Wakili Kibatala na Mbunge Hawa Mwaifunga wazua mvutano mzito Mahakamani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,043
Mvutano mkali umeibuka baina ya Kiongozi wa jopo la mawakili wa Chadema, Peter Kibatala akimhoji mlalamikaji wa 11, Hawa Mwaifunga katika kesi ya wabunge 19 wa Viti Maalumu waliofukuzwa uanachama na chama hicho.

Mvutano huo umetokea wakati Kibatala akimhoji Mwaifunga kuhusiana na muhtasari wa Chadema wakati wa Baraza Kuu wa Mei 11, 2022 lilipokaa kuamua rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Novemba 27, 2020 uliowavua uanachama.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa ambapo mlalamikaji wa 11, Mwaifunga ameendelea kuhojiwa na mawakili wa Chadema kuhusiana na ushahidi wake aliouwasilisha mahakamani kwa njia ya kiapo.

Hata hivyo, mahojiano baina yao yamekuwa ni makali, kutokana na kila upande kushikilia masimamo wake, jambo ambalo limemlazimi Jaji Cyprian Mkeha kuingilia kati kwa kutoa mwongozo ili kuwezesha mwenendo wa kesi hiyo kusonga mbele.

Wakati Wakili Kibatala akimtaka Mwaifunga ajibu maswali yake kwa mujibu wa muhtasari huo, Mwaifunga alikuwa akijibu kwa jinsi anavyojua akidai kuwa anachokijibu ndio uhalisia wa kilichotokea siku hiyo na kwamba huo muhtasari ni maelezo ambayo yaliandikwa tu baadaye na Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika.

Baada ya kuzungushana kwa muda kuhusu suala hilo, Jaji Mkeha ameingilia kati na kutoa mwongozo akisema kuwa kwa namna hali ilivyo haitakuwa rahisi pande hizo kukubaliana kwa kuwa kila upande unashikilia msimamo wake.

Jaji Mkeha amemshauri Mwaifunga kujibu tu maswali kulingana na anavyoulizwa hata kama hakubaliani na muhtasari huo akisema kwamba jibu lake halitamaanisha kuwa anakubaliana na kila kitu katika muhtasari huo.

Pia, Jaji Mkeha amemwondoa Mwaifunga wasiwasi kwamba maswali hayo anavyoulizwa na wakili Kibatala si nafasi yake ya mwisho kwani bado anayo nafasi ya kutoa ufafanuzi wakati atakapoongozwa na Wakili wake.

Baada ya Wakili Kibatala kumaliza kumhoji Mwaifunga, Kiongozi wa jopo la mawakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya ameomba ahirisho fupi kabla ya kuendelea na mahojiano ambapo atamwongoza mbunge huyo kutoa ufafanuzi wa majibu yake aliyoyatoa wakati akihojiwa na Wakili Kibatala.

Wabunge hao akiwemo Halima Mdee ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), na wenzake 18 wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama, kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Hata hivyo jopo la mawakili wa Chadema likiongozwa na Kibatala liliomba mahakama na ikaridhia na kuwaamuru wabunge hao wanane kati yao akiwemo Mdee wafike mahakamani kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano kuhusiana na ushahidi wao waliouwasilisha kupitia viapo vyao (malalamiko yao).

Mwaifunga ambaye aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Bawacha ni mlalamikaji wa pili kuhojiwa na mawakili hao wa Chadema kuhusiana na ushahidi wake huo wa kiapo, akitanguliwa na aliyekuwa Katibu wa Bawacha, GraceTendega.

Wengine walioitwa kuhojiwa ni Mdee, Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, na Cecila Pareso.

Katika kesi hiyo wanapinga uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema wa Mei 11, 2022, kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu wa Novemba 27, 2020 kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama.

Hivyo wanaiomba mahakama itengue mchakato na uamuzi huo, iamuru Chadema kutimiza wajibu wake kisheria, yaani kuwapa haki ya kuwasikiliza na itoe zuio kwa Spika na Nec kuchukulia hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapoamuriwa.

Mbali na Chadema kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wadaiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye pia anasimama niaba ya Bunge la Tanzania na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
 
Hii kesi itatoa somo kubwa kwa siasa za nchi yetu.

Hitaji la mgombea binafsi naliona kupitia kesi hii
 
Kuna msemo kwamba ukitaka kushinda majibizano yoyote kuwa mtu wa kuuliza maswali mazito kwa usahihi badala ya kuzungumza kwa u bila kukurupuka.
 
Nilidhani ungetuwekea hayo mahojiano na sisi tuone hayo mabishano makali kumbe ni story tuu..
 
Hii kesi itatoa somo kubwa kwa siasa za nchi yetu.

Hitaji la mgombea binafsi naliona kupitia kesi hii
Ukiachana na Halima na Esther Bulaya, kuna mwingine kati yao mwenye ushawishi wa kushinda popote kama angegombea kama mgombea binafsi?
 
Kuna msemo kwamba ukitaka kushinda majibizano yoyote kuwa mtu wa kuuliza maswali mazito kwa usahihi badala ya kuzungumza bila kukurupuka.
 
Ukiachana na Halima na Esther Bulaya, kuna mwingine kati yao mwenye ushawishi wa kushinda popote kama angegombea kama mgombea binafsi?
Siasa ni kujenga uwezo na uthubutu.

Hatujawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki hivyo nina uhakika wapo hapo wanaoweza kushinda
 
Hii kesi itatoa somo kubwa kwa siasa za nchi yetu.

Hitaji la mgombea binafsi naliona kupitia kesi hii
Mgombea binafsi na viti maalum mbona havina connection unless useme 2025 akina Mdee wanahifia kupotea kisiasa bila kuwa na fursa ya kugombea ubunge.
 
Mgombea binafsi na viti maalum mbona havina connection unless useme 2025 akina Mdee wanahifia kupotea kisiasa bila kuwa na fursa ya kugombea ubunge.
Yes havina connection
Viti maalum siyo demokrasia bali tukapambane kwenye ballot.

Logic yangu ndo hiyo mkuu
 
Back
Top Bottom