Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Ujinga na umasikini. Ukijitambua huwezi kuwa na akili za kishamba hivo.
Yaani kumcheka kiongozi ni kosa. Wallahi tunapo elekea ni shimoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli kwamba watu wengi sana wana support ujinga huu, hata hapa JF, na watu tukieleza huu ni ujinga tunapingwa kwa cognitive dissonance za kila aina, unaeleza mengi kuhusu kwa nini sisi kama nchi bado tunaelea katika wimbi wa umasikini wa kutupwa.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
22,829
2,000
Unacheka , unaendelea na maisha yako, kujirekodi ukiwa unacheka na kuisambaza hapo itabidi dhamira yako ya kufanya hayo mawili yaani kujirekodi na kuisambaza aingaliwe , je Ni dhamira ovu?

Sent using Jamii Forums mobile app
vichekesho mnavyoviona mitandaoni vna tofauti gani na hiyo picha. Sema mmeshakubali kuwa watumwa wa Jwe. Slaves, umekubali kuwa mtumwa!
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,458
2,000
Marekani, nchi ya makazi yangu, nchi iliyoendelea kiuchumi kwa kupitia figisu nyingi sana na kuweka misingi ya sheria, imejiwekea sheria hivi.

Mimi Kiranga, raia, nikitaka kuchukua picha yako Nyani Ngabu, raia mwenzangu usiye na cheo, halafu niiweke picha ike kwenye T-Shirt. Labda tuseme wewe Nyani Ngabu ni firefighter uneokoa watu, nikiweka picha yako kwenye T-Shirt, ama kwa kuuza ama kwa kuvaa mimi mwenyewe, ama kwa kukusifu, ama kwa kukutukana, wewe una uhuru wa kunishitaki na kunishinda mahakamani nisiweke picha yako. Ukashinda kesi, mimi nifungwe au nilipe faini, na nikatazwe kutumia picha yako.

Kwa nini? Kwa sababu wewe ni private citizen. Una privacy rights kubwa sana.

On the same token.

Nikiamua kuchukua picha ya Donald Trump. Niziweke kwenye T-Shirt. Ama kwa kumsifu, ama kwa kumtukana. Donald Trump na serikali yake hawana haki ya kisheria ya kunukataza.

Nina ruhusa za kuchapisha T-Shirt za kumtukana Donald Trump, nikaweka picha yake na maneno "Donald J. Trump is a douchebag".

Kisheria, hiyo ni sehemu ya free speech tu. Hakuna sheria itakayonikataza.

Raia wa kawaida anatetewa na sheria kuliko rais katika hili.

Kwa sababu, rais alikuwa na uchaguzi, awe raia wa kawaida aachiwe maisha yake yawe private bila figisu na maneno mengi, au atake uongozi, kwa kujua "ukubwa gunia la chawa", pamoja na figisu zote zinazokuja na uongozi.

Akachagua figisu. Hakuchagua privacy.

Sasa keo watu wamemcheka suti msulupwete tu?

Sasa akitukanwa kikwelikweli serikali itaweza kuvumilia?

Tuna umasikini kwa sababu nyingi sana.

Na serikali yenyewe ina ji undermine. Haijui kula na kipofu usimshike mkono.

Sasa wanaendesha serikali kisiri na kujuwekea mazingira ya kuiba mabilioni, watu hawahoji.

Unapoanza kukamata watu wanaomcheka rais kwa sababu ya suti msulupwete, hapo ndipi unaanza kumgusa mkono kipofu unayekula naye.

Wanaiba kura, wanaiba hela, hata kuwaachia uhuru wa msingi tu watu wacheke wasahau machungu wanashindwa?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Right on!

Sisi Watanzania, kwa ujumla wetu, naona hata haki zetu hatuzijui vizuri.

Magufuli ni Rais. Sawa, hilo halina ubishi.

Lakini kimsingi ni mtumishi wetu. Sisi ndo mabosi wake. He is answerable to us, the people.

Mpaka leo hii, kwa mfano, hakuna taarifa sahihi au za kuaminika kuhusu mshahara wa Rais wa Tanzania.

Kuna figures huwa zinarushwa rushwa tu lakini zipo all over the place. It’s like watu huwa wanajitungia tu.

Ukihoji [kama nilivyowahi kuhoji mimi humu takriban miaka 13 ilopita, watu watakuhoji wewe eti unautakia nini mshahara wa mtu. Mshahara wa mtu ni siri yake!!!!

Hapo ndo utaona kuwa pengine tunahitaji kuweka msisitizo sana katika somo la Civics ili tuweze kuwa na jamii yenye watu wanaojielewa na kuzijua haki zao kama raia wa nchi hii.

Maana wakati mwingine inavunja sana moyo kuona watu wakiwa wapole na kukubali kunyanyaswa na kundi la wachache wasio na mamlaka wala haki ya kunyanyasa watu.

Kama kesi zingine za ajabu ajabu zilizowahi tokea katika kipindi hiki cha Magufuli, kesi ya huyo dogo wala haitofika mbali. Itaisha tu kinyemela nyemela maana lengo lao ni kumnyanyasa na kumtia hofu ili asirudie tena.

Ningependa kuona jamii ikikataa unyanyasaji wa raia namna hii toka kwa viongozi.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Unacheka , unaendelea na maisha yako, kujirekodi ukiwa unacheka na kuisambaza hapo itabidi dhamira yako ya kufanya hayo mawili yaani kujirekodi na kuisambaza aingaliwe , je Ni dhamira ovu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kusambaza habari ni haki ya kikatiba.

Kama kitu kinachekesha unatakiwa kuwasambazia wenzako.

Usiwe mchoyo mpaka wa vichekesho.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Ulimbukeni wa mitandao ya kijamii ili kupata likes na views ndio kinapelekea watu ku-share kila kitu.

Inatosha ukicheka na kufurahi binafsi, alichofanya Idris asingeweza fanya kwa baba yake au ndugu.

HOPE>fear
Ulimbukeni ni kutaka kumfunga mtu kwa sababu kamcheka rais.

Tumerudi katika hadithi ya "The Emoeror Has No Clothes".

This time it is "The Emperor Has Baggy Clothes".

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,458
2,000
Hivi comedians wa Tanzania wakiamua kufanya Magufuli Roast itakuwaje?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Hahahaaa mazee....seriously?

Wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua Rais na kui roast nyama yake [kama roast beef] sitoshangaa 🤣🤣🤣.

Maana jamaa ni washamba sana aisee.

Na wewe kuwa mwangalifu usijepews ban humu kwa sababu ya kuzungumzia kum-roast Magufuli.

Waweza shitakiwa for conspiracy to aid and abet in the attempted murder of one JPM and cooking him thereafter in order to consume him for a meal....
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Hahahaaa mazee....seriously?

Wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kutaka kumuua Rais na kui roast nyama yake [kama roast beef] sitoshangaa .

Maana jamaa ni washamba sana aisee.

Na wewe kuwa mwangalifu usijepews ban humu kwa sababu ya kuzungumzia kum-roast Magufuli.

Waweza shitakiwa for conspiracy to aid and abet in the attempted murder of one JPM and cooking him thereafter in order to consume him for a meal....
Haha, eti roast beef.

Mimi nasubiri tu dunia i pick up this.

Kuna kioindi 2Pac alikuwa ana fujo sana, mpaka watangazaji wakawa wanasema "In 2Pac news...". Yani kinakuwa kama ki segment maalum kika mara kinakupa muendelezo wa habari za 2Pac.

Sasa hivi international media itabidi iweke segment ya "In Magufuli news..."

Naona washaanza hapa kwenye link.

No jokes: Tanzania comedian detained over president's over-sized suit | Africanews

Kuna kipindi serikali ilitaka kuifungia JF kwa sababu watu walikuwa wanapaka sana.

Jakaya Kikwete kwa busara zake zote akakataza hilo, akasema msinichafukie image ya nchi dunia nzima.

Serikali ya keo inaelewa image issues, hata kama haijali haki?

Hii issue ilikuwa Tanzania tu, sasa hii kesi itaifanya dunia nzima imcheke Magufuli.

Kwanza kwa suti mswelepwete, pili kwa kutaka kumfunga comedian kwa sababu comedian ni comedian.


Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Magufuli angeweza kumaliza hili sakata kwa urahisi sana.

Angemwita Idris Ikulu, kama raia na mwanawe ki rika and by virtue of tye presidency (Magufuli is 60, Idris is 27), akaongea naye, kisha akatoa statement kwenye TV akiwa anacheka na Idris, akiwaambia Watanzania ukweli tu kwamba, kwa mfano, yeye Magufuli ni mtoto wa wakulima ambaye hakuwa na suti za anasa, hiyo suti aliazima last minute kwa kufanya kazi tu nandiyo maana imempwaya hivyo.

I am sure hiyo suti ina explanation iliyo very interesting. Labda kairithi. Labda alioeea bula kupimwa. Hiyo suti si ya kushonesha kwa vipimo.

Angesema tu kwamba yeye alikuwa anajali kazi kuliko mavazi.

Hilo linge resonate na zaidi ya 90% ya Watanzania, wangemuelewa.

Uhuru wa watu kujieleza ungelindwa, na rais angepangua utani kwa kujichekesha na "mtesi" wake.

Sasa hivi rais kukaa kimya inaonekana kama anafurahia yanayotokea, au yeye ndiye kaagiza.

Kuna wakati pilisi waliraka kunshukia Nay wa Mitego kwa sababu za kijinga hivi hivi, moqka Nay na Magufuli wakaongea ikaonekana kumbe hata Magufuli mwenye hakujali sana hayo mambo.

Mara nyingine hizi ni kesi za "wapambe nuksi" wa Polisi tu.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,458
2,000
Magufuli angeweza kumaliza hili sakata kwa urahisi sana.

Angemwita Idris Ikulu, akaongea naye, kisha akatoa statement kwenye TV akiwa anacheka na Idris, akiwaambia Watanzania ukweli tu kwamba, kwa mfano, yeye Magufuli ni mtoto wa wakulima ambaye hakuwa na suti za anasa, hiyo suti aliazima last minute kwa kufanya kazi tu nandiyo maana imempwaya hivyo.

I am sure hiyo suti ina explanation iliyo very interesting. Labda kairithi. Labda alioeea bula kupimwa. Hiyo suti si ya kushonesha kwa vipimo.

Angesema tu kwamba yeye alikuwa anajali kazi kuliko mavazi.

Hilo linge resonate na zaidi ya 90% ya Watanzania, wangemuelewa.

Uhuru wa watu kujieleza ungelindwa, na rais angepangua utani kwa kujichekesha na "mtesi" wake.

Sasa hivi rais kukaa kimya inaonekana kama anafurahia yanayotokea, au yeye ndiye kaagiza.

Sent from my typewriter using Tapatalk
Sawa kabisa.

Or he can just self-deprecate. He can say that was the shit back then...he looked fly and Janeth fell for him 😂.

More importantly, they can let Idris go [if they haven’t already] and let him be.

No crime was committed there.

And honestly, many of us have photos from way back when that we can look at today and be somewhat embarrassed about or laugh at.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Sawa kabisa.

Or he can just self-deprecate. He can say that was the shit back then...he looked fly and Janeth fell for him .

More importantly, they can let Idris go [if they haven’t already] and let him be.

No crime was committed there.

And honestly, many of us have photos from way back when that we can look at today and be somewhat embarrassed about or laugh at.
Nyerere alivyotoka Scotland alikuwa anavaa vikaptula vyake ambavyo kwa wazee wa pwani vilikuwa culturally inappropriate. Mpaka leo nikienda Zanzibar huku nimevaa cargo shorts wenyeji wangu wananisema navaa kama mtalii.

Tumekubali tu kuwa wakati ule Nyerere alikuwa hajajua kuvaa ilivyotakiwa kwa watu wa Dar.

Alivyojua, aliacha kuvaa vikaptula. Maisha yakaendelea.

Rais Nkurunzinza wa Burundi miaka ya tisini alivaa T-Shirt ya 2Pac ya "Me Against The World". Leo kakua, kaacha.

Wenzetu wanatumia humility kutoa narrative ya "look how far I came". Kuonesha adversities walizozipita na kuweza kufanikiwa despite all odds.

Magufuli angeweza ku narrate hivyo pia.

Miaka kama 17 iliyopita nilikuwa nasoma kitabu cha one of the Rockefellers, David Rockerfeller. Kinaitwa "Memoirs".

David Rockefeller aliandika kitabu hicho kuelezea maisha yake.

Yani jamaa hakuweza kutoa story ya "rags to riches" kwa sababu familia yao ilikuwa matajiri wakubwa tayari wakati anazaliwa. Ila alitafuta adversities alizozishinda ili tu atoe narrative hiyo ya ku overcome something.

Akaelezea story yake kwamba alikuwa na matatizo ya dyslexia, hakuweza kusoma vizuri, kila akisoma alikuwa anaona herufi zinapandiana. Akaeleza jinsi alivyotumia memory na conversation zaidi ya kusoma. Akawa ni kati ya watu wanaoheshimika sana kwa kuwa na memory kubwa sana, akiongea nawe hakusahau hata ipite miaka mingapi. Pia alikuwa na one of the most extensive rolodex miaka hiyo kabla ya computers kuwa mainstream.Ikamsaidia sana kwenye business.

Sasa wenzetu mpaka kina Rockefeller wanajua kutumia hizi narratives za ku humanize na za humility.

Sisi tuna lionize sana mtu, mpaka inakuwa hagiography na upumbavu.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

mpwaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2015
549
500
Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.

Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!

Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Wewe ni nani mpaka umpe into wakati ni boya fokonyolewaji team praise.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.

Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!

Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna hoja nzito zaidi ya Idris na Magufuli.

Kuna hoja za uhuru wa watu kucheka vitu vinavyochekesha katika nchi yao.

Uhuru wa msingi unaotetewa kikatiba unavunjwa.

Kwa hilo, Idris anaonesha mapungufu makubwa sana katika mifumo yetu, mapungufu ambayo yanachangia katika umasikini wetu.

Nchi ambayo wananchi hawaruhusiwi kumcheka rais anayevaa suti msulupwete, rais akiiba hela, wananchi wataruhusiwa kusema rais kaiba hela?

Au wataambiwa kusema hivyo ni kinyume cha sheria na ni kumdhalilisha Mkuu wa Nchi?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
22,897
2,000
Kuna hoja nzito zaidi ya Idris na Magufuli.

Kuna hoja za uhuru wa watu kucheka vitu vinavyochekesha katika nchi yao.

Uhuru wa msingi unaotetewa kikatiba unavunjwa.

Kwa hilo, Idris anaonesha mapungufu makubwa sana katika mifumo yetu, mapungufu ambayo yanachangia katika umasikini wetu.

Nchi ambayo wananchi hawaruhusiwi kumcheka rais anayevaa suti msulupwete, rais akiiba hela, wananchi wataruhusiwa kusema rais kaiba hela?

Au wataambiwa kusema hivyo ni kinyume cha sheria na ni kumdhalilisha Mkuu wa Nchi?

Sent from my typewriter using Tapatalk
Hawa ndiyo wale niliokuambia kuwa wanagandamizwa ila bado wanaunga mkono juhudi za ugandamizaji za wanaowagandamiza!
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Nimeangalia ile sio commedy, alilenga kumdhalilisha Mkuu wa Nchi lazima achunguzwe huwenda kuna mtu anamtumia nyuma ya pazia
Comedy ni nini na kumdhalilisha mtu ni nini?

Na wapi comedy inaisha na kumdhalilisha mtu kunaanza utuambie tuchore mstari, na utuoe sababu umeupataje huo mstari, na kwa nini mstari huo uwe hapo na si pengine.

Kipanya anavyomchora Magufuli na bichwa lililopinda kwa mabonde, anamdhalilisha rais au anakuwa comic tu?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,642
2,000
Hawa ndiyo wale niliokuambia kuwa wanagandamizwa ila bado wanaunga mkono juhudi za ugandamizaji za wanaowagandamiza!
Exposure nayo ni issue.

Kuna samaki wanaogelea katika maji kika siku, hawajui kitu tofauti na maji.

Wameyazoea sana maji, kiasi kwamba sio tu hawajui kitu tofauti na maji, baki hata hayo maji yenyewe wanayaona ya kawaida kiasi kwamba hata hawayatambui kwamba haya ni maji.

Kwa sababu wameyazoea tangu wanazaliwa.

Hawajawahi kuishi katika hangwa la Sahara wakaona sehemu ambayo haina maji ikoje.

Sasa mtu hajakaa nje ya Tanzania, hajasoma vitabu vinavyielezea mambo mazito ya politics, wigo wa dhana na mawqzo yake ni mabishano ya watu kama yeye, tena kwa Kiswahili ambacho ni cha mtaani kisicho na msamiati wala dhana za juu.

Utategemea vioi aelewe kwamba kuminya uhuru wa mawazo kunamuumiza yeye mwananchi?

It is all very abstract kwake.

Kitu immediate kabisa ni self preservation.

Na in some ways mtu huyo atakuwa right.

Lakini, the larger issues remain.

Na kama mtu hana exposure ya kujadili haya mambo kwa kina cha kutosha, ninachofanya ni kumuelewa tu.

Kama victim of circumstances.

Utamlaumu vipi kipofu kwa kutokuona?Sent from my typewriter using Tapatalk
 

Poyongo

Member
Jan 8, 2020
18
45
nyie ma CCM wapuuzi kweli kweli, kama nyie ni waoga msidhan kila mtu ni muoga kama nyie, kuicheka picha tuu eti nako ni kosaa??? duuu yajayo yanafurahisha!
sawa lakini huo ujinga wake akafanye kwa billnas ndo saizi yake sio kwa kiongozi wa nchi jamani
Ile ni dharau kafanya awaeleze police alikua anamaanisha nini mpaka sasa atakua hana hasababu za msingi ndo mana haachiwi alikosa cha kufanya mpaka kumcheka rais kweli? Mbona vitu vya kufanya vipo vingi tu
 
Top Bottom