Uchaguzi 2020 Wakili Jebra Kambole: Tutazuia uchaguzi kutokana na suala la mgombea binafsi kutofanyiwa kazi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Tumerudi tena African Court @court_afchpr tunadai kwanini Serikali haitekelezi uamuzi wa mgombea binafsi?, Mtikila amepambana mwisho wa siku ameondoka, tunaendelea alipoishia Mtikila. Serikali yatakiwa kujibu kabla ya tarehe 22/10/2020, tutazuia uchaguzi.
1603242331154.png
 
Napata mashaka na hizo hukumu zinazotolewa na mahakama za nje sioni uwezo wake wa ku-enforce hukumu zao ndani ya nchi yetu.

Mtikila alikuwa anashinda hizo kesi mara nyingi tu, lakini mpaka leo sioni lolote jipya, sijui huyo Kambole na wenzake kama wao wataweza.
 
Tumerudi tena African Court @court_afchpr tunadai kwanini Serikali haitekelezi uamuzi wa mgombea binafsi?, Mtikila amepambana mwisho wa siku ameondoka, tunaendelea alipoishia Mtikila.Serikali yatakiwa kujibu kabla ya tarehe 22/10/2020 ,tutazuia uchaguzi.
Alikuwa wapi siku zote?
 
Tumerudi tena African Court @court_afchpr tunadai kwanini Serikali haitekelezi uamuzi wa mgombea binafsi?, Mtikila amepambana mwisho wa siku ameondoka, tunaendelea alipoishia Mtikila.Serikali yatakiwa kujibu kabla ya tarehe 22/10/2020, tutazuia uchaguzi.

Barua ya kwenda Mahakama ya Afrika iko katika akaunti ya twitter ya Wakili Jebra.

Hii timing imekusudia kufanikisha nini kwenye hizi dakika za lala salama?
 
😂
Kwa hiyo tayari kuna mtu Kesha kata tamaa,

Ndowano ya Mabeberu tayari imeishiwa chambo, wanachotaka kufanya ni Hiki tena ambacho ni cha kishama Sana!!
 
Ni kweli alikuwa wapi ,ila mahakamani swali kama hilo sidhani kama linaweza kuwa na nguvu ya kuzuia haki kupatikana /kutafutwa kwani serikali nayo inaweza kuhojiwa ilikuwa wapi kutekeleza amri ya mahakama.
Thank you jebra
 
Napata mashaka na hizo hukumu zinazotolewa na mahakama za nje sioni uwezo wake wa ku enforce hukumu zao ndani ya nchi yetu.

Mtikila alikuwa anashinda hizo kesi mara nyingi tu, lakini mpaka leo sioni lolote jipya, sijui huyo Kambole na wenzake kama wao wataweza.
Uchaguzi Mkuu uendelee isipokuwa mgombea wa urais wa CCM aenguliwe maana Serikali yake ndiyo iliyokuwa madarakani na ndiyo iliyopuuza maagizo ya mahakama ya Afrika.
 
Jebra Kambole kawazidi kwa pamoja "CCM/SERIKALI/NEC/ZEC/BUNGE" akili na maarifa, aliliona hili muda mrefu ila alisubiri kufanya mapingamizi ya kuzuia uchaguzi mkuu ndani ya muda mfupi sana uliobakia kufanyika (Siku 7).

Ninacho kiona, mahakama ya africa iliamuru na itaamuru sheria ibadilishwe kama hukumu ilivyotaka kabla ya uchaguzi huu, kwasababu serikali haina sababu za kujitetea kwa kutotekeleza maagizo ya hukumu ile kwa miaka 9 (Tokea 2011). Lazima sheria ibadilishwe iruhusu mgombea huru, na ndio mchakato wa kutangaza nia na kuchukua form uanze tena upya.

HAPA KUNA MAWILI:

1) Serikali ya jiwe ikubali kuahirisha uchaguzi na kufanya kwanza mabadiliko ya Sheria ya kugombea ili iruhusu mgombea huru kama hukumu ilivyotaka.

2) Serikali ikaidi kwa "MABAVU" kutekeleza maagizo ya hukumu ile ya mahakama ya africa.

La kwanza likitekelezwa, basi CCM wana changamoto kubwa sana katika uchaguzi utakaofanyika baada ya kubadilishwa sheria ya uchaguzi (Sheria itawabana na kuwapunguzia nguvu na wengi watakimbia chama baada ya kukatwa mikia). Serikali pia itakutana na changamoto kubwa zaidi baada ya kutumia tayari mabilioni (Fedha za walipa kodi) kujiandaa vikali na uchaguzi huu na kisha uchaguzi kutofanyika, ukizingatia serikali sasa haina fedha (Serikali itaingia gharama mara mbili kufanyika kwa uchaguzi mmoja, kwa fedha za ndani).

Serikali ikikubali kupokea msaada kutoka mataifa ya nje au UN, basi uchaguzi utakua na usimamizi mkali sana kutoka kwa mataifa ya nje/UN.

La pili, serikali ikikaidi kwa mabavu kutekeleza maagizo ya hukumu, kwa kubadili sheria kwanza ndio uchaguzi ufanyike, kisha ikasema uchaguzi upo pale pale na sheria haibadilishwi. Basi "UMOJA WA AFRICA/UMOJA WA MATAIFA/UMOJA WA NCHI ZA ULAYA/MAREKANI/UMOJA WA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI" watatoka na tamko moja. Tamko litakua "HAWAMTAMBUI RAIS WA TANZANIA".

NB: Serikali itumie busara kwenye hili, akisikilizwa mmoja tu kwa kufuata matakwa yake anayotaka basi ataiponza nchi yetu pendwa.
 
Back
Top Bottom