI = ?

Ndugu zangu kwa kweli ni wazi sasa kuwa sitakua nimefanya dhambi kusema kuwa mbio za sakafuni huiishi ukingoni.

Mimi ni mmoja wa vijana waliokuwa wakiangalia uteuzi wa Masha kama mwanzo mzuri wa utekelezaji wa mapinduzi ya CHIMWAGA yaliyotoa ushindi kwa kizazi kipya cha uongozi wa CCM nchini. Kwa mara chache nilizopata kumuona Masha na michango yake katika mijadala niliamini kuwa akiacha ubrazameni basi ana mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya utamaduni wa kisisiasa nchini. Ingawa nilikuwa na maswali mengi kuhusu mwenendo wake kijamii lakini niliamini kuwa Masha akiwa kijana aliyepata bahati ya kuujua ulimwangu wa kidemokrasia, kuwa na upeo mzuri wa mambo ya kisiasa na kisheria na kutokana na historia yake kuwa katika siasa za upinzani kabla kurudi nyumbani CCM, basi angeweza kuwa kiungo muhimu katika juhudi za kubadili utando wa uongozi mbovu na usiojali demokrasia wala utawala bora miongoni mwa viongozi wetu wanaoshindwa kuona mbali zaidi juu ya hatima ya Tanzania na ile ya CCM.

Likaanza suala la kutoa siri za serikali akiwa maskani pale rosegarden, likaja la kumlilia Lowasa, likaja la nyumba ndogo hadharani, likaja la DEEP GREEN (nililisikia kabla lakini nikampa benefit of doubt), Likaja la kuandaliwa na kina ROSTAM na LOWASSA kushindana na JK 2010 (nikadhani ni yaleyale), Likaja la kuwatembelea MAFISADI gerezani, Mara sasa hili la mkakati wa kufilisi wanaothubutu kutoa sauti dhidi ya mfumo fisadi nchini mwetu....

Kwanza nilifikiri kuwa ni moja ya yale matamshi yake akishapata vinyaji vyake lakini kumbe ni kwenye kikao nyeti kabisa? Hii ni kali tena kutoka kwa mwanasheria aliyekulia katika mazingira kama ya MASHA. Kwa kweli hii sio tu ni kuvunjika moyo na vijana wenzangu lakini pia ni aibu kubwa sana.

Tukumbuke wako wengi ambao bado wanafikira ya kutokuamini kuwapa majukumu makubwa vijana. Kupewa nafasi kuwa waziri tena wa wizara nyeti kwa ndugu Masha kulikuwa ni muhimu katika kuwafanya wazee wetu waliogubikwa na fikira za kihafidhina kuamka na kuthamini mchango wa uthubutu wa vijana katika maswala ya uongozi. Makosa ya Lawrence Masha si tu yanatia aibu lakini pia ni pigo kubwa kwa wote wenye kuamini umuhimu wa kuwaamini vijana kupewa nyeti za uongozi. Kwa kifupi Masha amem......JK na ajenda yake ya kizazi kipya. Masha amewaangusha vijana wa Tanzania....

Tanzanianjema
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
0
anhaaaaa FMES atamprintia ampelekeee hahahaha maana mwanzo nilimwambia kuwa nahisi kuna mgongano wa kimaslahi juu yake na makampuni ya mengi ndo mana anamuona Masha yupo sahihi akasema hakuna kitu kama hicho kuja kuangalia post zake amethibitiosha kuwa Masha ni swhiba wake wa nguvu doh komaa mwanangu FMES komaa bwana maana kama unajipatia ugali hapo wala usiache kumtetea lakini atakapokuja kuaibika ujue mtaaibika wote na sijui utatueleza nini hapa JF

- Mkuu Waga heshima mbele bro, maneno yako hayawezi kusaidia anything maana nina mali zangu bro ambazo nimezipata kwa jasho langu, kuanzia ubaharia mpaka sasa ninamiliki kampuni yangu, yote toka kwenye jasho na damu yangu,

- Lau waziri ni rafiki yangu sana, lakini kama ana ufisadi ni wake sio wangu, na kwa taarifa yako hapa JF wananchi wengi wananifahamu sana na wanajua maisha yangu kua ni clean, tena kama unajua anything ya mimi kuhusika na ufisadi weka hapa mkuu, na kwa taarifa yako mtoto wangu wa kiume ni mcheza Cinema za cartoon za "Dora the Explorer Arround The World" sasa tafuta hii kitu utaona mtoto amevaa kimasai huyo ndio dogo wangu, halafu nenda "Sesame Street" nako utakuta vitu vya dogo sasa usinihusishe na ufisadi umekosa sana, sina utajiri lakini sina shida ndogo ndogo bro, ugali ninapewa na Mungu, unahangaika sana na jina langu kwamba siku likiharibika hapa itakuwa furaha yako maana ninakubana sana mbavu hapa JF, hasa kule Hall of fame,

- Sipendi haya ila mnanichokoza wenyewe, mimi siwezi kuabikia maana mimi sio mwizi wala fisadi, je vipi wewe huna ufisadi na viongozi wa bongo? Au tuuseme hapa? Mimi sina kama unao uweke hapa ninakupa ruhusa, na mimi unipe ruhusa nikufunue ufisadi wako na viongozi wa bongo tuwaachie wananchi waamue ukweli ulipo,

Usichezee moto nitakuchoma mkuu! Msinichokoze jamani hapa tunataka ishus sio FMES kila wakati enough mmeshanipa umaarufu wa kutosha na chuki zenu na wivu, sasa niacheni nikate ishus za taifa, maana maneno kama yako yanaharibu the topic nashangaa unaachiwa kuandika maneno ya hovyo kama haya hapa JF vipi Mods?

Tafadhali tuheshimiane mkuu kama ninavyokuheshimu. Sasa turudi kwenye ishus za taifa mimi ni mlalahoi saafi sana kama wengine, niacheni nikate ishus za taifa maana this now inakua ni kantankalous! Bwa! ha! ha! ha! ha! ha!

Wazee wa sauti ya umeme, super FMES!
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,301
2,000
Ashauri Waziri Masha achunguzwe EPA

2008-12-12 13:04:27
Na Ashauri Waziri Masha achunguzwe EPA (Nipashe)


Kada machachari wa CCM aliyehamia Chadema hivi karibuni, Mwita Mwikabe, amevishauri vyombo vya dola kuanza kumchunguza Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha endapo alihusika na wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Amesema kwa kuwa Masha alikuwa mmoja wa Wakurugenzi kwenye kampuni ya Deep Green iliyochota Sh. bilioni 10 kwenye akaunti ya EPA, lazima ahojiwe na ikibainika alihusika afikishwe mahakamani kuungana na wenzake 20.

Akizungumza na Nipashe jana, Mwikabe alisema Masha ameanza kutoa vitisho vya wanaoandika habari za ufisadi.

``Kabla ya kuanza kutishia watu wanaopiga vita ufisadi, lazima tujue uhusuika wake Deep Green, kampuni iliyoko kwenye kundi la mafisadi...Masha anaanza kujihami ili mambo yake yasianikwe kwa kutishia watu,`` alisema Mwikabe ambaye hivi karibuni alikuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Tanga.

Aidha, alisema watu wote waliohusika katika wizi wa fedha za umma, wamekuwa maadui wakubwa wa vyombo vya habari kutokana na kufichua uovu wao.

Wakati huo huo, Mwikabe alimshangaa Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba kwa kudai kuwa mjadala wa EPA umefungwa.

Alisema Makamba hastahili kutoa kauli kama hiyo kwani chama chake ndicho kinatuhumiwa kwa makosa yaliyotokea na kuisababishia serikali hasara ya mabilioni.

Alisema mtuhumiwa hawezi kuwa hakimu kwenye kesi yake mwenyewe.

``Walengwa kama Kagoda Agriculture Ltd hawajakamatwa halafu unasema mjadala umefungwa? yeye ni nani mpaka afunge mjadala,`` alisema Mwikabe.

Hivi karibuni, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, amemtuhumu Waziri mmoja wa Serikali ya Awamu ya nne kuwa ameagiza abambikiwe kodi bandia ya kiasi kikubwa atakachoshindwa kulipa ili hatimaye afilisiwe.

Alisema Waziri huyo ameahidi kunyamanzisha kabisa kutokana na kupigia kelele ufisadi.

Mengi alisema Waziri huyo amekuwa akijigamba kuwa atanyamanzisha kwa kuhakikisha anafilisiwa kama alivyofilisiwa tajiri mmoja huko Urusi.

Mengi alisema Waziri huyo anadai kuwa vyombo vyake vya habari vimekuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri na linawanyanyasa baadhi ya watu.

``Nilitarajia Waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanyakazi...anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na si mmiliki,``.alisema.

Alisema ingawa tayari amemsamehe Waziri huyo lakini anapaswa kujua kuwa asiyekemea maovu katika jamii anakuwa sehemu ya maovu hayo.

Alisema Waziri huyo na wale ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa vitisho lazima wakumbuke kuwa hata wakifanikiwa kunyamanzisha yeye (Mengi), moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za watanzania hauwezi kuzimika kamwe.
 

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
250
Kama kuna mambo huwa yananiudhi humu ni pale tunapovuka mstari wa hoja na kuingia upande wa pili wa kumshambulia mtoa hoja. Nafikiri siku zote kinachoshindanishwa hapa jamvini JF ni hoja na mwenye hoja tena hoja za kweli huibuka kidedea bila ubishi. Sasa hili la mara FMES hivi mara Mwanakijiji vile na kumhusisha mtu yeyote awaye aliyemo jamvini na mafisadi au na kutumwa na mafisadi bila ushahidi wowote nadhani si kitu kizuri.

Si siku zote lazima kila mtu akubaliane na hoja iliyopo mezani wakati mwingine tunatofautiana lakini hilo lisiwe jambo linaloweza kuharibu jamvi badala yake liwe kama chachu ya kuijenga zaidi JF yetu ili kila anayekuja na issue awe ameifanyia kazi kweli kweli kabla ya kuiweka hadharani.

Asanteni wakuu
 

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,004
2,000
THISDAY REPORTER
Dodoma

A MEMBER of parliament from the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) yesterday linked the Minister for Home Affairs, Lawrence Masha, to the mysterious Deep Green Finance Limited company that received dubious payments amounting to at least 10.5bn/- from the Bank of Tanzania in the run-up to the 2005 general elections.

Without mentioning Masha by name, Simanjiro MP Christopher Ole Sendeka said in Parliament that a Cabinet minister in the current fourth phase Government was involved in the Deep Green Finance scandal.

’’Deep Green is alleged to have received around 10bn/-. This is a company that was represented by a certain law firm linked to a Cabinet minister in this government,’’ said Ole Sendeka when contributing to the Bunge debate on the 2009/10 budget estimates of the Prime Minister’s Office (PMO).

’’We will continue to speak out as long as we are MPs, and I have no plans to relinquish my parliamentary seat any time soon,’’ the legislator added.

He called on the Government to ensure all individuals behind major scandal-hit companies in the country are prosecuted, citing Deep Green Finance and Kagoda Agriculture Limited from the BoT’s external payment arrears (EPA) embezzlement scam.

Although Ole Sendeka did not directly name Masha in the House, it is a widely-known fact that Deep Green Finance was registered by prominent local law company IMMMA Advocates.

And according to current information posted on the IMMMA Advocates website, the firm has seven partners - Protase R. Ishengoma, Lawrence K. Masha, Sadock Dotto Magai, Fatma Karume, Faustin A. Malongo, Gaspar Nyika, and Stella Ndikimi.

The current long version of the company’s official name is Ishengoma, Karume, Masha & Magai Advocates.

According to previous THISDAY findings, Deep Green Finance Co. Ltd was registered in Dar es Salaam on March 18, 2005 and issued with certificate number 51870 by the Business Registration and Licensing Authority (BRELA).

One of the IMMMA Advocates partners, Protase Rwezahura Gervas Ishengoma, was named as subscriber and first shareholder of the newly-registered company.

IMMA Advocates’ clients include a number of major banking and insurance corporations, and some well-known mining conglomerates in the country.

The law firm has also been involved in the privatization of a number of key parastatals, both as counsel for Government and on behalf of investors.

According to the IMMMA Advocates website, Masha is currently a non-active partner of the company.

’’Mr Masha is currently on sabbatical leave following his appointment as Cabinet member in Tanzania’s fourth phase Government,’’ the website states.

However, at the time of Deep Green Finance’s registration back in 2005, Masha was in fact still a practising partner in the law firm.

Official BRELA records also show that Deep Green Finance filed for ’’member’s voluntary winding up’’ on April 24, 2007, declaring that board members not identified in the document had appointed Protase Rwezahura Gervas Ishengoma as liquidator with effect from July 27 of the same year.

It has been established that during the relatively short time of its existence, the mysterious Deep Green Finance company was the beneficiary of a series of highly questionable payments from the BoT.

Furthermore, some of the payments are heavily linked to at least two dubious gold-related companies - TANGOLD Limited and its ’predecessor’ Meremeta Gold.

According to documents seen by THISDAY, the central bank transferred a total of 10,484,005.39/-to Deep Green Finance Ltd within a four-month period leading up to the 2005 general elections.

The payments were delivered in instalments between August 1 and December 10, 2005, with the election 'postponed from October' held in the final week of December that year.

But hardly a year-and-a-half later, Deep Green Finance Ltd unexpectedly filed for bankruptcy and voluntary liquidation, in a move bearing striking similarities to the Meremeta company case.

According to available official documents, the breakdown of the suspicious movements of huge amounts of cash through the Deep Green Finance company bank account is as follows:

- August 1, 2005: BoT deposited $1.354m into the company’s bank account through cheque number 241740. The funds were withdrawn on the same day by special clearance.

-September 1, 2005: BoT, through cheque number 015558, transferred another $1.827m to Deep Green Finance. The funds were again withdrawn by special clearance the same day.

-September 8, 2005: TANGOLD Limited transferred $100,256.62 to the Deep Green Finance account.

-September 16, 2005: A total of 129m/- (in Tshs) was withdrawn from the Deep Green Finance account and deposited in a special FDR account.

-October 3, 2005: A total of 2,083,333,333.33/- belonging to the Ministry of Finance was paid through special clearance from the Deep Green Finance company account.

-October 4, 2005: BoT deposited $1.789m into the Deep Green Finance account.

-October 8, 2005: A total of 39,761,397.98/- was transferred from Deep Green Finance to TANGOLD Limited.

-October 31, 2005: Some 2,083,333,333.33/- from the Ministry of Finance was transferred to the Deep Green Finance account.

-November 2, 2005: A total of $1.821m was withdrawn from the Deep Green Finance account.

-November 30, 2005: BoT deposited 2,083,333,333.33/- from the Ministry of Finance to an account owned by Deep Green Finance. The next day, $1.817m was withdrawn from the account.

-December 10, 2005: A total of 100,940,489.71/- was transferred from TANGOLD Ltd to Deep Green Finance.

-December 19, 2005: A total of $88,722.17 was withdrawn from the Deep Green Finance account.
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,587
2,000
By Guardian Reporter


26th June 2009Masha.jpg

Home Affairs minister Lawrence Masha


Home Affairs minister Lawrence Masha yesterday was put on the spot in the National Assembly over his involvement in a law firm linked to Deep Green Finance, which is among the companies alleged to have facilitated the illegal transfer of 215bn/- from the Bank of Tanzania (BoT).

On the attack line this time was Simanjiro legislator, Christopher Ole Sendeka, who during his contribution to the Prime Minister’s Office 2009/10 Budget estimates slammed the government for failure to offer a timely response in addressing high-profile corruption.

The ruling CCM MP charged that Masha and other leaders who played a role in the widely publicised grand corruption scandals in the country should be disciplined by state agents, regardless of their positions in the governance system.

Pointing an accusing finger directly at Masha, the lawmaker said, the minister should help agencies probing the matter in identifying the culprits by using his connections inside the IMMA law firm to shed some light on the alleged transfer of 10bn/- from central bank through Deep Green Finance.

He said the fact that Masha was linked to IMMA, put him in a position to help in probing the illegal transfer of money from the central bank, because the law firm used the services of Deep Green Finance.

Sendeka dismissed suggestions championed by people inside and outside the parliamentary debating chamber that public discussion on grand corruption cases should be stopped and instead people should pick other agenda or talk about other development issues.

Quoting teachings from the holy Prophet Muhammad, the Simanjiro lawmaker said both leaders and members of CCM should fight corruption by actions, words and their hearts.

He told Parliament that the holy Prophet of Islam taught that if one was annoyed or disliked something, he or she should get rid of it by using his own hand, speak out about it or if unable, condemn it through the heart.

As a lawmaker, Sendeka said, he would continue speaking openly of the evils of grand corruption until state authorities address the issues of Kagoda, Deep Green Finance and all pending scams exhaustively.

“We shall keep on shouting about Kagoda, Deep Green Finance and other grand corruption cases until the government takes decisive actions to curb the deepening problem,” vowed the MP, warning: “If the government takes no action, we shall keep on shouting about it as long as we are alive and serve the people as Members of Parliament.”

Earlier, Sendeka supported comments by Anne Kilango (Same East, CCM), who early this week vowed in Parliament to keep on fighting alongside fellow lawmakers and other volunteers in the war against grand corruption in the country.

He dismissed assertions that the ruling party was harbouring leaders and members linked to grand corruption scams. “CCM is completely against grand corruption and this is clearly stated in its policies and ideology,” said Sendeka.

Sources have several times linked Masha to IMMA, whose ventures involving Deep Green Finance has drawn the law firm to the centre of the much debated Meremeta scam.

For over one year now, the opposition camp in the House has been demanding a special audit of Meremeta and the other companies over allegations of the illegal transfers of 215bn/- from the central bank through, Deep Green Finance using accounts operated in the NBC Corporate Branch in Dar es Salaam as well as South Africa’s NedBank.

The opposition wants the Controller and Auditor General to carry out a professional study on the companies, along the lines applied in auditing BoT’s external payment arrears (EPA) account in 2005/06 to check the alleged transfer.

Citing the relationship between IMMA and the defunct Deep Green Finance of South Africa, Minister Masha said his firm provided legal services and was paid for that.

“IMMA provides legal services to various clients both local and international. It is unfair to link our firm with any wrongdoing or misconduct on the part of some of our clients,” he was quoted saying.

Deep Green Finance was among 22 companies receiving payments from the BoT saga, cited in an audit report on the BoT External Payment Arrears (EPA) account to have received Sh8 billion.

Media reports said company records at Brela, the company registration agency, listed advocate Protace Ishengoma and Stella Ndikimi as Deep Green Finance directors, with Ishengoma being one of the partners at IMMA.SOURCE: THE GUARDIAN
 

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
1,195
Hivyo Sisi watanzania tunakwenda wapi?? Masha ana kila wajibu wa kujiuzulu kama waziri wa mambo ya ndani..
 

Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,587
2,000
Hivyo Sisi watanzania tunakwenda wapi?? Masha ana kila wajibu wa kujiuzulu kama waziri wa mambo ya ndani..
mimi hapo ndio nashangaa viongozi wengi waliopatwa na scandal bado wapo madarakani,hivi hii ni kumaanisha kwamba hakuna viongozi wengine bora zaidi ya hawa au?
 

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
1,195
Na ndio maana utasikia kuwa ukifika uchaguzi wanaongea Lugha za upinzani. CCM wanajua madudu yao ya ufisadi na ndio maana unaona bado wapo Madarakani. Hivyo nani ni Mkombozi wa Kweli
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Hawezi kujiuzulu kwani kampuni yake ya IMMA iliwaajiri watoto wawili wa marais, wa muungano na wa Zanzibar. nadhani huyu mtoto wa rais wa Kikwete, Ridhwani kaacha kazi hapo katika jitihada za ku-save the situation.

Kama nchi hii ingekuwa na wapelelezi wenye uadilifu na wanaolinda masilahi ya taifa -- na siyo hawa wanaolinda masilahi ya wakubwa -- wangegundua mkondo wa hizi pesa za Deep Green. Kuna madai kwamba ndizo zinaendesha Clabu ya Yanga kwa kupitia Ridhwani-Manji.

Hivyo Manji ni kama 'front' tu katika suala la ufadhili wa klabu hiyo (inayoshabikiwa vikali na JK) na amelazimika/amelazimishwa kutumika ili alinde mazito yake -- ya NSSF na mengineyo kuhusu biashara/dili zake za kifisadi na serikali.

Kwa hivyo sababu ya Masha kuula uwaziri, tena unaoshughulikia masuala ya jinai inajulikana -- na watu kama kina Manji, Kagoda n.k. kamwe hawawezi kutinga mahakamani.
 

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
1,195
Hawezi kujiuzulu kwani kampuni yake ya IMMA iliwaajiri watoto wawili wa marais, wa muungano na wa Zanzibar. nadhani huyu mtoto wa rais wa Kikwete, Ridhwani kaacha kazi hapo katika jitihada za ku-save the situation.

Kama nchi hii ingekuwa na wapelelezi wenye uadilifu na wanaolinda masilahi ya taifa -- na siyo hawa wanaolinda masilahi ya wakubwa -- wangegundua mkondo wa hizi pesa za Deep Green. Kuna madai kwamba ndizo zinaendesha Clabu ya Yanga kwa kupitia Ridhwani-Manji.

Hivyo Manji ni kama 'front' tu katika suala la ufadhili wa klabu hiyo (inayoshabikiwa vikali na JK) na amelazimika/amelazimishwa kutumika ili alinde mazito yake -- ya NSSF na mengineyo kuhusu biashara/dili zake za kifisadi na serikali.

Kwa hivyo sababu ya Masha kuula uwaziri, tena unaoshughulikia masuala ya jinai inajulikana -- na watu kama kina Manji, Kagoda n.k. kamwe hawawezi kutinga mahakamani.
Kuna Madai kuwa Mzee wa Kaya ametoa hata Majaji toka katika IMMA na kwenda mahakama kuu, sasa unategemea nini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom