Wakili Ishabakaki: Idris Sultan anahojiwa kwa kuicheka picha ya Rais

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,716
2,000
1590064195236.png

Mchekeshaji Idriss Sultan wa Tanzania anashikiliwa na polisi tangu Jumanne wiki hii.

Wakili wa mchekeshaji maarufu nchini Tanzania Idriss Sultan ameiambia BBC kuwa msanii huyo anahojiwa na polisi juu ya 'kuicheka picha ya Rais John Pombe Magufuli'.

Kwa mujibu wa wakili Benedict Ishabakaki, japo bwana Sultan hajafunguliwa mashtaka rasmi na polisi, maswali anayohojiwa kufikia sasa yanahusiana na mkanda wa video aliotuma mitandaoni hivi karibuni akionekana akiicheka picha ya zamani ya rais Magufuli.

"Hawajamwambia mpaka sasa kama amevunja kifungu chochote cha sheria...lakini mwenendo wao wa maswali ni kuhusiana na ile video," wakili Ishabakaki ameiambia BBC.

Bw Sultan anashikiliwa na polisi toka Jumanne mchana punde tu alipoitikia wito wa kuripoti kituo cha polisi na mpaka sasa bado hajapatiwa dhamana wala kupandishwa kizimbani.

Wakili wake pia ameiambia BBC kuwa Jumatano jioni polisi walienda kufanya upekuzi nyumbani kwa mteja wake.
"Tunataraji anaweza kuachiwa kwa dhamana hii leo...masharti tuliyopewa ni awe na wadhamini wawili wanaotambuliwa na serikali ya mtaa," amesema wakili Ishabakaki.

Kumekuwa na kampeni katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania ambapo watu kadhaa wakiwemo wanasiasa wa upinzani wa wanaharakati wanatuma ujumbe wa kutaka msanii huyo kuachiwa huru.

Kampeni hiyo inaendeshwa kwa kutumia anuani maalumu ya mtandao ya #FreeIdrisSultan.
 
Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
26,712
2,000
Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.

Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!

Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
4,991
2,000
Nimeangalia ile sio commedy, alilenga kumdhalilisha Mkuu wa Nchi lazima achunguzwe huwenda kuna mtu anamtumia nyuma ya pazia
Hamna haja ya kumuumiza Sana,sisi siyo sadist na Kama sikosei hili kosa lake la pili,nadhani kijana Ana kichwa kigumu bado hajaelewa tuko kipindi gani,apewe onto Kali Sana na akirudia Tena Basi adhabu Kali ya kumfunga adabu ihusike,
Mfano viboko,faini etc
 
Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
16,255
2,000
Washauri wa Idriss sijui ni akina nani! Ile video tokea nilipoiona nilijua itamletea shida, kwa jinsi picha zile za ‘TBT’ za Rais zilivyoenea mitandaoni huku wengi wakifanya dhihaka haikufaa yeye kujifunga kibwebwe kuchekelea waziwazi.

Kwa hili umelivagaa Idriss, umepatikana...
Ni wazi Rais hakupendezwa na dhihaka zile, utayabeba machungu yake wewe mwenyewe!

Ukiponea hili uache kiherehere cha kurukia mambo, cheap stunts zitakuponza!

Sent from my iPhone using JamiiForums
kwa hiyo Jpm hachekwi

Hii nchi kuja kuendelea ni kazi sana kwa mentality hizi

Mkulima wa mahindi
 
Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,591

Seriously! Yaani ni kosa kumcheka Rais? Tena picha ya mtu aliekuja kuwa Rais!!! Seriously?
 
Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
26,712
2,000
kwa hiyo Jpm hachekwi

Hii nchi kuja kuendelea ni kazi sana kwa mentality hizi

Mkulima wa mahindi
Seriously! Yaani ni kosa kumcheka Rais??? Tena picha ya mtu aliekuja kuwa Rais!!! Seriously???
Acheni siasa, ile ni dhihaka na sio vinginevyo. Tupingane na Rais katika mambo ya msingi ila sio kumdhihaki.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
DUMPER

JF-Expert Member
Sep 19, 2017
349
500
Kwani yule anae muiga kuongea na kuvaa kutofauti gani na huyu anae cheka picha ya Rais? Wacheni upumbavu Watanzania kucheka picha ya Rais sio kumcheka Rais.......Labda alikuwa anamchekla fundi aliyeshona hiyo suti ya Rais......Tunarudishwa kwenye ukomonisiti...Wajinga nyie
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
15,952
2,000
Jamani eeh kama hapa ndiyo tulipo tuna kizazi tatizo kidogo.

Kuicheka picha binafsi sioni kama big deal. Wengine wanamchora ana kichwa kibaya na siyo tatizo kwanini hili liwe tatizo?

Ajabu zaidi ni wanapotokea watu wakisema hilo ni kos kubwa sana afunzwe adabu. Yaani, kucheka picha ni kosa kubwa sana ufunzwe adabu.

Jpm akiibuka na akasema haoni tatizo? Itabidi wamuachie. Kisha same people waliosema afunzwe adabu wataside upande wa jpm. Also if jpm will do this atavuna popularity na atatutofautisha sisi na North Korea.
 
Top Bottom