Wakili IPTL aomba kukiri kosa akamzike baba yake

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Dar es Salaam. Mwanasheria wa kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege, ameiomba tena kufanya mazungumzo na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili akiri makosa yanayomkabili na kwenda kumzika baba yake.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 980,000 na kutakatisha fedha.

Mwakandege ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ipange siku ya Ijumaa kwa ajili ya suala hilo kwa kuwa watakuwa wamekamilisha utaratibu wa kufanya mazungumzo na DPP.

"Naomba sana mahakama hii ipange shauri hili siku ya Ijumaa kwa sababu mimi nategemewa kufanya taratibu zote za mazishi,"alidai mshtakiwa huyo.

Shauri hilo lilikuja leo kwa ajili ya kutajwa.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya aliiambia mahakama wametaarifiwa kuwa mshtakiwa huyo anataka kufanya mazungumzo na DPP ili aweze kukiri makosa yanayomkabili.

Komanya alidai kumbukumbu zao zinaonesha mshtakiwa huyo aliwahi kueleza nia ya kufanya mazungumzo na DPP lakini alijiondoa.

"Naomba aeleze mbele ya mahakama hii kama ni kweli ana nia ya kuendelea kufanya mazungumzo na DPP," alidai Komanya.

Baada ya maelezo hayo, wakili wa mshtakiwa huyo, Alex Balomi alidai ni kweli mshtakiwia huyo ana nia ya kufanya majadiliano na DPP kama alivyoomba katika barua yake ya awali.

"Mshtakiwa yupo katika kipindi kigumu cha kufiwa na baba yake mzazi, naomba tufanye haraka ili mshtakiwa aweze kumzika baba yake,” amedai wakili huyo.

Baada ya maombi hayo Komanya alisema: “Sisi tupo tayari kufanya naye mazungumzo hata leo au kesho, hivyo hakuna shida yeyote siku ya Ijumaa tunaweza kukamilisha ili tuweze kumsaidia mshtakiwa aweze kwenda kuzika.”

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alikubaliana na maombi ya pande zote mbili kabla ya kuliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 22,2021.

Mwananchi
 
Dar es Salaam. Mwanasheria wa kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Joseph Makandege, ameiomba tena kufanya mazungumzo na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ili akiri makosa yanayomkabili na kwenda kumzika baba yake.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, alikubaliana na maombi ya pande zote mbili kabla ya kuliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 22,2021.

Mwananchi
Hapa ndipo tulipo fikia. Anaomba akiri makosa sio kwamba ana yakubali ila anatka akamzike Baba yake.. Are we serious!!!!!!!??????
 
Back
Top Bottom