Wakili Awadh Ali: Uchaguzi wa Zanzibar haupo kisheria

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wakili Awadh,akihojiwa na ITV,amesema kuwa Katiba na Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar haitambui uchaguzi wa marudio.

Wakili Awadh amesema kinachofanywa na ZEC ni kuwashurutisha wanasiasa na wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio hapo Machi 20. Wakili Awadh amesema kuwa washindi wa uchaguzi wa mwaka jana walishapewa vyeti vya ushindi na hivyo hawawezi kupokwa vyeti vyao.

Kuhusu pendekezo la kukimbilia mahakamani kupinga uchaguzi wa marudio,Wakili Awadh amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Katiba haziruhusu kupingwa au kuchunguza ZEC kimahakama.
 
Kuna vituko sana nchi hii

1. Leo Jecha anatoka na vifungu vya sheria, hakuwahi kueleza vifungu vilivyompa haki yeye binafsi au tume ya uchaguzi kufuata uchaguzi

2. Jecha hajatoa kifungu cha katiba kinachoonyesha utaratibu wa uchaguzi wa marudio. Nimeipitia katiba ya ZNZ ya 1984 na marekebisho yote sikuona kitu kinaitwa uchaguzi wa marudio wa nchi nzima isipokuwa wa eneo lenye utata

3. Jecha hajatoa kfungu anachosimama nacho kufuta matokeo.
Alikuja na malalamiko 10 ambayo leo hayaongelei amebaki na la kujitangaza

4. Jecha hajaonyesha kifungu cha kujitangaza kinatoa hukumu gani kwa aliyefanya

5. Jecha anasema majina yatakuwa yale yale bila kutueleza sheria za tume yake na katiba zinasemaje

6. Jecha huyo huyo anayesema wagombea ni wale wale anatoa ulinzi kwa waliokubali kushiriki. Hawa waliokubali kushiriki ni wapi ikiwa majina ni yale yale kama alivyosema hapo juu?

7, Jecha anasema tume itatoa ulinzi. Ulinzi na usalama wa wagombea hautolewi na tume kwasababu si mamlaka yake. Tume inaomba ulinzi kutoka vyombo husika!

8. Jecha aliwahi kukaririwa na gazeti moja akisema amethibitisha vyama kutoshiriki.
Leo hajarudi kufuta kauli ile anapandikiza nyingine. Jecha anajua anachosema?
 
Kupinga uchaguzi kumezuiwa na kifungu gani?

Nachofahamu ni kuzuia kuhoji matokeo yaliyotangazwa na ZEC kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Hivi mahakama kuu ya Zanzibar haiaminiki kwa kiasi hiki?
 
12688197_1210133665682973_158335613037596739_n.jpg
 
Katiba waliyoiandika 2010 ili kuwakomoa Watanganyika imefanya kazi ya Karma!

They reap what they sow!
Unajishtukia tu ndugu mtanganyika, lengo la katiba ile ni kuwaunganisha wazanzibar na kuondoa uhasama na chuki baina yao,hilo limefanikiwa kwani wazanzibar kwa umoja wao tarehe25-10-2010 waliandika historia mpya kwenye siasa za zanzibar,kwa vile mkoloni mtanganyika hakupendezwa na umoja huo amekula njama kuvuruga uhusiano mwema wa wazanzibar,lengo la mkoloni ni kuturejesha tena kwenye siasa za kizamani ili apate fursa ya kuendelea kuitawala zanzibar ila kwa sasa imekuwa ngumu kwani wazanzibar wameshaamua.
 
Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Wakili Msomi Awadh Ali amesema kuwa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar haupo kisheria. Wakili Awadh,akihojiwa na ITV,amesema kuwa Katiba na Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar haitambui uchaguzi wa marudio.

Wakili Awadh amesema kinachofanywa na ZEC ni kuwashurutisha wanasiasa na wananchi kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio hapo Machi 20. Wakili Awadh amesema kuwa washindi wa uchaguzi wa mwaka jana walishapewa vyeti vya ushindi na hivyo hawawezi kupokwa vyeti vyao.

Kuhusu pendekezo la kukimbilia mahakamani kupinga uchaguzi wa marudio,Wakili Awadh amesema kuwa Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Katiba haziruhusu kupingwa au kuchunguza ZEC kimahakama.
Kwenye Aya ya mwisho ndipo ulipo uhalali....kwani hata katiba yetu chadema haituruhusu kupeleka mambo ya chama mahakamani....,pili Cuf na CCM wote wakiwa 50/50 ndio walikubaliana vifungu hivyo ikiwamo kuipa tume nguvu kutopingwa kortini..Awadh anajichanganya kwa mujibu wa sheria japo kisiasa anaweza kuwa sahihi ikiwa kutafikia muafaka wa pande mbili.
 
Kuna vituko sana nchi hii

1. Leo Jecha anatoka na vifungu vya sheria, hakuwahi kueleza vifungu vilivyompa haki yeye binafsi au tume ya uchaguzi kufuata uchaguzi

2. Jecha hajatoa kifungu cha katiba kinachoonyesha utaratibu wa uchaguzi wa marudio. Nimeipitia katiba ya ZNZ ya 1984 na marekebisho yote sikuona kitu kinaitwa uchaguzi wa marudio wa nchi nzima isipokuwa wa eneo lenye utata

3. Jecha hajatoa kfungu anachosimama nacho kufuta matokeo.
Alikuja na malalamiko 10 ambayo leo hayaongelei amebaki na la kujitangaza

4. Jecha hajaonyesha kifungu cha kujitangaza kinatoa hukumu gani kwa aliyefanya

5. Jecha anasema majina yatakuwa yale yale bila kutueleza sheria za tume yake na katiba zinasemaje

6. Jecha huyo huyo anayesema wagombea ni wale wale anatoa ulinzi kwa waliokubali kushiriki. Hawa waliokubali kushiriki ni wapi ikiwa majina ni yale yale kama alivyosema hapo juu?

7, Jecha anasema tume itatoa ulinzi. Ulinzi na usalama wa wagombea hautolewi na tume kwasababu si mamlaka yake. Tume inaomba ulinzi kutoka vyombo husika!

8. Jecha aliwahi kukaririwa na gazeti moja akisema amethibitisha vyama kutoshiriki.
Leo hajarudi kufuta kauli ile anapandikiza nyingine. Jecha anajua anachosema?
Kama katiba ya 2010 iliyoridhiwa na CCM na CUF inaipa tume kinga kutohojiwa uamuzi wake mahakamani....hamna namna zaidi ya CUF kushiriki marejeo ya uchaguzi,kumbuka katiba ya chadema hata ikitokea mbowe na viongozi wengine wamekuonea mahakama haiingilii na utaishia kufukuzwa uanachama....kisheria CUF hawana chao japo wanatumia haki ya kikatiba kutowa maoni.
 
Kwenye Aya ya mwisho ndipo ulipo uhalali....kwani hata katiba yetu chadema haituruhusu kupeleka mambo ya chama mahakamani....,pili Cuf na CCM wote wakiwa 50/50 ndio walikubaliana vifungu hivyo ikiwamo kuipa tume nguvu kutopingwa kortini..Awadh anajichanganya kwa mujibu wa sheria japo kisiasa anaweza kuwa sahihi ikiwa kutafikia muafaka wa pande mbili.
Kinga imepewa tume na sio jecha,sasa jiulize je tume ilikaa kikao gani kufuta uchaguzi ulio kamilika?
 
Kusema tu "haupo kisheria" hakuufanyi usiwepo kisheria. Haitoshi tu kusema 'haupo'. Kama kuna ulazima wa kwenda hata mahakamani ili angalatu tuone watu wametafuta haki.
 
Mkuu,suala linapopelekwa mahakamani,hupelekwa chini ya kifungu mahususi cha Katiba au Sheria. Hakuna kifungu kinachoruhusu suala la kiuchaguzi kupelekwa mahakamani kwa uchunguzi au uamuzi.
 
Kama katiba ya 2010 iliyoridhiwa na CCM na CUF inaipa tume kinga kutohojiwa uamuzi wake mahakamani....hamna namna zaidi ya CUF kushiriki marejeo ya uchaguzi,kumbuka katiba ya chadema hata ikitokea mbowe na viongozi wengine wamekuonea mahakama haiingilii na utaishia kufukuzwa uanachama....kisheria CUF hawana chao japo wanatumia haki ya kikatiba kutowa maoni.
Kinga ya tume inapata uhai kwa kufuata taratibu na sheria,kama taratibu na sheria hazifuatwi zinakiukwa basi moja kwa moja kinga hiyo haina nguvu kwa tume na ndio maana wanasheria wanauita uamuzi wa jecha ni uhuni kwa sababu haujafuata sheria.
 
Back
Top Bottom