Wakili Emmanuel Muga: Uandishi wa habari kama unafanyika kisawasawa hauwezi ukawa rafiki na Mamlaka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Awamu za serikali zilikuwa na malengo tofauti, mfano wakati wa Mwl. Nyerere vyombo vya habari vilikuwa ni vya ku-promote siasa za ujamaa na kujitegemea hakukuwa na vyombo huru kulikuwa na vyombo vya chama na serikali"- Emmanuel Muga, Wakili.

Alivyokuja Mzee Mwinyi akaruhusu vyombo vya habari kukawepo na vyombo huru, sasa Hayati Mkapa alivyokuja akasema vyombo vya habari haviendeshwi vizuri kwa sababu ya elimu na ndipo hata vyuo vingine vikaanzishwa.

Hizi sheria inabidi mziangalie vizuri, ukileta jinai kwenye sheria za habari maana yake ndiyo tunaona mwandishi ukianzisha YouTube Channel bila leseni unapelekwa Kisutu na unaweza ukapewa hata kesi ya uhujumu uchumi.

Tumeona awamu ya sita Mh Rais kasema hizi Online TV fungulieni, nafikiri wamefungulia bila masharti yoyote, nimemsikia Mhariri mmoja akisema hivi sasa wakimpigia 'source' haogopi kuzungumza hivyo ni mwanzo mzuri.

Bahati nzuri Tanzania hatujawahi kufanya uandishi ambao unaibua mambo, na mambo ambayo yanaibuliwa Tanzania mengi yameibuliwa na Bunge, ile 'serious Journalism' inayoibua mambo tumekuwa tukipwaya kwa muda mrefu.

Uandishi wa habari kama unafanyika kiusawasawa hauwezi ukawa rafiki na mamlaka kwa sababu uandishi maana yake ni kuibua mambo na uwazi na hakuna serikali Duniani inataka vyombo vya habari viwe huru.


East Africa Radio
 
Tazama Tanzania = mwaka mzima linaandika uzushi kuhisu mbowe tu
Janvi la habar.
The echo
Na upuuzi mwingine wa musiba
 
Back
Top Bottom