Wakili maarufu, Dancan Oola aporwa bastola na majambazi. Polisi yawadaka gesti

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watuhumiwa wawili Sugu wa Ujambazi wanaotuhumiwa kumpora silaha aina ya Bastola mwanasheria maarifu wa kujitegemea jijini Arusha Dancan Oola Mkazi wa Mbauda jijini hapa.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoani hapa,Jonathan Shana,watuhumiwa hao ambao ni wachimbaji wadogo wa Madini katika Machimbo ya Mererani , aliwataja kwa majina kuwa ni Jumanne Mwalukwa (24) na Ally Khatibu ambao wote wakiwa wakazi wa Mererani Mkoa wa Manyara.

Alifafanua kwamba watuhumiwa hao walipora silaha hiyo Mei 19 mwaka huu nyumbani kwa Wakili huyo eneo la Mbauda jijini Arusha na kwenda kujifisha katika nyumba ya kulala wageni ya Songambele iliyopo katika mji mdogo wa Mererani.

Kamanda alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Jana majira ya jioni katika nyumba hiyo ya kulala wageni ya Songambele iliyopo katika mji mdogo wa Mererani, baada ya polisi kupata taarifa za kiintelijensia.

Kamanda aliitaja Bastola hiyo kuwa ni aina ya Browning yenye Namba B0990 ambapo Polisi walifanikiwa kuipata mikononi kwa watuhumiwa hao.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili pindi upelelezi utakapokamilika


IMG-20190611-WA0076.jpeg
 
Kamchongo kujisafisha lini washawahi kukamata jambaz? utasikia wamewaua na kuwabambika silaha zao za kwenye maghala yao.
Mbinu nzuri sana.
1. Zinawatisha wengine walio na michongo ya namna hiyo.
2. Kujisafisha ili raisi au Waziri akuone mchapakazi.
 
Back
Top Bottom