Wakili Jebra atinga Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kupinga matokeo ya Urais kutopingwa mahakamani

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu, salaam!

Wakili Msomi, Jebra Kambole ameibukia Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu kupinga matokeo ya Urais kutopingwa mahakamani

Katika hoja alizowakilisha, Wakili msomi anaitaka Mahakama iipitie ibara 41 (7) ya Katiba ya Jamhuri wa Muuungano wa Tanzania inayosema “Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake” na kuona kama inakiuka Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu.

IMG_4297.JPG

Ibara ya Katiba ambayo Wakili Jebra ameamua kuiendea Mahakamani

IMG_4298.JPG


Majibu ya Mahakama ya Afrika:

IMG_4299.JPG


My take:
Hii ni move nzuri, tunaita “Strategic Litigation” maana ina maslahi ya wengi.

Tutarajie nini baada ya hapa?
 
Hiyo safi sana.....

Haiwezekani itungwe Katiba ambayo mtu mmoja anafanywa kuwa kama Mungu wa dunia!

Hairuhusiwi kwa aina yoyote ile kumkosoa huyo mtu kwa namna yoyote ile, kwa vile kila anachofanya mtu huyo ni 100% perfect!
 
Katiba hupitishwa Na bunge Na kuridhiwa Na wananchi walioiridhia waliopata wengi yaani majority unapinga bunge Na wananchi walioiridhia?
Hivi wewe umewahi kuona wapi yale yanayopotishwa na Bunge, yanakuja pata ridhaa ya sisi wananchi??
 
Back
Top Bottom